Ni kwanini habari kubwa ya Amnesty International na Human Rights Watch haikutangazwa na vituo vyote vikubwa vya runinga nchini?

Itv nao tulikuwa tunawategemea kupata habari za uhakika ila siku hizi hamna kitu muda wamekuwa waoga kupindukia hili kampuni sio muda litajifia wameshindwa kureport habari

Sio ITV tu, AZAM pia kupotezwa kabisaa

Nani unapenda kupotezwa na wasiojulikana ndugu

DAB na Genge lake clouds nini nimetoka?
 
Kwanini hapo Amnesty International na Human Rights watch wasiipublish hiyo ripoti yao hapa nchini ikiwa content yote inaihusu Tanzania?

Pia kwako mtoa maada, umeonesha kukerwa zaidi na vyombo vyetu kutokuichukulia maanan ripoti hiyo na ukaenda mbali zaidi eti wamehighlight mambo Muhimu na nyeti kuhusu Tanzania, je mambo hapo ni yepi halafu ningependa unambie uhalisia wa hoja zao in real Tanzanian life regarding to social - economic.

Binafsi, bado nawaona Waafrika especially Watanzania wengi wakiwa kwenye dimbwi la utumwa kifikra kiasi cha kuamini kila jambo kutoka ng'ambo bila hata kutumia common sense na kupima uhalisia wake kwa jamii husika.
 
Kagame na wewe amekuwa mfano wa kuigwa??
Mimi naangalia maendeleo ya nchi sijali Democracy! Hata Mwalimu alikuwa mkali ajabu ndio maana nchi ikajengeka. Pamoja na mapungufu ya Magufuli ila kunyamazisha akina Kabendera au Tundu Lissu ni ruksa
 
Kiukweli hali uhuru wa habari ni mbaya mno.

Hizi hadithi nilisikia kitambo kwa wale wanaoenda Rwanda kuwa huwezi kuta wanyarwanda wanamuonge vibaya Kagame.

Sasa hali imekuja bongo yani siku hizi hata ukienda kijiweni watu wanabishania mipira tu.

Ukiingiza habari ya serikali watu kimyaaa.
 
Siasa za vyama zimeharibu kabisa uwezo wa kufikiri wa vijana na hata wazee Tanzania.

Ule uwezo wa watu kufikiri mambo madogo tu umepotea kabisa,sasa watu wanafikiria ndani ya vyama vyao vya siasa,hawatoki nje kabisa na kufikiria wakiwa huru.

Ukisoma baadhi ya majibu katika huu uzi ndio utabaini ni kwakiasi gani watu hawafikiri sawasawa.​
 
@="GKado,
Kibaya ni kwamba unaweza kukuta hamna mtu anayepangiwa taarifa gani atoe ila tatizo ni ile tabia komavu ya watanzania ya kujipendekeza na kujikombakomba.​
 
Zile ni Habari kubwa kwa Mabeberu na watu wa chache wa hapa nchini
 
@="Lucas philipo,
Wewe ni mtukanaji mzuri sana ila bahati mbaya uwezo wako wa kupambanua mambo ni duni, unahoji kama mauhuru watayala huku ukiona madege watayala! Stop, think before you leap.
Kutukana ruksa.
 
@="Mystery,
Mkuu leo naambiwa ni Birthday ya Mheshimiwa hivyo nani anataka kumharibia siku yake (LoL).

Kiuhalisia kitu kama hiki kinaonyesha tulipofika kama nchi kuhusu human rights na utawala bora. Na majibu mengine humu ndani yana akisi hali hii.

Fikiria mtu anasema kwa kujiamini hatuli demokrasia. Mwingine anasema kama hukubaliani na kutotangazwa taarifa hizo basi anzisha vituo vyako.

Kwenye media circles hiyo ndiyo inaitwa self-censorship ambayo ikipita kiasi basi tutapata habari zile za mapambio tu na miziki ya kina Harmonise etc. Tushukuru at least kuna social media kama JF ambamo mambo kama hayo huwekwa wazi.
 
Hapo tu imeshaprove kuwa kilichoandikwa ni kweli. We are moving fast into dictatorship country, unknowingly.
 
@="Mystery, Mtia mada

Amnestry inernational na Human rights watch ni vituo vya kipropaganda kusambaza propaganda za mabeberu na vipo makini sana pale ambapo vinaona mataifa hayo manene hayapati maslahi ipasavyo kwnye haya mataifa bikra hasa ya Afrika na Asia

Jiulize...wakati marekati inawaua wairaki amnestry walisema chochote?

Kule Afghan waarabu walivyochinjwa na mavifaru ya marekan uliiona Human rights watch?

Alupoulizwa na mwandishi wa BBC rais Asad wa Syria kwamba kwa nini serikali yake inawaua watu magerezana na kuyafanya magereza ya syria kua ni kama mabucha????

Asad akamuuliza mwandishi hizo habari umepata wapi?

Mwandishi: Ripoti za amnestry international

Asad:
Amnestry international is an American mouth

They always cook whatever information they want on us

We question the credibility of Amnestry international and other propagandist organs of US on Syrian politics
 
Hivi wewe Lumumba unadhani kama vyombo vya habari vimeminywa ukifungua chako ndiyo utaruhusiwa? Wakati mwengine uwe unatumia kiungo stahiki kufikiri.@ ="MsemajiUkweli,
 
@="Mystery,
Heri lawama kuliko fedheha! Vituo vyote vya hapa nchini vimerusha habari hiyo kupitia mashirika ya kigeni na tumeipata live.
 
Back
Top Bottom