Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,913
Hapo juzi waziri wa mambo ya nje wa Urusi ,Lavrov akiwa New York alikumbusha kwa masikitiko mengi kuwa Marekani wakisaidiwa na Uiengereza sasa hivi wako vitani rasmi na taifa lake la Urusi.
Kauli yake hiyo inazidi kuungwa mkono na misimamo ya Marekni pamoja na matamshi yao ambapo Rais Biden alipokutana na Zelensky huko huko New York na katika kuhitimisha maamuzi ya kuipatia Ukraine makombora ya ATAMCS, amesema Ukraine sasa inabidi iipige Urusi kwenye maeneo yake ya ndani ndani.
Mizinga ya ATACMS yaliyoombwa na Ukraine kwa nguvu yana uwezo wa kupiga mpaka maili 190 ndani ya Urusi kutoka mipaka yake.
ATACMS ndiyo iliyotumika mwaka 1991 wakati Marekani ikiipiga Iraq kuyafikia maeneo ya mbali ya Iraq kulikokuwa na vituo vya gharama vya nchi hiyo ya kiarabu.