Ni kweli Kiarabu ndio lugha pekee ya Peponi?

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,132
34,106
Asalaam Aleykhum warahmatullah Wabarakatul....!

Wadau hasa Waislam (Ndugu katika Imaan) naomba kujuzwa kuwa ni kweli Kiarabu ambacho kilitumika katika Quran iliyoshushwa na katika Hadith ndio pekee itatumika Peponi?

Hii ni kwasababu kuna Ustadh mmoja huwa anasisitiza Waislam waache kusoma lugha zingine na badala yake wasome Kiarabu ambayo ni Lugha ya Peponi

Aidha leo katika ukurasa wa Twitter nikaona Mdau mwingine akisisitiza hilo.
Screenshot_20220731-204338~2.jpg
 
Ha ha ha hizi dinii hizi

Imagine ktk mafundisho ya vitu ambavyo Huwa waislam wanavyo fundishwa ni kwamba lugha ya kiarabu ndio lugha Bora kuliko lugha zote Duniani hivyo basi ni lazima muislam aijue lugha hiyo Kwa sababu ndio lugha Ambayo itatumika kuzungumza siku ya kiama

Na watu Wana Amini Wana weka juhudi na maarifa katika kujifunza lugha hiyo

Masikini hawajui kuwa Wameaminishwa hivyo Ili lugha hiyo ipate kusambaa Kwa wepesi zaidi Duniani na Endapo ikisimbaa na kufika mbali zaidi itakuwa ni rahisi Kwa mataifa ya uarabuni kuweza kujitangaza kimataifa zaidi

Hawajui hata kwenda kuhiji maka ni chanzo cha mapato kwa nchi ya saudi arabia.. watu wanaoenda kuhiji wanachangia pato la taifa la saudi arabia kupitia utaliii wa kidini. Baada ya mafuta Hija ndiyo chanzo cha pili kikubwa cha mapato kwa nchi ya saudi arabia

Every year, the Hajj pilgrimage generates $8 billion and Umrah $4 billion and it is projected to be $150 billion by the year 2022. In the ten years between 2010 and 2019, the average number of pilgrims in attendance was 2.4 million.

Jiulize Mungu gani mbaguzi. Akupe lugha yako ya kabila lako...ila neno lake akuletee kwa lugha ya wengine
 
Ujumbe muhimu kwa waislamu wenzangu na wale wote wanaotaa kufahamu..

Lengo la hii mada si kutaka kujifunza bali ni muendelezo wa yale wanayoyapenda kukashifu uislamu kama mlivyoona comments zao na mleta mada ukichunguza profile yake ni kinara wa sekta hiyo.

Ni vizuri kutambua mada kama hizi ni za kuachana nazo bila kujibu chochote kwani wamefanya swala la dini tu kila mtu anaweza kuwa msemaji bila kuchunguza katumia vifungu vipi na elimu yake kuhusu dini imefika kiwango kipi lakini ikiwa swala la Afya huwezi kukuta kila mtu anatoa ufafanuzi au kuchukua kauli ya mtu yeyote lazima wahakikishe kuwa ni daktari kweli na amesoma hiyo fani.

Ukiapita mbali mada itadoda na lengo lao halitotimia hata ukileta hoja kwa vile wana lengo haitosaidia kitu bali watazidisha kejeli na uzi kuzidi kushika chati
36e321094a4c913e3ec537d8e71510fd.jpg

Nafarijika sana ninapoona waislamu wa Jf tumezinduka hatimaye mada kama hizi tunawaachie wenyewe wakashifu na kutukana wanavyoweza
40564942-tumblr_mx5dd8Z1JP1smyb0ko1_1280.png

UPDATES: kuhusu watu kuzungumza vipi majibu yanapatikana Ktk maneno ya Mtume Muhammad (SwallaAllahu'aleyhi wa salaam) hapo chini ikisisitiza hakutokuwa na mkalimani siku hiyo na kila mtu ataelewa moja kwa moja lugha itakayotumika siku hiyo.
Screenshot_20220802_105943.jpg

Nb:Kuna watu kwa makusudi wanapotosha na kusikiliza uzushi kwa maslahi yao na wakiambiwa haki ndio hii wanabisha .
 
Asalaam Aleykhum warahmatullah Wabarakatul....!

Wadau hasa Waislam (Ndugu katika Imaan) naomba kujuzwa kuwa ni kweli Kiarabu ambacho kilitumika katika Quran iliyoshushwa na katika Hadith ndio pekee itatumika Peponi?

Hii ni kwasababu kuna Ustadh mmoja huwa anasisitiza Waislam waache kusoma lugha zingine na badala yake wasome Kiarabu ambacho ni Lugha ya Peponi

Aidha leo katika ukurasa wa Twitter nikaona Mdau mwingine akisisitiza hilo.
View attachment 2310321
Tutatumia google translation
 
Ujumbe muhimu kwa waislamu wenzangu na wale wote wanaotaa kufahamu..

Lengo la hii mada si kutaka kujifunza bali ni muendelezo wa yale wanayoyapenda kukashifu uislamu kama mlivyoona comments zao na mleta mada ukichunguza profile yake ni kinara wa sekta hiyo.

Ni vizuri kutambua mada kama hizi ni za kuachana nazo bila kujibu chochote kwani wamefanya swala la dini tu kila mtu anaweza kuwa msemaji bila kuchunguza katumia vifungu vipi na elimu yake kuhusu dini imefika kiwango kipi lakini ikiwa swala la Afya huwezi kukuta kila mtu anatoa ufafanuzi au kuchukua kauli ya mtu yeyote lazima wahakikishe kuwa ni daktari kweli na amesoma hiyo fani.

Ukiapita mbali mada itadoda na lengo lao halitotimia hata ukileta hoja kwa vile wana lengo haitosaidia kitu bali watazidisha kejeli na uzi kuzidi kushika chatiView attachment 2310362

Nafarijika sana ninapoona waislamu wa Jf tumezinduka hatimaye mada kama hizi tunawaachie wenyewe wakashifu na kutukana wanavyoweza View attachment 2310366
HAPANA

Hizi mada si zakuacha bali kuziendeleza na zivume zaidi ikiwezekana ziboreshwe ili wengi waelimike na wajue kweli.

Hao waarabu+wazungu kama waliweza kutukana imani za babu zetu kwa kuita ushenzi basi hata hizi imani zao ni ushenzi mtupu na tutaendelea kuzikashifu na kuzichafua mpaka huyo Mungu wenu ajishushe dunian nae tutamchanganya kwa kipigo.

Ukweli mchungu acha watu wafungue akili zao, sio mnawaaminisha vitisho na upumbavu usiotaka kuhojika
 
Back
Top Bottom