KUNA tunda la pekee ambalo limesambaa ulimwenguni pote. Tunda hilo hutumiwa kama chakula na kinywaji. Na umbo la pekee la mti unaozaa tunda hilo ni ishara ya visiwa vyenye joto. Ni tunda gani tunalozungumzia? Ni nazi-mojawapo ya matunda muhimu zaidi duniani.
Nazi ni kiungo muhimu sana katika mapishi ya nchi na visiwa vyote kuanzia Hawaii hadi Bangkok." Kitabu hicho chasema pia kwamba kwa wakazi wa maeneo hayo "nazi ni lishe muhimu sana maishani . . . katika njia nyingi na hutumiwa sana kutia ladha katika vyakula mbalimbali."
Sababu inayofanya nazi itumiwe sana katika mapishi ya maeneo hayo ni hii: Huwa na maji, tui, na mafuta ya kupikia. Madafu huwa na maji matamu ya kunywa, na mara nyingi huuzwa katika vibanda vilivyo kandokando ya barabara. Na tui hutengenezwa kwa kuchanganya maji na nazi iliyokunwa kisha kukamuliwa. Tui huongeza ladha na uzito kwenye michuzi na unga uliokandwa.
Wakulima hutengeneza mafuta ya nazi kwa kupasua nazi iliyoiva na kuikausha juani. Inapokauka, nyama ya nazi au mbata, inaweza kutolewa kwenye kifuu, kisha mafuta hutengenezwa. Katika maeneo yenye joto, mafuta ya nazi hutumiwa sana kupikia ilhali katika nchi za Magharibi hutumiwa kupaka mikate, kwenye aiskrimu, na biskuti.
CC Mzizimkavu