Ni kwanini kiswahili cha Mtwara kiko tofauti na kiswahili cha kawaida?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Heshima zenu wadau zangu,

Kwa sasa nipo mkoani Mtwara ila kinachonishangaza katika huu mkoa.

Ni aina ya lugha ya kiswahili kiko tofauti ninachokijuaa yaani wakati sisi tunapaita Mtwara wao wanaita Ntwara, mtu wao wanasema 'ntuu'.

Sikubali wao ni 'chikubali' au sielewi wao wanasema 'chielewi' hayo ni baadhi ya maneno ninavyowasikia wenyeji wangu wakiongea ila kubwa ni kwanimi kiswahili chao kipo tofauti na kile cha kawaida?.
 
SIO WATANZANIA WALE NI WATU WA MSUMBIJI TUNAWAVUMILIA TU!
 
SIO WATANZANIA WALE NI WATU WA MSUMBIJI TUNAWAVUMILIA TU!
Basi mtwara nayo ni sehemu ya msumbiji tuwape msumbiji sasa natives wa mtwara ni watu gani wakati historia inaonyesha wao ndio mji wao huo ..
 
Lugha zao asili ndizo zinaleta athari au wazungu wanasema mothertongue
 
Tatizo lipo kwako mtoa Uzi, Hukutembea mikoa mbalimbali, Mwanza nao wana kiswahili chao, Arusha,Dar, Sumbawanga,Mbeya,Musssoma,Tanga, nk.,, Kiujumla tembea Uyaone Na ujifunze mengi, Singida pia Hali kadhalika. Hii imetokana na matabaka ya Makabila yalioko Nchini, Pia kumbuka tatizo Kubwa zaidi lililo Pelekea watu kuwa na viswahili visivyo fanana, kumechangiwa sana na Kutopatiwa Elim mapema, watz walidumu ktk Lugha zao za Asili, Hili tatizo pia serekali ya ccm inapaswa kulaumia sana Kw kuwanyima watz Elim tangu mapema, Hivyo taifa limekuwa na watu wasiejuwa kiswahili ,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…