Ni kiasi gani kinapaswa kuchangiwa kama mchango wa harusi?

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,956
6,887
Habari wakuu, ni katika hali ya kunishangaza leo nimepokea kadi ya mchango kutoka kwa jirani yangu ambae anatarajia kufunga ndoa.

Nimepokea kadi hii na shughuli yao inaonekana inafanyika mwezi ujao, Hii ni kadi ya kwanza napokea ya kuhusu haya masuala toka nizaliwe 23years ago maana nilizoea kuyaona kwa wazazi wangu na watu wengine walionizidi umri.

Hili suala limenifanya nione sasa naanza kuingia kwenye utu uzima wenye majukumu sasa na kwa kuwa sijui chochote katika haya masuala ndo maana nipo mbele yenu kutaka kujua ni kiasi gani minimum cha kuweza kumchangia huyu jirani yangu maana siwezi nikatoa maximum maana we do have no any such bond connection so sihitaji kujitolea sanaa bali kiasi ambacho tu kinafaa kuwa mchango wa shughuli yao hiyo.

Nasoma maoni⬇️
 
Hapana, hivyo vitu siwezi kufanya
Kwenye ile kadi wameandika wanaomba mchango wa "hali" na "mali". Wengi hua tunakimbilia kutoa mchango wa mali (fedha) na kusahau kua hata mchango wa hali unakubalika 😄😄. Mfano unaweza kutoa mchango wa kuwatakia maharusi kila la heri hapo umetoa mchango wa "hali"
 
Elfu tano tu,tena changanya na mashilingi shilingi ya mia mbili na mia mbovu mbovu.
Lengo;WASIKUZOEE
 
Kwenye ile kadi wameandika wanaomba mchango wa "hali" na "mali". Wengi hua tunakimbilia kutoa mchango wa mali (fedha) na kusahau kua hata mchango wa hali unakubalika 😄😄. Mfano unaweza kutoa mchango wa kuwatakia maharusi kila la heri hapo umetoa mchango wa "hali"
Kha!
 
Back
Top Bottom