Ni kweli mwenge haukufika kileleni?

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Inasemekana ni kutoelewana kati ya serikali na JWTZ kutokana na serikali kuvunja makubaliano ya awali kuwa jeshi la wananchi ndilo lishughulikie mipango yote ya kupandisha na kuzima mwenge miaka 50 ya uhuru. TBC nao (walisusa?). Tukio la mwenge kufikishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro lilipaswa kurushwa LIVE lakini hata hilo halikufanyika sababu wanazotoa ilitokana na kamera za kituo hicho kushindwa kufanya kazi vizuri katika miinuko ya juu. Hata hivyo, mmoja wa watangazaji wa TBC Sostehes Amas, alionekana kupitia kituo hicho akiripoti kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Hadi leo hakujatolewa hata picha moja ya mwenge ukiwa kileleni.

::Mwananchi
 
hii ya camera kutofanya kazi ktk miinuko ya juu imeniacha njia panda labda kwa mliowahi kukutana na hili mtusaidie.
 
Hah hah,this contry bwana..na camera tena inabagua??mh mh naomba watu wa technohama wanisaidia kama inawezekana kuwa the higher you go the camera resist to work..
 
Serikali iliyozoea kuchekacheka hata kwenye jambo muhimu itachekacheka na kuzisingizia kamera na vingine visivyo na uhai kuwa ndo chanzo cha tatizo...kisha kuchekacheka kutaendelea.
 
Infact kamera zinafanya kazi vizuri zaidi kwenye mazingira ya baridi kuliko joto!.
Picha inayopigwa asubuhi au jioni ni nzuri kuliko picha ya mchana!.

Picha ya Arusha ni mzuri kuliko picha ya Dar na picha ya juu ya mlima ni nzuri kuliko picha ya chini ya mlima!.

Kama ni kweli hakuna picha yoyote ya mwenge iliyopigwa ulipofika kileleni, then hii ni issue!.

Wangeweza hata kutupigia hoax ya huo mwenge popote ulipoishia na kuja kutuonyesha mwenge huo umetinga kileleni, wangapi wanakijua hicho kilele?. Tena kama wangekuwa wenzetu hadi sign board ya Gilman's Peak tungeisoma!.

Kwa vile significance ya Mwenge wa Uhuru doesn't exisit anymore hata huo mwenge ungefika huko, so what?.
 
Kamera ya miaka 50 iliyopita ilipiga picha kileleni, japo si ya video. Leo inakosekana kamera ya video? Sio kweli iko sababu ingine. Labda wapigaji ndio walichemsha maana fitness zetu siku hizi mgogoro. Hata mtoto wa Nyirenda anaitwa Foti kachemsha kupanda, mafuta yamezidi mwilini
 
TBC ilionyesha kipindi maalum wakiwa kilele cha mlima kilimanjaro na mwenge wa uhuru niliona labda tuombe warudie


Kuanzia griman point na uhuru peak juu ya kilele cha mlima kilimanjaro ni barufu na baridi negative nilipofika pale juu kamera yangu haikufanya kazi lakini sijui kama kuna uhusiano na hali ya kule juu au la
 
kipindi cha TBC kilikuwa kizuri tu na kilionyesha kila kitu hatua kwa hatua kuanzia kupanda, kileleni na kushuka hadi kupewa vyeti kwa waliofanikiwa kufika kileleni
 
Baada ya mwandishi wa habari wa TBC kushindwa kufika kileleni (aliishia Holombo) kituo cha pili kuelekea kileleni kuna mwanajeshi alichukua jukumu la kuchukua picha japo sio kwa kiwango cha juu. Vituo viko 6 cha kwanza Malangu, mandara, Holombo, kibo, Gilman's na uhuru peak
 
kukosekana kwa picha nzuri kiasi cha kutosha ukisasa wa sasa ni kwa sababu mpiga picha wa TBC hakufika kileleni lakini pia TBC hawakuwa makini kuchagua mtu wa umri mdogo kuweza kuhimiri vishindo vya mlima kilimanjaro mpiga picha hakuwa fit akaishia kituo cha pili kati ya sita
 
kazi ya kupanda mlima kilimanjaro huchukua siku tano na kushuka siku mbili ni jumla ya siku tano ni lazima mtu awe fit na abebe mgongoni chakula chake cha siku tano. chakula hicho kinapikwa kwenye vituo vya mlima huo kama vile mchele, unga, maharage, juice na viatu vya ziada vizito kama nusu kilo kwa ajili ya kuvaa eneo la barafu na nguo zaidi za kuongeza kileleni kwenye barafu. kutoka kituo kimoja hadi kingine ni masaa 8 hadi 10 inahitaji mazoezi ya kutosha na mwili wenye afya
 
kwa hiyo sisi kama nchi hatukufikia climax? Very bad. Tunaujua umuhimu wa climax lakini? Yaani maandalizi yote ya foreplay...?
 
Just a Confusion ... wapo walioona hatua kwa hutua hadi kileleni! Wapo wanaosema haukufika kileleni!

What is the story behind this STORY!!
 
Back
Top Bottom