Ni kwanini wanawake hung'ang'ania kubaki na watoto baada ya mahusiano kuvunjika?.

Ni kwanini wanawake hung'ang'ania kubaki na watoto baada ya mahusiano kuvunjika?.

Ozone_

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
505
Reaction score
669
Kwa kipindi cha mda mrefu nimekuwa nikisikia na kushuhudia kesi zinazohusu ukwepaji wa matunzo kwa watoto zikiwakabili wanaume baada ya kutengana na wapenzi wao waliojaaliwa kupata mtoto au watoto pamoja.

Wiki mbili zilizopita nilikutana na classmate wangu mmoja, bi dada flani hivi mwenye maringo, alikuwa akilalamika kiwa baba mtoto wake hatoi pesa ya kutosha mahitaji ya mtoto wao hali ya kuwa jamaa ana kazi yenye kipato kizuri. Mimi nikamwambia sasa kama wewe unaona huwezi kumuhudumia mtoto si umpeleke kwa baba yake. Mrembo kajibu kwamba wanaume hawajui kulea watoto.

Kesi kama hizi zimekuwa zikitaradadi katika siku za hivi karibuni.

Hivi ni kweli wanaume hatujui kutunza watoto vizuri au kuna sababu nyingine ambazo zipo nyuma ya wanawake kung'ang'ania kubaki na watoto hali ya kuwa hawana uwezo wa kuwahudumia?
Wenye ujuzi kwenye hili naombeni mawazo yenu...

#If you say yes, am here to stay.
 
Yaweza kuwa hao wanyama, wanweza wahudumia watoto wao
Je huduma ni Financially Pekee ? Je hizo pesa na matumizi hayawezi yakatumwa sehemu mama alipo ? Sababu kama hataki kutuma sehemu alipo mama je wakiwa karibu atatuma ?

Ukizingatia mama ana attachment kwa watoto kuliko baba (on average); Kwahio huenda huyu mama bila watoto karibu yake asipate usingizi wakati baba wala asikose lepe la usingizi...

Ushauri kwa wenye watoto nje kama uwezo upo nyie toeni tu matumizi within reason (at least consciously utaona umefanya your part sio baadae ukaja kujilaumu au kulaumiwa kwamba hata haukunisomesha....


View: https://youtu.be/_cim7dsia6Q?si=h-BUfjpCFt3EkH97
 
Shida sio kukaa nae, tatizo linaanza pale unapoona mwanao ndio chanzo cha mapato.
Kuwapikia, kuwafulia, kuwaogesha, kusafisha nyumba wakichafua, kufua nguo zenye pupu unaweza??

au unategemea ulete mwanamke mwingine ambae akili zenu huwa zinawaambia "naona mwanamke aje kunisaidia kulea" kitu ambacho hakipo.

Au uwabebe uwapeleke kwa dada ako akulelee.
 
Wengi wao hua wanawatumia watoto kama chanzo cha mapato tu,

Mtoto akilelewa na Mama yake kuna chance kubwa sana ya kuja kumchukia Baba yake ila mtoto akilelewa na Baba yake,hawezi kuja kumchukia Mama yake,

Wanawake huwapa sumu watoto,chuki zao kwa ex wao huzihamishia kumfitinisha Baba na watoto wake.
 
Back
Top Bottom