Ujumbe wa Leo: Vikundi vya kutetea na kulinda watu binafsi ndani ya CCM ni bomu hatari kwa maslahi ya CCM. Vikemewe kwa nguvu zote

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Nimetazama bwana mmoja kwenye mitandao ya kijamii akijinasibu kama ni mtetezi wa Mwenyekiti wa CCM na Mwenezi Makonda na ameenda mbali zaidi kutishia wote wanaomsema Mwenyekiti na Mwenezi Makonda kwamba atazaa nao kwa mdomo.

Kauli alizotoa zimetafakarisha wenye kuifahamu misingi ya CCM. Tangu enzi na enzi CCM imejengwa katika misingi ya kukosoana kwa hoja na kuvumiliana. Kauli ya kutishia watu kwamba utazaa nao wanapomkosea Mwenyekiti wa CCM hii sio kaliba ya Mwenyekiti wala ya CCM bali ni bomu linalotegwa makusudi.

Inasikitisha sana vikundi hivi vinapata nguvu kubwa ya kukiharibu Chama na kuleta mgawanyiko ndani ya CCM. Kauli huumba kitu kamili, je kama kilichosemwa na huyo anayedai atazaa na yeyote anayemkosoa Mwenyekiti wa CCM ni mwanzo wa kuumbwa kwa mambo ya aibu , Chama kitaweka wapi uso wake?

2025 sio mbali na haya makundi ya kulinda watu ndani ya Chama yanapata kuzaliwa Kila leo bila hatua madhubuti makundi haya yanaweza kuleta mgawanyiko mkubwa. Tuyakemee kwa nguvu zote makundi haya ,hapa ndio tunaweza kujenga umoja na mshikamano ndani ya Chama.

Mwenezi wa CCM, jukumu lako Kwa Sasa kubwa ni kuleta mshikamano ndani ya Chama. Vikundi vyenye mrengo wa kutisha watu wenye mawazo mbadala au tofauti na wengine ndani ya CCM vipige marufuku, vitenge mbali na uwepo wa CCM, hii ni kwa maslahi ya CCM.

Viongozi wa CCM , Sasa ni muda wa kukemea vikundi vya kutetea watu binafsi na maslahi ya watu binafsi ndani ya CCM .
 
CCM ni laana.
CCM ni takataka.
CCM ni mhimili wa maovu yote nnchini.

Ukila nyama ya binadamu,hutakaa uache kuila.
Walipokuwa wanafanyiwa hivyo wapinzani na hao makundi yenu ya CCM,mlikuwa mkishangilia.

Sasa leo imeanza kula upande wenu,mnaanza kupiga kelele.

Shetani hajawahi kuwa na urafiki.
Malizaneni.
 
Back
Top Bottom