Ni kheri arudi urais Benjamin Mkapa kuliko uongozi wa Jakaya Kikwete: What does that tell us?

Mambo kuwa hadharan si swala la kumsifu jk hata kidogo huu bado ni udhaifu ndan ya usalama wa taifa. Maana wao ndo wanatoa data hizo , jk ni total failed pia uongozi kwa ujulma yeye c ndo kiongoz anae wateua mbona hawawajibishi sasa sioni jema la jk hata moja

AshaDii,

Mkuu wangu nimekusikia na nimekupata vyema toka mwanzo isipokuiwa tu nimeona mahala kana kwamba unamsifia JK kiaina na kubeza wale wanaosema bora ya Mkapa kuliko JK.. Ndio maana nikasema hakuna cha afadhali wala mbora nani kuliko nani, wote hawa HAWAFAI kwa sababu wote tumbo moja mtu na kaka yake na wote wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao ktk uongozi na wote wameshindwa...

Jambo jingine nashindwa sana kukubaliana na baadhi ya watu wanaosema ati wakati wa Mkapa UCHUMI WETU ULIKUWA...Jamani hizi figure mnazipata wapi? nimewahi kuweka hapa mapato ya Mwalimu vs viongozi wote hawa na uki convert in dollars utaona serikali ilikuwasanya fedha zaidi wakati wa Nyerere kuliko wakati mwingine wowote.. It's somewhere ktk hoja zangu humu JF. Na hatuwezi kuhesabu makuzi ya GDP ikiwa wawekezaji wengi sio wa ndani, fedha haizunguki ndani inakwenda nchi za nje - GDP zenye sura ya ukoloni mamboleo hazina sababu ya kuzitazama.

Nashindwa hata kuelewa watu wanaotaka kuwasifia Mkapa au Jk wakati nchi inakwenda kwa kudra za mwenyezi Mungu sawa na wazee wetu vijijini ambao hakuna Hospital wala zahanati lakini ndio wanaishi hadi miaka 80..Tumshukuru Mungu na kusema Mungu mkubwa kuliweka taifa letu hai hadi leo kwa sababu sii Mkapa wala JK wanaotuweka salama leo isipokuwa sisi wenyewe Watanzania ni watu wa subra ya kupita kiasi kutokana na nidhamu ya woga..

Mkapa hawezi kusifika kwa kuweka mfumo wa ukusanyaji wa kodi zetu wakati ilikuwa ni l;azima afanye hivyo kulingana na utaratibu wa Ubinafsishaji....Haiwezekani nchi itoke ktk Ujamaa ambao serikali inamiliki njia za kuzalisha uchumi ukabinafsisha mali zake pasipo kuunda chombo cha kukusanya kodi hizo toka mashirika binafsi.. Wakati wa Nyerere hapakuwa na haja kubwa ya kukusanya kodi kwa sababu pato la mauzo yote lilikuwa ni mali ya serikali toka mashirika hadi vyombo vya ku export na Import ilikuwa lazima upitie Bank kuu kupata kibali na kubadilisha fedha.

Kwa nchi yoyote unapotoka Ujamaa na Kubinafsisha hizo njia za uzalishaji ni lazima kuwepo na mfumo wa kukusanya kodi kama pato la taifa tofauti na Ujamaa ambao serikali ilikuchukua pato lote, hiyo kodi serikali itajitoza yenyewe?...Ndio maana huwashangaa sana wasomi wanaomsifia Mkapa ktk ukusanyaji wa kodi wakati ni ilimlazimu kufanya hivyo laa sivyo ingechekesha..Ni sawa na mtu alokuwa akitumia usafiri wa Daladala ziku zote hana sababu ya kuwa na road licence au insurance ya gari lakini siku akinunua gari huwezi kumsifia kwa kukata road license na insurance kwa sababu inamlazimu kufanya hivyo ili apate kuendesha hilo gari lake. Lakini wengine pia watasema tunamsifia kwa kukunua gari? Yes kanunua gari kwa sababu daladala zimepigwa marufuku haikuwa maamuzi yake kupiga marufuku daladala. Ooh what if kama Mkapa angeacha kununua gari? then angekuwa mjinga kupita kiasi kwa sababu hana usafiri mwingine!..haaa! haaa! haaa!

Tatizo la Wadanganyika, na hasa wasomi wetu wanahesabu sana makuzi ya kiumri na mwili wa nchi yetu kusifia kama ndio maendeleo ya kiafya!.. 50yrs baada ya Uhuru ni lazima tuwe tumepiga hatua fulani kiumri na mwili wetu tuseme mashaallah Mungu katuwezesha lakini haina maana afya yetu ni nzuri kiuchumi..Hata mtoto anavyokua ndivyo maumbile yake hubadilika na kuwa makubwa, ufahamu wake unapanuka lakini haina maana AFYA yake pia inaboreka. Tanzania kama nchi hatyujawahi kuboreka Kiafya isipokuwa kila mwaka tunarudi nyuma kutokana na pato la taifa linafisadiwa.. Tunajaribu kujaza maji ktk ndoo ilotoboka hivyo hatuwezi kufanikisha chochote..

Haitakiwi kabisa kuchukulia kukua kwa uchumi kwa ujumla wake iwe sababu ya Uongozi bora kwani ukifuata hivyo basi JK ni kiongozi bora zaidi ya Mkapa kutokana na kwamba GDP yake inapanda toka ya Mkapa 2005 Billioni usd 23 hadi sasa hivi tumefika billioni 60 na ushee! - recorded one...Lakini nini pato ktk mfuko wa Taifa?...Tazama bajeti yetu tunazungumzia Billioni 5 (less than 10% ya GDP) hapa umechanganya na misaada ya nje.. Kwa hawa walioendelea hizo billioni 5 ni bajeti ya wilaya moja. Mji wa Toronto una bajeti kubwa (9.2/bil) kuliko nchi nzima ya Tz..

Ni ktk kufikiria makuzi haya ya kimwili ndio maana tunababaika.. wasomi wetu wanashindwa kuelewa kwa nini hatuendelei pamoja na mipango ambayo wao wenyewe wameipitisha through IMF.Lakini ukweli unabakia kwamba Mikataba mibovu ndio sababu kubwa ya kudorora kwa uchumi wetu mikataba aloweka Mwinyi, Mkapa na sasa hivi JK..

Chukulia mfano wa Barricks wameuza dhahabu nje za billioni 300 hii amount itaingizwa ktk GDP yetu..lakini ukweli ni kwamba tulichoambulia ni royalty ya asilimi 1.1 pekee wakati Sinclair dalali mtu mmoja anachukua aslimia 1.9 zaidi ya serikali yetu wenye ardhi na dhahabu yenyewe..Hao Barricks wapo ktk soko huria wapi?..Toronto na New York na makao yao makuu yapo Toronto, Canada. Wameajiri Tanzania wananchi waisozidi 300 sawa na hesabu ya waajiriwa nchini Canada na Marekani ambao wanapokea mishahara mkubwa kuliko wachimbaji na management ya Watanznia..Sasa kama huu sio Ukoloni mamboleo unaweza kunipa mfano bora zaidi ya huu?..Who made the deal tunaambiwa JK na Mkapa..

Mkapa Vs Kikwete
Unapofanya comparison kati ya tawala/uongozi wa watu wawili wa nyakati tofauti ni lazima pia uchgue maeneo ambayo unataka kuwapimia.
Tatizo ni kuwa walalamikaji wengi wapo too general katika malalamiko yao, kama ukiwauliza wakupe maelezo ya kwanini fulani ni bora utashanga mtua anavyoanza kuingia na kutoka, kiasi cha kujipoteza hata yeye mwenyewe kama utamuuliza alipoanzia ili aweze ku-summarize.
Kwa tabia ya mwanadamu na kimazingira si sahihi mtu kusema hakuna mambo ambayo Kikwete ameyaweza, binaadam yeyote ni progressive, inawezekana tabia yetu ya kutoweza kujituma ikawa ndiyo tatizo au tabia yake ya kuwaamini watu ndiyo inamponza.
Binafsi simuoni Kikwete kuwa na tatizo kwa kiwango na mtazamo waupatao wengine juu yake, kwangu matatizo ya JK ni kuwa si hard wala critical thinker, pia ni mtu na mwepesi kuwaamini watu with his life, bahati mbaya watu anaotokea kuwaamini ni wepesi sana kushawishika, hivyo kumuingia yeye ni rahisi zaidi ukitumia watu anaowaamini, kuliko yeye moja kwa moja.
Tatizo hapa ni layer nayomzunguka rais, kama pangekuwa na layer nzuri pale amini nawaambieni tungekuwa na bonge la rais katika historia.
Moyo wa kikwete na dhamira zake ni kuhakikisha anawafanyia watanzania yale wanayoyatarajia, it tears his heart anapohisi kushindwa, bahati mbaya amezungukwa na watu wanaojua kutumia mapungufu yake.
Kikwete ni kama Messi ndani ya timu ya Taifa ya Argentina au Torres ndani Chelsea, ni bahati mbaya mimi si mmoja wa watu wake wa karibu lakini amini ninachowaambia bado tunamuhitaji kikwete ili kila kitu kiende kwa kiwango tunachotarajia, isipokuwa kinachomshinda ni namna ya kujizungushia watu mahiri na wenye mioyo ya kizalendo ambayo haiingiliki au kuhujumiwa na fortune hunters.......We need him and I respect him believe me.......japo kwa aina ya watu wamzungukao na anavyoshindwa kuwamudu kwakeli sijivunii kuongozwa naye ila sitaacha kumkosoa lakini nikitambua kuwa ndiye rais wangu na wetu sote....

Nikija kwa upande wa Mkapa, hakika ni rais ambaye amefanya maamuzi makubwa, na hakika aliuvaa ujasiri ule ambao kiongozi anapaswa kuuvaa, alitumia kichwa chake na alijiamini. Kuna makosa aliyafanya hilo lipo wazi lakini ukweli utabaki kuwa rais huyu ambaye pia naweza nikam characterize kama a prolific speech writer or journalist alikuwa ni wa aina yake, na yeyot atakyetaka kufanikiwa would rather seek for his advise kwani yupo open minded sana, alisimamia alichoamini, alikuwa ni mtu anayependa changamoto, na alipenda kuzikabili hoja, hakuongoza nchi kwa fununu.
Pamoja na tuhuma za ufusadi zilizokuwepo kipindi kile, lakini alifahamu kuwa na sisi tunahitaji kuishi, akaweza kuzuia mfumuko wa bei, ili na sisi tumudu kuingia masokoni kujipatia mahitaji yetu, alirudisha nidhamu ya uongozi, na mengineyo mengi ambayo wote tunayafahamu hata tukijifanya wabishi tusioukubali ukweli…
Watu wawili hawa hawapiki katika mizani moja, labda ile ya utaifa wao na chama walichomo lakini si utendaji au uweze wa kufikiri na kufanya maamuzi

Wana JF…

Nimebahatika kutembelea kijiji Fulani na kubahatika kupita kijiwe na kusikia mjadala mzito wa kisiasa za hapa nchini.. (take note ni interior hasa!); To sum up – mjadala mzima ulikua centered on the Topic:-

“NI KHERI ARUDI URAIS BENJAMIN MKAPA KULIKO UONGOZI WA JAKAYA KIKWETE”

Hio kauli hapo juu kwa Mtanzania yeyote anesimamia na kufikiria hivo – IMO inasikitisha mno! Kwamba anawaza nini?? au anaichukulia vipi hali na muelekeo mzima wa nchi na hali za wananchi??

MY STAND

Kwa Mtanzania yeyote ambae anaona bora uongozi wa Mkapa kuliko wa Jakaya ni Yule asiyetaka/kubali CHANGE; Na kutaka siku zoote wananchi kuendeshwa kana kwamba ni watoto wadogo wakichukuliwa they can not be independent on their thoughts… For the simple reason… Both Leadership epochs (Mkapa Vs Kikwete) zana cons and pros and the best thing about both epochs is that walau sasa we know what was/is happening under the carpet…. While in conjuction with the worst thing kua ni dhahiri solving them is almost impossible!!!

unamuönea bure baba wa watu, mtu hana makuu anajichekea tu, hayuko siriasi wala hataki kutisha wananchi, kipindi cha njaa huwa anaenda ulaya kutuombea chakula..hataki tufe njaa. KATIBA IBADILISHWE K.IKWETE awe Rahisi wa Maisha(;-))

ʞontɹact Sniper;2382928 said:
Mkapa Vs Kikwete
Unapofanya comparison kati ya tawala/uongozi wa watu wawili wa nyakati tofauti ni lazima pia uchgue maeneo ambayo unataka kuwapimia.
Tatizo ni kuwa walalamikaji wengi wapo too general katika malalamiko yao, kama ukiwauliza wakupe maelezo ya kwanini fulani ni bora utashanga mtua anavyoanza kuingia na kutoka, kiasi cha kujipoteza hata yeye mwenyewe kama utamuuliza alipoanzia ili aweze ku-summarize.
Kwa tabia ya mwanadamu na kimazingira si sahihi mtu kusema hakuna mambo ambayo Kikwete ameyaweza, binaadam yeyote ni progressive, inawezekana tabia yetu ya kutoweza kujituma ikawa ndiyo tatizo au tabia yake ya kuwaamini watu ndiyo inamponza.
Binafsi simuoni Kikwete kuwa na tatizo kwa kiwango na mtazamo waupatao wengine juu yake, kwangu matatizo ya JK ni kuwa si hard wala critical thinker, pia ni mtu na mwepesi kuwaamini watu with his life, bahati mbaya watu anaotokea kuwaamini ni wepesi sana kushawishika, hivyo kumuingia yeye ni rahisi zaidi ukitumia watu anaowaamini, kuliko yeye moja kwa moja.
Tatizo hapa ni layer nayomzunguka rais, kama pangekuwa na layer nzuri pale amini nawaambieni tungekuwa na bonge la rais katika historia.
Moyo wa kikwete na dhamira zake ni kuhakikisha anawafanyia watanzania yale wanayoyatarajia, it tears his heart anapohisi kushindwa, bahati mbaya amezungukwa na watu wanaojua kutumia mapungufu yake.
Kikwete ni kama Messi ndani ya timu ya Taifa ya Argentina au Torres ndani Chelsea, ni bahati mbaya mimi si mmoja wa watu wake wa karibu lakini amini ninachowaambia bado tunamuhitaji kikwete ili kila kitu kiende kwa kiwango tunachotarajia, isipokuwa kinachomshinda ni namna ya kujizungushia watu mahiri na wenye mioyo ya kizalendo ambayo haiingiliki au kuhujumiwa na fortune hunters.......We need him and I respect him believe me.......japo kwa aina ya watu wamzungukao na anavyoshindwa kuwamudu kwakeli sijivunii kuongozwa naye ila sitaacha kumkosoa lakini nikitambua kuwa ndiye rais wangu na wetu sote....

Nikija kwa upande wa Mkapa, hakika ni rais ambaye amefanya maamuzi makubwa, na hakika aliuvaa ujasiri ule ambao kiongozi anapaswa kuuvaa, alitumia kichwa chake na alijiamini. Kuna makosa aliyafanya hilo lipo wazi lakini ukweli utabaki kuwa rais huyu ambaye pia naweza nikam characterize kama a prolific speech writer or journalist alikuwa ni wa aina yake, na yeyot atakyetaka kufanikiwa would rather seek for his advise kwani yupo open minded sana, alisimamia alichoamini, alikuwa ni mtu anayependa changamoto, na alipenda kuzikabili hoja, hakuongoza nchi kwa fununu.
Pamoja na tuhuma za ufusadi zilizokuwepo kipindi kile, lakini alifahamu kuwa na sisi tunahitaji kuishi, akaweza kuzuia mfumuko wa bei, ili na sisi tumudu kuingia masokoni kujipatia mahitaji yetu, alirudisha nidhamu ya uongozi, na mengineyo mengi ambayo wote tunayafahamu hata tukijifanya wabishi tusioukubali ukweli…
Watu wawili hawa hawapiki katika mizani moja, labda ile ya utaifa wao na chama walichomo lakini si utendaji au uweze wa kufikiri na kufanya maamuzi
Mkuu wangu utanisamehe sana ktk hili na wala hutakuwa unamtendea haki Messi kumlinganisha na JK kwa sababu Messi is the best Player duniani wakati JK kiuongoza hajawahi kucheza mahala popote akasifika na ktk hata list ya CCM sidhani kama alitakiwa hata kucheza..

Mimi binafasi yangu mkuu wangu niikuwa na matumaini na JK kupita kipimo, Na kama Mkapa mwaka 1995 nilikuja kujuta kwa sababu sikuwa nikiwajua watu hawa kwa undani na ndilo kosa kubwa la watanzania..Tunachagua wabunge na hata viongozi wa Kitaifa wakati hatuwajui, hatuna record ya ubora wa kazi zao hivyo inapotekea vitu kama hivi tunashtuka kumbe wale wanaowajua hawa watu watakwambia Mkapa hakuna kiongozi mzuri toka zamani - Mlevi na mpenda Vipapi, JK ndio kama hivyo msanii, mhuni kama Mkandara hapa utamweka vipi dhamana mtu kama huyu!..

By the way Messi he is good but not a winner kama Lebron!..Huko South Amerika wanamjulia sana kumkaba nashangaa Europe wanamshindwa akiamua kupasua. Huku South haendi hata hatua mbili nadhani mabeki wao pia wana speed kama yeye..

Sasa hapa mkuu nadhani tunaweza tukawa na suluhisho la pamoja kuhusu hatima ya Tanzania na uongozi wake:
Suluhisho hapa ni watu kama mimi na wewe kuondoa tabia ya kuweka matumaini juu ya wengine, na umefika wakati wa sasa kujiandaa au kuandaa watu wetu, kinyume na hapo tutaishia kulia tu.......Tujiangalie mapungufu yetu, tyafanyie kazi.....tutosheke na mijadala sasa na tushike hatamu, kitendo cha kuwajadili watu fulani kwa matukio yao yasiyo na tija kinadumaza akili zetu na kutuacha tukiwa walalamishi tu....
Tujitafute tujipange na tuanze kazi....

Kuna some characttersitics fulani za mkapa angekuwa nazo JK basi mambo yangekuwa mazuri na kuna some feeatures za JK kama Mkapa ngeuwa naz basi tungekuw tumepiga hatua nyingi zaidi mbele

Kwa nini nasema hivyo?

MKAPA

Mkapa alikuwa na some sort of dictatorship. Yes alitafuta kibwagizo kiuri ch utawala wake UKWELI na UWaZi lakini hakutaka kugusa wala kufutalia kesi za rushwa. Iwe ni Rada, BOT, na nyingine. Alichoamini yeye hauna aliyeweza kumbadilisha. vichache tumeona mazuri yake na vingine vingi bado mpaka leo kuna mswali tele hatujapata majibu. But huu udiketator fulani ndio JK anaukosa.

Nchi yetu sio fully democaratic kama UK, Canada. Tunatakiwa tupate rais fulani mbabe ikiwezekana . Lakini awe ni rais mbabe wa wa kutumia ubabe kwa manufaa ya wananchi sio uabbe wa kuneemesha genge la watu.( System)

KIKWETE

Jkaya Kikwete upande wake anaonekana ana tabia fulani ya usikivu. Kuwa msikivu kwa kupenda au kwa ulazima imebidi aonyeshe japo "sanaa" ya kuridhia "wasanii" wachache wafikikishwe mahakamani. Naamin Hii ni kinyume kabisa na matakwa ya CCM na hata sehemu kubwa ya "system" Tukipata matokeo kesi chache wa watuhumiwa wa mwanzo ndio tutajua jibu juu ya donda ndugu lililopo kwenye system na CCM

Pamoja na usikivu wake. JK ni kama hajui madaraka , nguvu na uwezo wa Rais. mambo yote yanaytokea japo yana baraa zake iwe ni moja kwa moja au kwa kificho hapendi au hatakio kuyasema au kuonekana akiyasema wazi wazi. Na pale anapobanwa kuyasema anachinganya JK haeleweki yuko upande gani. Kama mwenyekiti wa chama JK anaruhusu mramba kugombea majimbo kwa ticket ya CCM huku akijua wana tuhuma na baadae serikali yake inawashatki .... kifupi kwangu JK ni upredictable na haeleweki

Mwisho wa siku kwangu naona Mkapa na jk bado ni watu wanaogop kufanya maamuzi fulani kwa kuhofia labda maisha yao. Sasa kama mpaka kuna kitu rais wa nchi anapata kigugumizi kuifanya japo anajua ni maamuzi sahhii jua kazi tunayo.

Mkapa alifumbia macho Ufisadi, Jk yeye anfanya maigizo na sanaa wa kuwapeleka mahakamani hakuna kitchoendelea. Kwa style ya CCM ili kuanza na scene mpya atakapoishia kitwe ni pabaya sana kwa atayemfuata kama atakuwa ni wa CCM.

kurahishisha kazi sitsahangaa kusikia CCM wanatumia ile style waliotumia kwenye bunge. Zamu wa mwanamke. Hiyo itauwa ni neutralisation tosha ya mapambano ya UFISADI. Otherwise atatakiwa katika kundi la mafisadi ORIGINAL basimoja ndio epewe funguo kugombea urais.

ʞontɹact Sniper;2383083 said:
Sasa hapa mkuu nadhani tunaweza tukawa na suluhisho la pamoja kuhusu hatima ya Tanzania na uongozi wake:
Suluhisho hapa ni watu kama mimi na wewe kuondoa tabia ya kuweka matumaini juu ya wengine, na umefika wakati wa sasa kujiandaa au kuandaa watu wetu, kinyume na hapo tutaishia kulia tu.......Tujiangalie mapungufu yetu, tyafanyie kazi.....tutosheke na mijadala sasa na tushike hatamu, kitendo cha kuwajadili watu fulani kwa matukio yao yasiyo na tija kinadumaza akili zetu na kutuacha tukiwa walalamishi tu....
Tujitafute tujipange na tuanze kazi....
Kwa maelezo haya mkuu wangu nadhani umefunga mjadala!..Shukran na kusema kweli sioni sababu ya kuwazungumzia JK na Mkapa - ILI IWEJE?
Kama kila siku tutafikiria kwanza malengo ya mada au hoja ktk mtazamo wa - ILI IWEJE? maanake hatujifunzi kitu!...nadhani tutakuwa ktk kutafuta solution na sii kuzungumzia mambo in general as if tunatafuta kupata kuvikwa joho la Phd...

Azimio Jipya,
Sidhani Kikwete alikuwa na mpango wa ku expose uozo ulioko ndani ya serikali yake. Nakumbuka ilipoibuka scandal ya EPA Slaa aliitwa kila aina ya majina na makele ya kumpeleka mahakamani. Lakini walikwama. Hili wimbi lililoibuka la kufuchua ufisadi hawakuwa kabisa na mbinu za kulidhibiti. Angekuwa mtu jasiri, angekiri makosa yaliyofanyika na kuchukua hatua za kuwahakikishia Watanzania kwamba hayatatokea tena. Watanzania wangemsamehe. Lakini amekuwa akicheza dana dana tu na Watanzania huku akiwa hana jinsi ya kudhibiti uchafu unaozidi kufichuka kila kukicha ndani ya serikali na chama chake. Ni kama mtu aliyepigwa na wimbi ambalo hajui limetoka wapi.

Jasusi;

Anyway, Kulingana na hoja inayoendelea hapa ... inaniwia vigumu sana ... kulielewa somo la Siasa au Political Economy ... am not that good on this area.. HUWA NAJIULIZA ... Inakuwaje basi Historia au Political Forces etc ... zimfanye mtu kama JK awepo kwenye nafasi aliyopo hadi sasa ... Ni nini kina- Determine kupata kiongozi wa kisiasa kwenye jamii husika kwa kipindi husika? Ni bahati nasibu? Is it total chance or random? ...!!

Naweza kuruhusiwa kusema kuwa Mkapa na Kikwete walikuwa viongozi wazuri lakini Watanzania ndio wenye madhaifu ya kutosha kuwakubali!!?

angalau Kikwete alichomzidi Mkapa ni kupunguza majambazi ndani ya jeshi la polisi

Napepesa sidhani kama nitaona jingine

Jasusi;

Anyway, Kulingana na hoja inayoendelea hapa ... inaniwia vigumu sana ... kulielewa somo la Siasa au Political Economy ... am not that good on this area.. HUWA NAJIULIZA ... Inakuwaje basi Historia au Political Forces etc ... zimfanye mtu kama JK awepo kwenye nafasi aliyopo hadi sasa ... Ni nini kina- Determine kupata kiongozi wa kisiasa kwenye jamii husika kwa kipindi husika? Ni bahati nasibu? Is it total chance or random? ...!!

Naweza kuruhusiwa kusema kuwa Mkapa na Kikwete walikuwa viongozi wazuri lakini Watanzania ndio wenye madhaifu ya kutosha kuwakubali!!?
Kuna makala moja aliwahi kuandika marehemu Rugatiri Mekacha baada ya rais Mwinyi kuingia mamlakani na utendaji wake kwamba watu wengi walijiona kuwa "kumbe na sisi tunaweza." Katika hili kundi alikuwemo Kikwete. Mwinyi kumlinganisha Nyerere na mlima Kilimanjaro na yeye kichuguu haikuwa metaphor ya bahati mbaya. Sasa kama kichuguu kinaweza kushika nafasi ya Kilimanjaro si hata miinuko tu na vilima vidogo vidogo navyo vitajiona kuwa vinaweza? Nyerere aliweka high standard ya uongozi. Mwinyi akaishusha. Ndipo yakatokea ma akina Tom, Dick and Harry nayo yakajiona kuwa yanaweza kuwa rais wa Tanzania.

ʞontɹact Sniper;2383083 said:
Sasa hapa mkuu nadhani tunaweza tukawa na suluhisho la pamoja kuhusu hatima ya Tanzania na uongozi wake:
Suluhisho hapa ni watu kama mimi na wewe kuondoa tabia ya kuweka matumaini juu ya wengine, na umefika wakati wa sasa kujiandaa au kuandaa watu wetu, kinyume na hapo tutaishia kulia tu.......Tujiangalie mapungufu yetu, tyafanyie kazi.....tutosheke na mijadala sasa na tushike hatamu, kitendo cha kuwajadili watu fulani kwa matukio yao yasiyo na tija kinadumaza akili zetu na kutuacha tukiwa walalamishi tu....
Tujitafute tujipange na tuanze kazi....

Sniper;

Huo ni mtizamo muhimu... Nimekuwa nafikiri wakati mwingi kuwa ... kwa namna fulani jambo la msingi sio Viongozi wetu ... Ila ni sisi wanachi tunaowaweka kwenye nyadhifa walizo nazo. Kwani kwa kweli Sidhani kuwa kuna nguvu nyingine ya kisiasa ziadi ya Wanachi inayowawezesha wao kuwa hapo walipo. Na ninafikiri ni kweli labada tumepoteza mwelekeo kabisa katika mapambano haya... Tunge jitahidi kupata namana ya kuwajenga wapiga kura. Lakini Sniper nafikiri ni vema kuwajdili viogozi wetu kwa kina kwani kwa mijadala hiyo tunafikia kugundua kuwa sasa tuwaache na tujijadili sisi wapiga kura!

Kuna makala moja aliwahi kuandika marehemu Rugatiri Mekacha baada ya rais Mwinyi kuingia mamlakani na utendaji wake kwamba watu wengi walijiona kuwa "kumbe na sisi tunaweza." Katika hili kundi alikuwemo Kikwete. Mwinyi kumlinganisha Nyerere na mlima Kilimanjaro na yeye kichuguu haikuwa metaphor ya bahati mbaya. Sasa kama kichuguu kinaweza kushika nafasi ya Kilimanjaro si hata miinuko tu na vilima vidogo vidogo navyo vitajiona kuwa vinaweza? Nyerere aliweka high standard ya uongozi. Mwinyi akaishusha. Ndipo yakatokea ma akina Tom, Dick and Harry nayo yakajiona kuwa yanaweza kuwa rais wa Tanzania.

Jasusi;

@ Blue ... Najaribu kukupata ..lakini zidhani ... Im geting you cleraly..!

Mwinyi asingejilinganisha ..?

Au Tulianza kufanya KOSA la kuwapata viongozi kuanzia Mwinyi walipoingia Madarakani. Nikiamaanisha kuwa baada ya kosa hilo ... Kila mmoja akajiona ni bora...?

Jasusi;

Anyway, Kulingana na hoja inayoendelea hapa ... inaniwia vigumu sana ... kulielewa somo la Siasa au Political Economy ... am not that good on this area.. HUWA NAJIULIZA ... Inakuwaje basi Historia au Political Forces etc ... zimfanye mtu kama JK awepo kwenye nafasi aliyopo hadi sasa ... Ni nini kina- Determine kupata kiongozi wa kisiasa kwenye jamii husika kwa kipindi husika? Ni bahati nasibu? Is it total chance or random? ...!!

Naweza kuruhusiwa kusema kuwa Mkapa na Kikwete walikuwa viongozi wazuri lakini Watanzania ndio wenye madhaifu ya kutosha kuwakubali!!?
Hapana mkuu wangu Mkapa na JK wote ni viongozi wabovu, wadhaifu na wenye mapungufu kama tulivyo Watanzania wengi - Hawa ni reflection yetu..
Sasa asilimia 20 au 35 ambao hawakuwachagua viongozi hawa ktk chaguzi zilizopita, ni chini ya asilimia 1 tu ya Population ya nchi nzima.. Hivyo makosa yapo kwetu sisi wenyewe kuwachagua viongozi wabovu na sababu hatujawahi kuona kiongozi mzuri anatakiwa kuwa vipi..
Pili, vijana na wazee watu wengi hawapigi kura kutokana na sababu zisizojulikana.
Na mwisho ile asilimia 80 au 65 waloshinda JK na Mkapa inatokana na Ushabiki wa kimpira zaidi ya kuelewa wanapoteza kitu gani...

Hili la eti JK kaachia mambo yawe hadharani bado linanitatiza bado siamini kwamba ni mkakati alioupanga kwa makini manake kama ni hivyo hao mainjinia wa huo mkakati wana ulakini chukulia mfano suala la IPTL,baadhi ya mikataba tata ya madini au tuhuma zinazomkabili Porf.Mahalu hizi zinamgusa kwa namna moja au nyingine JK kwani zilitokea kipindi yeye akiwa ndo kiranja kwenye hizo wizara, ndo maana bado naamini yote yametokea bila ya wao kutegemea na bila ya kujua jinsi ya kujilinda, na hii ikichangawia zaidi na staili ya JK ya 'divide and rule' kwa kukumbatia zaidi watendaji waliomsapoti wakati wa uchaguzi wa ndani ya CCM 2005 kwahiyo wale waliosapoti wagombea wengine waliwekwa kando 'labda wakaamua' liwalo na liwe.
Lazima tukubali zama zinabadilika inawezekana enzi za Mkapa watu walikuwa na cha kupoteza hivyo wakaamua kukaa kimya na/au kuugulia kimyakimya tofauti na sasa ambapo tunakaribia kufika point of no return na wananchi hawana chachote cha kuhofia.,Kama alivyosema Jasusi Mkapa atalaumiwa daima kwa kukubali kuachia nchi kwa Mtandao wa visa na kujilimbikizia mali wakati anageweza kutoa chaguo sahihi zaidi..

Mkuu Iza… hilo ndo linanipa wasi wasi…. However ninaposema kua JK kayaachia nje (basing on assumption pekee) maana yake ni kua kalegeza kamba.. Katika milolongo na milipuko ya mambo; in most cases JK alikua in silent mode na no immediate reactions were taken… Na ndo maana nimegusia hapo nyuma kua only time will tell as it has done Kwa Mkapa. Imagine hili tendo la kuweza dhubutu fikiria kua kheri Mkapa – jamani yaani ina maana haijapita hata ten years na tushasahau what the guy has done??… kashfa zake zoote?? Na ufisadi dhahiri wa wazi… Uloongea ina ukweli ndani yake, but hata hivo JK hakuyavalia njuga kama vile the way Mkapa angevalia kama ingetokea wakati wake….

Wakuu nadhani tumeanza kusahau kidogo, mwishoni mwa enzi za Mwinyi Tanzania ilikuwa inaelekea kuwa a failed state (yes I mean it) failed state si lazima uwepo wa vita. Nchi somehow ilikuwa haitawaliki, kila mtu uliweza kufanya upendavyo ili mradi una hela tu, you could steal,maim, even kill tena hadharani!!!!, Government was broke, discredited and confused. Ndiyo haswaa mwanzo wa ngonjera ya ukosefu wa madawati, walimu kukosa mishahara, ukosefu wa uwajibikaji, misheni town etc. Migomo ya wafanyakazi, wanafunzi..

Hii paragraph i completely agree with you... Mwinyi hakua raisi, ila tu alikua

anadimbadimba uraisi... angeongeza tu five more years... ingekua mo' disaster!!!

The main thing ambayo Mkapa atakumbukwa Daima ni kurudisha credibility ya serikali, if you don't know what this is, just look at Somalia, Congo na hata Pakistan (Tofauti kuu ambayo tungekuwa nayo na hao labda ni ukosefu wa vita). Ni wakati huu wa Mkapa serikali ilipoonekana kumbe ikiamua inaweza, makusanyo ya kodi yaliongezeka kwa asilimia karibu elfu moja (1000%) kutoka Bilioni 25 kwa mwezi mpaka bilioni 200 - 250. This is the time ada ya shule ya msingi ikafutwa, migomo vyuoni ikapungua sana , Ajira ya serikali ikarudishwa heshima, inflation ikawa truly contained na si hii ya sasa ya data za kupika. (Kwa mwananchi wa kawaida this is the centre of all the troubles) For the first time miradi mikubwa kama ya barabara ikaanza kufanyika kwa hela zetu wenyewe. It is in Mkapa's term Tanzania ikaondoka kwenye the best 5 if not 2 poorest countries in the world. Tukaona madirisha na milango hadi ceiling boards zikirudi shule za msingi mambo yaliyoanza kuwa historia. (Kwa faida ya wengine shule nyingi tu enzi za Nyerere zilikuwa mpaka na vyoo vya "kuflash"). Kifupi serikali ikawa na hela na ndiyo sasa gateway ya ufisadi mkubwa mkubwa ikajitokeza. Who would steal the monies we didn't have in Mwinyi and Nyerere's era??????? Another big plus ya wakati wa Mkapa ni uongozi, serikali ilieleweka inasimamia nini na what was the vision. The big issue with Mkapa though na hayo aliyoyafanya ni "at what price??"

Nakubaliana nawe kua the guy deserves some credibility... but kuitoa Tanzania as an analogy with the likes of countries such as Sudan and Somalia.... Unazungumzia suala la kodi - nakubali kua Mkapa alileta the most organises system than before hadi kuanza lipia mapato katika banks; but kumbuka kua ni wakati huo huo ambao mapata yamekua yakilenga manufaa ya serkali kkuliko mwananchi... natolea mfano mdogo wa usafiri wa magari kwa wale wano miliki... kuna mambo kibao ya kulipia... acha bara bara, mapato, stickers na maswala kibao ambayo mengi hayana msingi na unashindwa elewa - Mtu analazimishwa kununua fire extinguisher kuweka kwenye gari.... haya umenunua, but bado inatakiwa uilipia kila mwaka... kama sio wizi ni nini?? hapa mapato yanakosa kupatikana?? Mwananchi anafungua kiduka chake anaambiwa lipa mapato kwanza.... jamani hayo mapato duka ndio linafunguliwa ndo yepi?? Lakini sababu mwananchi hana jinsi inambidi alipie....

Tatizo naloliona kwa JK ni kama vile amepewa uraisi kwa kushtukizwa whilst he's on record kujiandaa for more than 10 yrs. Suala la mambo kuwa exposed au the so called uhuru wa vyombo vya habari ni debatable! ni sawa na kusema Obama ana-interact sana na wananchi kwa njia za kisasa kama twiter, emails etc. wakati Clinton alituma email moja tu in the white house. in 8 years. JK kwanza amemaliza hela zote alizoacha Mkapa, kwa mara ya kwanza tunashuhudia serikali ikikopa toka benki za biashara, Ask any govt employee (wale wa kawaida) entitlements zao ndiyo kama zimeyoyoma hivyo. Ametuletea shule za kata, barabara haziishi, Giza, ufisadi ndiyo haswaa umepamba moto, Uongozi sifuri, ule ujanja ujanja wa enzi za mwinyi ulioanza kuondoka umerudi kwa kasi ya ajabu na maradufu. Nepotism at it's best, ofcourse huwezi kukwepa hili maadili yakikosekana na jamii ikiwa corrupt.

Kwa maoni yangu there's pieces of Mkapa's work unaweza kuziweka kwenye uongozi wa JK na mambo yakaenda kiasi flanni lakini I doubt if there is any piece of JK (The good side) unayoweza kwenda kuichanganyisha na utawala wa Mkapa to get the country going.

Hitimisho langu though hao wote Mkapa na JK wameacha makovu (JK anaendelea) yatakayochukua miaka mingi sana kuwa properly healed.

Im my opinion.... JK alivo sasa ndio JK original and what ever he is doing and his reactions.... that is the way he is... Hata angeongeza miaka kumi ndo agombee, ingekua kazi bure.. Hana nature ya Leadership... he is not strong enough nor does he have the guts....

Back
Top Bottom