Mlima Kilimanjaro kuungua sababu ni nini?

Quimica

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,029
1,254
Wakuu habari,

255743689184_status_a332ac2ba8b248c985c29424e972bf58.jpg

Hili suala la mlima Kilimanjaro kuungua limekaaaje? Maana nimeona inavuma. Mlima umeungua jana na mpaka sasa hivi na mimi mwaka juzi nilivyokuwa Moshi uliungua tena bila sababu kujulikana.

Huu mlima ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi sana waliopo Kilimanjaro na Arusha na hata mikoa ya jirani wanapopeleka watalii.

=========

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umezuka katika mlima Kilimanjaro, karibu na eneo la Karanga Camp lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka na jitihada ya kuuzima zinaendelea.

Moto huo ulianza kuonekana jana Ijumaa Oktoba 21, 2022 usiku kutokea Moshi Mjini, ambapo Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi Tanzania (Tanapa), William Mwakilema aliyezungumza na Mwananchi leo Oktoba 22, amesema vikosi vinaelekea kuuzima moto huo.

Taarifa zinaeleza moto huo unawaka ukanda wa Moorland, ambao mimea yake ikishika moto huwa ni mkali na tayari Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) na Hifadhi ya Kilimanjaro (Kinapa) wametuma vikosi kwenda kuukabili.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi jana Oktoba 21, Kamishina wa Uhifadhi kanda ya Kaskazini, Betrita James amesema baada ya kupata taarifa za kuonekana kwa moto huo, menejimenti ya Kinapa ilianza mara kazi ya kukusanya nguvu kazi na vifaa, na tayari timu zimeelekea eneo hilo.

Mbali na timu hiyo, video ambazo zimesambaa katika makundi mbalimbali ya Whatsapp zinawaonyesha baadhi ya waongoza watalii (Guides) na wapagazi (porters), wakijaribu kuzima moto huo kwa kutumia majani ya miti.
Mmoja wa waongoza watalii mwenye uzoefu na njia hiyo, Geness Shirima, amesema kwa kadri alivyojulishwa, moto huo uko karibu na Karanga Camp na Askari wa Kinapa na wadau wengine walikuwa wakielekea huko kushiriki kazi ya kuuzima.

“Ukitoka kituo cha Mweka ndio unaenda Millennium au High Camp halafu ndio Karanga yaani iko kwenye zone (ukanda) moja. Ni eneo liko juu kama urefu wa karibu meta 4,000 hivi kutoka usawa wa bahari.

“Mfano kama chakula cha wageni kinapandishwa huwa kinapelekwa Karanga camp kwa sababu ndio kituo ambacho ni kabla ya kwenda kituo cha mwisho kwenda Summit (kileleni) pale ndio wageni wanapelekewaga chakula fresh”

Amesema moto huo unaonekana kutokea njia ya Mweka kuelekea ukanda wa Moorland wenye vichaka.
“Ndio maana huu moto unakamata kwa kasi sana ni kama umewasha petrol,” amesitiza.

Oktoba 2020, moto mwingine ulizuka katika mlima huo katika ukanda wa nyasi na vichaka na kuteketeza vibanda 15 vya kulala wageni katika mlima Kilimanjaro pamoja na mifumo ya umeme wa jua na miundombinu ya maji taka.

Chanzo: Mwanachi
 
Hii hoja sijui niijibuje..

Kama uliwahi kushuhudia unaungua hebu tuambie ilikuaje kuaje kwanza mkuu maana wengine tupo ziwani huku
 
yawezekana
1. huwa warina asali wanawasha moto kufukisha nyukii wakishapata asali wanasahau kuzima moto
au
2. wakati wa ukame nyasi zinakuwa zimekaukaa, hivyo akipita mangi mmoja akatupa kipisi cha sigara moto unaenea kote
 
Wakati. Wa kiangazii kunakuwa kukavu na inapelekea nyasi na vichaka kukauka ko ikitokea chanzo Cha Moto ni rahisi kuwaka. Na sidhani hio sio volcano maake ingekuwa hio inatanguliwa na tetemeko. Shimboni
 
Mbona hicho kitu huwa kinatokea hasa kwa sisi huku watu wa mabonden lazm kila mwaka upite moto kuunguza nyasi kavu hasa hasa karibu na masika
 
1666428553764.png

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umezuka katika mlima Kilimanjaro, karibu na eneo la Karanga Camp lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka na jitihada ya kuuzima zinaendelea.

Moto huo ulianza kuonekana jana Ijumaa Oktoba 21, 2022 usiku kutokea Moshi Mjini, ambapo Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi Tanzania (Tanapa), William Mwakilema aliyezungumza na Mwananchi leo Oktoba 22, amesema vikosi vinaelekea kuuzima moto huo.

Taarifa zinaeleza moto huo unawaka ukanda wa Moorland, ambao mimea yake ikishika moto huwa ni mkali na tayari Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) na Hifadhi ya Kilimanjaro (Kinapa) wametuma vikosi kwenda kuukabili.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi jana Oktoba 21, Kamishina wa Uhifadhi kanda ya Kaskazini, Betrita James amesema baada ya kupata taarifa za kuonekana kwa moto huo, menejimenti ya Kinapa ilianza mara kazi ya kukusanya nguvu kazi na vifaa, na tayari timu zimeelekea eneo hilo.

Mbali na timu hiyo, video ambazo zimesambaa katika makundi mbalimbali ya Whatsapp zinawaonyesha baadhi ya waongoza watalii (Guides) na wapagazi (porters), wakijaribu kuzima moto huo kwa kutumia majani ya miti.
Mmoja wa waongoza watalii mwenye uzoefu na njia hiyo, Geness Shirima, amesema kwa kadri alivyojulishwa, moto huo uko karibu na Karanga Camp na Askari wa Kinapa na wadau wengine walikuwa wakielekea huko kushiriki kazi ya kuuzima.

“Ukitoka kituo cha Mweka ndio unaenda Millennium au High Camp halafu ndio Karanga yaani iko kwenye zone (ukanda) moja. Ni eneo liko juu kama urefu wa karibu meta 4,000 hivi kutoka usawa wa bahari.

“Mfano kama chakula cha wageni kinapandishwa huwa kinapelekwa Karanga camp kwa sababu ndio kituo ambacho ni kabla ya kwenda kituo cha mwisho kwenda Summit (kileleni) pale ndio wageni wanapelekewaga chakula fresh”

Amesema moto huo unaonekana kutokea njia ya Mweka kuelekea ukanda wa Moorland wenye vichaka.
“Ndio maana huu moto unakamata kwa kasi sana ni kama umewasha petrol,” amesitiza.

Oktoba 2020, moto mwingine ulizuka katika mlima huo katika ukanda wa nyasi na vichaka na kuteketeza vibanda 15 vya kulala wageni katika mlima Kilimanjaro pamoja na mifumo ya umeme wa jua na miundombinu ya maji taka.

Chanzo: Mwanachi
 
Globle warming inachangia na hii ni ukataji wa miti sisi wenyewe sababu ya ujenzi na mkaa. Ujenzi hatuwezi kuulaumu sababu tunahitaji timber ili tujenge na walifanya hivyo dunia nzima na sisi inabidi tuendelee kufanya hivyo mpaka njia mubadala yenye kufikia watu wote vijijini na mijini imefikiwa.
 
Fungu la rescue lifanye kazi, ifike pahala TANAPA wawe na helicopter za kuzimia moto ina maana ulivyoonekana tu wangekua washaudhibiti usiku ule ule
 
Ngoja wenye uzoefu wakusaidie.
Tangu nakua nimeshapanda mlimani kuzima moto mara nyingi Sana lakini Kwa uchunguzi wangu kidogo ni kwamba Kuna fungu kubwa la pesa huwa linatengwa Kila mwaka Kwa ajili ya majanga ya moto Kwa hiyo kinachofanyika ni kuchoma msitu makusudi ili watu wapige pesa na ukizingatia wanakijiji hukamatwa na kwenda kuzima Bure hii nchi mchwa wengi sana
 
Kinapa waache tabia ya kusingizia warina asali kwa sababu huko moto unakowaka mrina asali hawezi kufika huko na pia wapanda mlima wote wanatumua majiko ya gesi narudia Tena kinapa waache tabia ya kuchoma mlima ili wapige ela
 
Kuna jambo la kiutamaduni/kimila pia,kwa mfano msimu huu mvua za vuli zimechelewa kunyesha mpaka muda huu,sasa ulipotokea moto mlima Kilimanjaro nimemsikia mzee mmoja akisema ukiona moto mlimani basi jua mvua zinanyesha.leo pia kuna taarifa kuwa leo mvua zimeanza kunyesha baadhi ya maeneo hususani Dar es Salaam.Mungu ni Mwema
 
Back
Top Bottom