Antony Blinken yuko mjini Kyiv kwa mazungumzo baada ya mashambulizi ya Ukraine kwenda polepole kuliko ilivyotarajiwa

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,314
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili Kyiv Jumatano kwa ajili ya mikutano na maafisa wakuu wa Ukraine, akiwemo Rais Volodymyr Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje Dmytro Kuleba.

Safari yake inakuja baada ya mashambulizi ya Ukraine kwa Russia (Counteroffensive) yakienda polepole kuliko ilivyotarajiwa.

Blinken pia anatarajiwa kutangaza zaidi ya dola bilioni 1 za ufadhili mpya kwa Ukraine, kulingana na afisa mkuu wa Idara ya Mambo ya Ndani.

Kyiv ililengwa na makombora ya Urusi usiku kucha, ambayo yalizuiliwa, kulingana na utawala wa kijeshi wa jiji hilo.

CNN
 
Hicho ndiyo siku zote Marekani anakipenda. Kutengeneza migogoro ya vita duniani kote! Na mwisho wa siku anawaletea silaha za makampuni yake kwa masharti magumu.
 
Hicho ndiyo siku zote Marekani anakipenda. Kutengeneza migogoro ya vita duniani kote! Na mwisho wa siku anawaletea silaha za makampuni yake kwa masharti magumu.
Kati ya urusi na Ukraine nani aliyeanzisha vita vya kichokozi sasa marekani anahusikaje wakati urusi ndie aliyeanzisha vita vya kivamizi

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Kuna muda nawaza "hivi hiyo dini ya putin (orthodox) ndiyo inasupport njia ya kutumia vita ili kumlazimisha mtu aliyekataa kuwa mshirika wako kukubali...?..🤔🤔

Haya sasa kaua 16 na majeruhi zaidi ya ishirini ndani ya usiku mmoja,

Je orthodox wana Biblia tofauti na madhehebu mengine ya kikristo au ni geresha tu huko kwenda kwake kanisani??
 
Hicho ndiyo siku zote Marekani anakipenda. Kutengeneza migogoro ya vita duniani kote! Na mwisho wa siku anawaletea silaha za makampuni yake kwa masharti magumu.
Kumbe mmarekani ndiye aliyevamia Ukraine...😳😳😳!

Hebu waza kama mtu mzima basi hii ni JF...
 
Utakuwa ni mtoto mdogo bila shaka kwenye masuala ya kisiasa. Na ndiyo maana umeshindwa kutambua chanzo halisi cha hiyo vita ni Marekani na wapambe wake wa NATO.
Wewe ndiyo mtoto....maana hufahamu kuhusu expansionism ya mrusi ndiyo imesababisa hii vita siyo kama wewe ulivyodanganywa kwamba mrusi anataka kujilinda dhidi ya NATO...

Prove me wrong.....mrusi ameisha nyan'ganya ardhi ya kila jirani yake ikiwemo rafiki yake mchina naye mchina akatafuta kibonde wake India, eti hivi sasa ni marafiki 😄😄😄😄
 
Kati ya urusi na Ukraine nani aliyeanzisha vita vya kichokozi sasa marekani anahusikaje wakati urusi ndie aliyeanzisha vita vya kivamizi

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
Rejea kwanza kwenye mapinduzi ya mwaka 2014 nchini Ukraine (Maidan Coup)na ambayo yalifuatiwa na kura ya maoni kwenye eneo la Crimea!

Halafu uone ni kwa namna gani Marekani na nchi za Magharibi zimechangia kwa namna moja au nyingine Urusi kuendesha hiyo oparesheni yake maalum nchini Ukraine.
 
Wewe ndiyo mtoto....maana hufahamu kuhusu expansionism ya mrusi ndiyo imesababisa hii vita siyo kama wewe ulivyodanganywa kwamba mrusi anataka kujilinda dhidi ya NATO...

Prove me wrong.....mrusi ameisha nyan'ganya ardhi ya kila jirani yake ikiwemo rafiki yake mchina naye mchina akatafuta kibonde wake India, eti hivi sasa ni marafiki 😄😄😄😄
Watu hata historia hamuijui! Ila mnajifanya wajuaji. Ungekuwa unafahamu eneo la Crimea kabla ya kupewa kwa Ukraine mwaka 1954 na Rais wa USSR wa wakati huo (Nikita Khruschev), lilikuwa ni eneo halali la Urusi!! Wala usingesema hicho unachosema.

Hayo maeneo yote ya Donbass tangu hapo yalikuwa na wananchi wengi wenye asili ya Urus!! Na hata kwenye awamu zote walizofanya uchaguzi, watu wa Kaskazini mwa Ukraine waliwachaagua wagombea wenye asili ya Ukraine, huku wale wa Kusimi wakiwqchagua wagombea wenye asili ya Urusi!

Sasa unapoanza kuwanyanyasa hao watu, unategemea watakuunga mkono wewe kibaraka wa Marekani, au wataona bora wapate ulinzi kutoka kwa kaka yao Urusi??

Kijana, hapa Historia ndiyo imelala.
 
Hivi ni kwa nn Ukraine hataki kabisa suala la negotiations maana yeye kutwa kucha anapigwa tu lkn hata kirusha jiwe moja ndani ya Urusi hawezi?
 
Back
Top Bottom