Ni kweli mwanamke huleta baraka katika ndoa

pet geo pet

JF-Expert Member
Jun 30, 2018
461
644
Mimi ni kijana amabaye sijaoa mpka sasahivi ninakaribia 28+ lakini vijana wenzangu katika rika hili wameshao. Kilichonifanya niseme wanawake wana baraka ni maendeleo ya vijana wenzangu walioyapata soon tu baada ya kuoa.

Mwanzo tulikuwa na maendeleo sawa pia hata kipato kikawa sawa kabisa. Ila gap limetokea baada ya kuoa tu wameniacha mbali sana..pia kipato wamenizidi. Tupo sehemu ya madini Geita wao wakienda wanapata dhahabu sana ila Mimi hapana...hata kama tukijaribu kutafuta wote tunakosa ila wakienda wao wanapata.

Sasahivi wana nyumba kubwa tu na nzuri mpaka nawaza sijui nioe pia nakumbuka nilikuwa na mpenzi wangu ingawa hatukufanikiwa kuoana alikuwa ananiambia MME WANGU KAFANYE KAZI UTAPATA TU nikienda kweli nilikuwa napata.

Karibu kwa ushauri sijui nioe tu na mwanamke anabaraka na ridhiki yake katika ndoa?

1628846946613.png
 
Ni kwel kuna baraka zake kama utapata mtu sahihi na wewe kuamua kutulia.

Kwahiyo jipe moyo na mda usije kukurupukia sehemu ambayo sio sahh ukaichukia ndoa
 
Ukiona kijana wa age hiyo anamafanikio na kaoa hana back up ya mama wala baba ujue anatumia ushirikina kwenye mipango yake
 
Mithali 18:22

"Apataye mke apata kitu chema,naye ajipatia kibali toka Bwana"

Kibali ni pamoja na kupata madini mengi,fedha na usaidizi wa Mungu kwenye kazi.

NB:Huu mstari utatimia ukimshirikisha Mungu kwenye kuoa,akusaidie upate kitu chema kwanza,ndipo upate kibali.

Kitu kisipokua chema au ukakurupuka,utaambulia vumbi tu huko kwenye madini.

Kila la heri
 
Mkuu ni kweli kila mwanamke au mwanaume ktk ndoa analeta baraka ktk mahsiano.
-- kama imeandikwa mwanamke ataolewa na mwanamme Mwenye kipato kikubwa,,
basi yeyote atakayemuoa atapata kipato kikubwa.
--kama imeandikwa mwanamke ataolewa na choka mbaya.
Basi yeyoye atakayemuoa ataishia kuwa choka mbaya.

Halikadhalika mwanaume kama imeandikwa ataoa mwanamke Mwenye kipato,
Basi mwanamke yeyote utakayeoa atakuwa na.kipato kikubwa.
-au kama imeandikwa mwanamke ataolewa na masikini basi hata ndoa yake itakuwa hivyo.

Sometimes juhudi zetu za kutafuta maisha zinasababishwa na.mahusiano yetu ya ndoa.

Huwezi ukaamini maneno yangu lakini yana ukweli 100%.
 
Kwa hiyo mkuu unamaanisha maisha yetu yamekuwa programmed? Kama ni hivyo unaweza vipi kumtambua aliyeandikiwa mafanikio?
 
Mimi ni kijana amabaye sijaoa mpka sasahivi ninakaribia 28+ lakini vijana wenzangu katika rika hili wameshao. Kilichonifanya niseme wanawake wana baraka ni maendeleo ya vijana wenzangu walioyapata soon tu baada ya kuoa.

Mwanzo tulikuwa na maendeleo sawa pia hata kipato kikawa sawa kabisa. Ila gap limetokea baada ya kuoa tu wameniacha mbali sana..pia kipato wamenizidi. Tupo sehemu ya madini Geita wao wakienda wanapata dhahabu sana ila Mimi hapana...hata kama tukijaribu kutafuta wote tunakosa ila wakienda wao wanapata.

Sasahivi wana nyumba kubwa tu na nzuri mpaka nawaza sijui nioe pia nakumbuka nilikuwa na mpenzi wangu ingawa hatukufanikiwa kuoana alikuwa ananiambia MME WANGU KAFANYE KAZI UTAPATA TU nikienda kweli nilikuwa napata.

Karibu kwa ushauri sijui nioe tu na mwanamke anabaraka na ridhiki yake katika ndoa?

Mkuu kama umeona tofauti na wewe vuta wako.

N.B: wengine ndio wanakuporomosha so nenda taratibu
 
Back
Top Bottom