ila cha hawa jamaa kimezidi kuwa tofauti jamani, utafikiri sio watanzania, hata unapo fanya mazungumzo nao kama hujajua uzungumzaji wao huwezi elewa kama ji kiswahili wanaongeaKiswahili cha sehemu yoyote ile kipo tofauti na kiswahili cha kawaida.
Kiswahili chao badoo nafanya tathminibwanuweweee, mi bado sielewi kwanini wapo hivi , yaani kama ndio unakutana na mtu wa mtwara kwa mara ya kwanza na hujajua namna ya uzungumzaji wao basi unaweza sema aio mtz kabisa,
ndio watanzania wa kila mkoa wameadhirika na namna yakuongea kiswahili , ila cha hawa sidhani kama nikiswahili ,
Kwenye kila lugha kuna dialects. Ukienda Pemba kiswahili chao tofauti na cha bara, ukienda usukumani utasikia tunakwendhaga. Kwendhaga siyo standard swahili hivyo ujue hata wewe yawezekana kiswahili chako siyo kile cha darasani.Heshima zenu wadau zangu,
Kwa sasa nipo mkoani Mtwara ila kinachonishangaza katika huu mkoa.
Ni aina ya lugha ya kiswahili kiko tofauti ninachokijuaa yaani wakati sisi tunapaita Mtwara wao wanaita Ntwara, mtu wao wanasema 'ntuu'.
Sikubali wao ni 'chikubali' au sielewi wao wanasema 'chielewi' hayo ni baadhi ya maneno ninavyowasikia wenyeji wangu wakiongea ila kubwa ni kwanimi kiswahili chao kipo tofauti na kile cha kawaida?.
Wacha matusi, weSIO WATANZANIA WALE NI WATU WA MSUMBIJI TUNAWAVUMILIA TU!
Jamaa inabidi alielewe hili,..pengine ndio Mara yake ya kwanza kutoka nje na mahali anapoishi ndio maana anaona tofauti,ila kila kona ya nchi hii ina lafudhi yake.Fanya uchunguzi, kila mkoa wana lafuzi yao kwa sisi ambao tumesafiri mikoa mbali mbali utasikia tu, mfano tunaotoka Arusha tukienda Dar imekuwa ni rahisi sana kutambulika wao wa dar wakija tunajua kabisa ni wa pwani hawa, ukitokea Moshi ah basi wanajua Mangi, kadhalika, akitokea Maswa au ukanda wa Mwanza unajua huyu msukuma ndivyo ilivyo kwa hiyo hakuna haja ya kuuliza kwanini ila akikaa miaka anaanza kupoteza ile lafuzi.
Nkuona ntoto nzuri anny! Karibu kwtu n'ntwara.Ila wanavyoongea ni kama wana kera sana. Wanongea kama watoto
Tatizo lipo kwako mtoa Uzi, Hukutembea mikoa mbalimbali, Mwanza nao wana kiswahili chao, Arusha,Dar, Sumbawanga,Mbeya,Musssoma,Tanga, nk.,, Kiujumla tembea Uyaone Na ujifunze mengi, Singida pia Hali kadhalika. Hii imetokana na matabaka ya Makabila yalioko Nchini, Pia kumbuka tatizo Kubwa zaidi lililo Pelekea watu kuwa na viswahili visivyo fanana, kumechangiwa sana na Kutopatiwa Elim mapema, watz walidumu ktk Lugha zao za Asili, Hili tatizo pia serekali ya ccm inapaswa kulaumia sana Kw kuwanyima watz Elim tangu mapema, Hivyo taifa limekuwa na watu wasiejuwa kiswahili ,,