Ni kwanini habari kubwa ya Amnesty International na Human Rights Watch haikutangazwa na vituo vyote vikubwa vya runinga nchini?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,532
2,000
Habari kubwa nchini hivi sasa ni hizi ripoti za Amnesty International na Human Rights Watch kuionya Tanzania kuhusu mwenendo wake wa kila kukicha, tokea Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015, kupeleka sheria Bungeni za kukandamiza vyombo vya habari, kuziminya kampuni zisizo kuwa za kiserikali na kuvipa wakati mgumu sana kufanya shughuli zake za kisiasa, vyama vya siasa vya upinzani.

Habari hizo zimepata "coverage" kubwa sana katika vyombo vya habari vya nje, kama vile BBC, VoA na Deutsche Welle, lakini nimeangalia vituo vyote vikubwa vya runinga hapa nchini, kama vile TBC na ITV, vyote hapa nchini havikutangaza kabisa hiyo habari.

Tumeshuhudia pia Waziri wa Sheria na Katiba akikiri kupokea ripoti hizo mbili za Amnesty International na Human Rights Watch na kuahidi kuwa wataijibu ripoti hizo kikamilifu.

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi hizi habari hazikuwa na maslahi na nchi yetu, hadi wakuu wa vyombo vya luninga vyote vikubwa nchini kutotangaza habari hizo?

Au ndiyo tuseme kuwa wakuu wa vyombo hivyo vya habari "wametishwa" na watawala ili wasizitangaze habari hizo kubwa zenye maslahi mapana kwa Taifa letu, kuwa vituo hivyo vya luninga vitafungiwa vikitangaza habari hizo?

Tukumbuke kuwa hata enzi za Rais wa zamani wa Zimbabwe, marehemu Robert Mugabe, alitumia sana nguvu kubwa kuvidhibiti vyombo vya habari vya nchini kwake kutotoa habari zozote ambazo serikali hiyo haikutaka zitoke na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona ya nchi hiyo kutengwa na kuwekewa vikwazo na jumuiya ya kimataifa, hali iliyowafanya wananchi wake waishi maisha magumu sana ya kulia na kusaga meno.

Je, watawala wetu nao wamejawa na kiburi cha madaraka hadi kututaka nchi hii nayo ipitie njia hiyo hiyo na "kuvitisha" vyombo vyetu vya habari visitangaze habari zozote hasi na kutaka vyombo vyote vya habari nchini viingie katika mapambio ya "kusifu na kuabudu" hayo mafanikio ya serikali hii ya utawala wa awamu ya tano?

Imenenwa na wahenga kuwa mficha ficha maradhi, mwisho kilio ndicho kitamuumbua!
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,968
2,000
Uhuru wa kupashana habari haupo, sheria za hovyohovyo na vitisho vingi vimetawala,

Kinachopaswa kutangazwa na media zetu nikumsifu mfalme hata kama anatembea uchi.

Serikali isiyotaka kupewa changamoto zozote isiyotaka kuambiwa ukweli wala kukosolewa ni 100% udikteta na hawezi kufanya maendeleo ya kweli.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,532
2,000
Hivi watawala wetu wanawezaje kuziachia habari za "uongo" za kuwachafua viongozi wakubwa wa kisiasa hapa nchini za magazeti ya Tanzanite na washirika wake na kuzipiga "pin" habari zenye maslahi makubwa ya kitaifa za Amnesty International na Human Rights Watch zisitangazwe kabisa kwenye kituo chochote cha runinga hapa nchini?
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,532
2,000
Kwa kutotangaza kabisa habari hiyo ya Amnesty International na Human Rights Watch kwa vituo vyetu vya runinga nchini ndiko kumewapa ushahidi wa "beyond reasonable doubt" kuwa uhuru wa kupashana habari hapa nchini unaminywa kiasi cha kutisha sana.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,867
2,000
Mkuu,

Kila kituo kina code of conduct katika kazi/biashara zake.

Kwani wenye vituo walikuja kukuomba ushauri ili wafungue hivyo vituo vyao vya runinga?

Ni sawa na mtu mwingine amefungua duka lake halafu unaanza kuwahoji wanunuzi kwa nini hauzi bidhaa fulani?

Kama unadhani hauzi hicho unachotaka akiuze, basi fungua duka lako ili uuze. Vivyo hivyo, hata kwenye suala la vituo vya runinga. Kama unadhani hawazitangazi habari unazotaka zitangazwe, basi fungua runinga yako ili uzitangaze!

Samahani kama nitakukwaza na majibu yangu!
 

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
4,237
2,000
Amnesty International na Human Right Watch ni wakina nani? Walianzishwaje na UN ni nani kwa maslahi ya nani? Tuanzie hapo.
 

njinjo

JF-Expert Member
Feb 15, 2019
2,334
2,000
Hivi watawala wetu wanawezaje kuziachia habari za "uongo" za kuwachafua viongozi wakubwa wa kisiasa hapa nchini za magazeti ya Tanzanite na washirika wake na kuzipiga "pin" habari zenye maslahi makubwa ya kitaifa za Amnesty International na Human Rights Watch zositangazwe kabisa kwenye kituo chochote cha luninga hapa nchini??
Kama ulimsikiliza kagame ulipata jibu. Achana na upuuzi huo wa AI
 

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
6,968
2,000
Hizo taarifa nimezipitia juujuu mahali fulani, kwa kweli ni aibu kubwa kwa taifa letu!

Rais Magufuli katufikisha mahali ambapo hatukutegemea kabisa katika nchi hii! Ukandamizaji na ukiukwaji huu usio na aibu tulikuwa tunausikia tu kwa wenzetu!

Mtu huyu anaogopwa kuliko Idd Amin. Wanahabari wanaishia kujikomba na kujichekelesha tu.

Anafanya mambo utafikiri alifanya mapinduzi kukalia hicho kiti!

Tunatakiwa kumwambia inatosha, la sivyo ataivuruga kiasi cha kutorekebishika nchi hii!

Mwalimu alituasa, tuwe tayari kulipa gharama za kuwapinga viongozi madikteta. Hata kama watatuvurumishia risasi kama walivyomfanyia Tundu Lussu.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,867
2,000
MsemajiUkweli,
Umejibu utumbo mtupu

Hivi wewe kada wa Lumumba umezisoma hizo ripoti mbili za Amnesty International na Human Rights Watch, au ndiyo umeamua kubweka tu?
Umepewa akili na macho ili utumie kwa faida yako.

Yaani unaniambia nisome ripoti iliyoandikwa na wageni kuhusu suala ambao ninaliishi.

Ni sawa na mgeni anakuja ndani ya nyumba yako halafu anaandika alichodhani amekiona na kukutaka ukisome wakati wewe ndio unaijua nyumba yako.

Hakuna jipya ambalo silijui. Au wewe unadhani repoti ikiandikwa na wageni hasa wazungu basi ni ya maana sana zaidi ya kile unachokijua?
 

Lucas philipo

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
1,581
2,000
Kwanini BBC na DW tu ndio wachukue coverage? Unadhani huko kwao hakuna human rights violation?

Kwani bila hata hizo organizations sisi hatujui kama kun haki za binadamu hadi wazungu watuambie ?

Je, kwenye hizo ripoti mbona hatujasikia ukandamizwaji na misafara ya waafrika wanaotupwa bahari ya mediterania na hao unaowatetea?

Waafrikq wangapi wanafukuzwa marekani kisa tu ni wahamiaji haramu lakn wazungu wakija huku tunawaita wawekezaji na watalii? Kwanini Afrika? Kwanini Tanzania?

Kama ni ishu ya uhuru na mambo ya demokrasia je kwanini hawatupi ripoti za ukandamizwaji wa demokrasia nchi za china ,Russia na North korea?

Je, matusi anayowapa waafrika Trump na waandishi wa habari au yale hayahusiani kabisa na human rights?

Afrika amkeni, acheni kufugia nywele tu hivi vichwa tulivyopewa na Mwenyezi Mungu.

"We will be free if our minds are decolonized" Ngugi Wa Thiong'o
 

Echolima

JF-Expert Member
Oct 28, 2007
3,784
2,000
@="Lucas philipo,
Na wewe akili yako imefinyiliwa kila kukicha unajiona unaonewa ungekuwa mwarabu wewe ungekuwa Gaidi!!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom