Mali hazipatikani kwa njia ya maombi, hawa wafia dini wametupiga
Biblia inaonesha watu wengi waliofanikiwa kutatua shida zao baada ya kumuomba
nenda kasome kitabu cha 1 samuel 2
Kinamzunguzia mwanamke hana alikuwa anatatizo la kushindwa kushika mimba ila alipoomba alipata kushika mimba
Sala ya Hana
1 Halafu Hana aliomba na kusema:
“Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu.
Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu.
Nawacheka adui zangu;
maana naufurahia ushindi wangu.
2“Hakuna aliye mtakatifu kama Mwenyezi-Mungu;
hakuna yeyote aliye kama yeye;
hakuna aliye mwamba kama Mungu wetu
Kitabu cha mambo ya nyakati kinamzungumzia mfalme wa yuda mfalme yehoshefati alivyoweza kushinda vita dhidi ya adui yake aliyekuwa na jeshi kubwa kuliko yeye kupitia maombi mfalme yehoshefati aliposikia jeshi hilo linakuja kumpiga alikusanya watu wakafunga wakaingia kwenye maombi
2 MAMBO YA NYAKATI 20
Sala na ushindi wa Yehoshafati
5.Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa BWANA, mbele ya ua mpya; 6 akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu yeyote kusimama kinyume
Nataka niseme kuwa siri kubwa ya mafanikio ipo kwenye maombi ukiangalia sala za hana na mfalme yehoshefati wote walipitia magumu lakini angalia maombi yao ni tofauti na wakristo wengi leo hii
Maombi yao yamebeba zaidi sifa ,nguvu na utukufu kwa Mungu na sio shida waliokuwa nazo kama ambavyo watu wengi leo hii wanaomba