Ni kweli Simba waliovamia Iringa vijijini wamefika maeneo ya karibu na mjini?

Duduvwili

JF-Expert Member
Jan 31, 2015
3,884
3,807
Nikiwa katika matembezi yangu hapa Iringa Mjini nimepata kusikia habari za uwepo wa makundi mawili ya Simba wanaosadikika kutafuna mifugo katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya Lupembe lwa senga na vijiji jirani

Kama kuna mtu anaweza kuwa labda kashuhudia au muhanga tunaomba taarifa rasmi tujue maeneo haya ya jirani na mjini ni kweli kuna uwepo wa Simba?

Ikumbukwe ni msimu wa mavuno huu watu tunajinywea komoni zilizoiva vizuri kama tulale saa12 tuambiwe jamani!!!

Naambatanisha picha inayosemekana imepigwa kijijini Lupembe lwa senga baada ya Simba hao kuvamia zizi na hicho kingine inasemekana ni kinyesi Cha Simba

Wajuvi mtatusaidia kutuelewesha.

IMG-20230623-WA0003.jpg
IMG-20230623-WA0001.jpg


Soma: Iringa: Mbwa Mayele asifika kusaidia kufanikisha doria ya kuwasaka Simba waliovamia vijiji
 
Huyo aliyesema wapo makundi mawili anaweza kuwa na taarifa zaidi pengine aliwaona kwahiyo Anza na huyo ndiye anajua ukweli
 
Yeah ni kweli hao simba wapo mtaani na taarifa zao zimetolewa wiki moja sasa imepita.
Nilimsikia mkuu wa hifadhi alienda na timu maalum kuwakamata hao simba, sasa sijajua kama walifanikiwa.
 
Nikiwa katika matembezi yangu hapa Iringa mjini nimepata kusikia habari za uwepo wa makundi mawili ya Simba wanaosadikika kutafuna mifugo katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya Lupembe lwa senga na vijiji jirani kama Kuna mtu anaweza kuwa labda kashuhudia au muhanga tunaomba taarifa rasmi tujue maeneo haya ya jirani na mjini ni kweli Kuna uwepo wa Simba?

Ikumbukwe ni msimu wa mavuno huu watu tunajinywea komoni zilizoiva vizuri kama tulale saa12 tuambiwe jamani!!!

Naambatanisha picha inayosemekana imepigwa kijijini lupembe lwa senga baada ya Simba hao kuvamia zizi na hicho kingine inasemekana ni kinyesi Cha Simba wajuvi mtatusaidia kutuelewesha.

View attachment 2666345View attachment 2666348
Haya mazali ya kukutana na simba natamani yanitokee. Yani huo mkono ntakavyoutembeza. Hawa wanyama wapuuz sana na wanakera.
 
Haya mazali ya kukutana na simba natamani yanitokee. Yani huo mkono ntakavyoutembeza. Hawa wanyama wapuuz sana na wanakera.
Dogo unaangalia sana movie za kihindi mpaka unaanza kujiona na wewe ni Sanjey Datey au Mithun. Muda huo ungeutumia kusoma katiba au mkataba wa DP World si ingekusaidia kuchangia wanapoongelea wenzio?
 
Back
Top Bottom