Kila umma na zama zinasheria zao na maamrisho yao hata baadhi ya sheria kutoka kwenye Taurati ya Nabii Muusa(upon him pe peace) alipokuwa Jesus(upon him be peace) akaleta mabadiliko kwenye baadhi ya vipengele na yote inatokea kwa hekima ya Mwenyezi Mungu kutokana na sababu mbalimbali anazojua yeye na zinazofahamika wazi.
Maana ya Uislamu ni dini ya kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kutenda kila jambo sambamba na kanuni na sheria alizozibainisha Ktk mwongozo wake .Na miongozo hupewa Manabii na Mitume kama walimu kwa watu hivyo akileta kila mwalimu vyema kumfuata na akija mwengine inatakiwa kumfuata yeye tu mfano hata shule baada ya kupita kipindi na akija Mwalimu mkuu mpya unakuta sare zinadilishwa na baadhi ya taratibu lakini msingi na wa ufundishaji na malengo yanabaki vilevile(kufaulisha wanafunzi)
Na nilivyosema uislamu ni kufuata kwa usahihi
Qu'ran na Sunna sawa sawa ningekuwa Muislamu (aliyejisalimisha kwa Mungu) wa kipindi cha Yesu(upon him be peace)halafu mtu aniulize uislamu ni nini ningesema ni kufuata
Injili na Sunna za Yesu(matendo na kauli) Sawa Sawa Kwa Muusa(upon him be peace) nitasema ni kufuata Taurati na Sunna za Muusa.
Na kila umma unamuongozo wake swala , nguzo na ibada kutokana na Mwenyezi Mungu alivyowapangia ila kiungo kikuu kinachounganisha umma zote za Manabii na kumwabudu Mwenyezi Mungu mmoja pasi na kumshirikisha(mfano kuahidi kisichokuwa yeye na kumpa kiumbe yeyote awe Nabii ,malika nk sifa za Mungu na kumuomba Yeye ) mfano Ibrahim (upon him be peace alivyokua)
View attachment 2312132