Ni kheri arudi urais Benjamin Mkapa kuliko uongozi wa Jakaya Kikwete: What does that tell us? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kheri arudi urais Benjamin Mkapa kuliko uongozi wa Jakaya Kikwete: What does that tell us?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AshaDii, Aug 18, 2011.

 1. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Wana JF…

  Nimebahatika kutembelea kijiji Fulani na kubahatika kupita kijiwe na kusikia mjadala mzito wa kisiasa za hapa nchini.. (take note ni interior hasa!); To sum up – mjadala mzima ulikua centered on the Topic:-


  “NI KHERI ARUDI URAIS BENJAMIN MKAPA KULIKO UONGOZI WA JAKAYA KIKWETE”

  Hio kauli hapo juu kwa Mtanzania yeyote anesimamia na kufikiria hivo – IMO inasikitisha mno! Kwamba anawaza nini?? au anaichukulia vipi hali na muelekeo mzima wa nchi na hali za wananchi??

  MY STAND

  Kwa Mtanzania yeyote ambae anaona bora uongozi wa Mkapa kuliko wa Jakaya ni Yule asiyetaka/kubali CHANGE; Na kutaka siku zoote wananchi kuendeshwa kana kwamba ni watoto wadogo wakichukuliwa they can not be independent on their thoughts… For the simple reason… Both Leadership epochs (Mkapa Vs Kikwete) zana cons and pros and the best thing about both epochs is that walau sasa we know what was/is happening under the carpet…. While in conjuction with the worst thing kua ni dhahiri solving them is almost impossible!!!
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkapa ndiye aliyetupachikia Kikwete. Alikuwa na nafasi ya kutupatia kiongozi mwenye ruuya lakini baada ya kutumbukia kwenye limbwi la ufisadi akawa compromised na Rostum na matokeo yake ndiyo haya tunayojutia hivi leo. He really let the country down.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Watch my word here....

  Tutakapopata rais mwingine wa ccm.....

  Itakuwa .....bora kikwete kwa kweli.......
   
 4. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Uongozi wa awamu ya nne umeandika historia ya aina yake kwa kuwa ndio uongozi ulioongoza kwa kufanya na kuendesha mambo yake kutegemea nini kimeandikwa kwenye magazeti. kwangu mimi uongozi huu umekosa maono na unaendeshwa kwa ujanja ujanja tu ili siku ziende. kitu uongozi huu unachojisahau ni kuwa times change....and would never be the same again! historia itatuhukumu vema kama haya tunayoyaona tumekosea....
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yaani una maana kwamba Tanzania tutapata rais worse than Kikwete? God forbid!
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Jasusi you genuinely believe angekua kiongozi mwingine hata kama ni CCM humo

  humo ndani hali ingekua tofauti?? Na in other words huu ufisadi umeanza miaka hii mitano ya karibuni??
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  wewe umesahau nyerere alisema tusije kumpata rais atakae tufanya tuseme mwinyi ni bora zaidi???????

  Well, tumeshapata wawili so far....
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Boss,
  I would like to say yes. Salim asingekuwa mpuuzi kama alivyo Kikwete. Salim angefanya makosa mengine lakini angejitahidi sana kutoa
  credible leadership to the country. Hatumhukumu Kikwete kwa ufisadi peke yake. Tunamhukumu Kikwete for his inaction hata pale inapoonekana kuwa hatua za mara moja zilistahili kuchukuliwa, yeye anakaa kimya. Mfano ni suala la Jairo. Huyu jamaa hakutakiwa kuwa kwenye likizo ya malipo.
  Unamstaafisha kwa manufaa ya umma na kazi kwisha, lakini nasikia alimgombeza Pinda kwa kusema hadharani kwamba ungekuwa uamuzi wake Pinda Jairo angeachishwa kazi. Kikwete was angry!
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  One thing i am sure is that historia huko mbele iko siku itampongeza JK..

  Pamoja na kwamba hana Leadership qualities...

  Uongozi wa awamu ya nne ni uongozi ambao umefanya mambo mengi amabayo ni manufaa kwa mwananchi as much as unamkandamiza kila aspect ya maisha... Nafikiri hii awamu ndo ilitakiwa iwe kauli mbiu ya uwazi na ukweli for sasa everything swept under the carpet iko nje... Nakubaliana na blue thou for naamini kabisa hata Jakaya anataka siku ziishe haraka aachie ngazi kuliko hata walo against nae... for he knows too kua kashindwa...
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Well, you just answered your question. Kikwete is worse than Mwinyi, and he is worse than Mkapa. Yaani mizani inazidi kwenda chini badala ya kupanda juu. Sasa hatutaki rais atakayekuwa worse than Kikwete. I believe Tanzania deserves better.
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Jasusi ... unazungumzia la Jairo hili la juzi... angalia ungozi mzima wa JK... mangapi yamekua exposed?? matatizo mangapi saizi yamekua as a result of that exposure?? Na umejiuliza hayo yoote yalokua exposed ni since when yalianza na mizizi yake iko tangled vipi?? JK yupo kwenye politics like forever - swali napenda nijue ni kwamba alijua yoote hayo, alifanya hivo kwa malengo gani kama hawezi ya solve??
   
 12. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Asha;

  @ Blue, Nakubaliana na ukweli kuwa chini ya uongozi wa Rais Jk ..imetokea fursa... iliyowezesha mapungufu na madhaifu makubwa ya muda mrefu ndani ya serekali na Chama kujulikana hadharani... Hilo haliwezi kupingwa. Ningependa Mimi, kudadisi kuwa mafanikio hayo ya kui xpose ccm na serekali was it delibarate move kama mkakati aliojenga Rais JK? au was it just out of coincidence!! Maana kama Rais Jk ..alikaa akaiwazia nchi jinsi gani aisaidie halafu akafanya aliyofanya huo ni ushujaa na make him very strong as a Leader ..but kama ilitokea tu, bila msukumo toka akilini na moyoni kwake kama hata kama imeleta matunda mazuri ...I will always say .. Doing the right thing for a wrong reasons/motive ... !!
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  ...
  Naamini kuwa tukichukulia Taifa kama kiumbe kinachozaliwa na kinachokuwa na kupitia mabadiliko mbalimbali, sina shaka historia itamkunbuka JK kwa udhaifu au kwa ushujaa ... ALIFANIKIWA Kufanya ukweli mkubwa kuwa hadharani... hii ni bora kuliko kama ungefichika huku wananchi wakiendela kufikiri wana serekali na chama imara chenye uwezo wa kupamabana na ufisadi kwa mfano! ...lakini kwa kuwa sasa all is out there exposed ... Taifa linajua fika udhaifu uliopo na hatua za kuuushughulika sasa zichukuliwe ...!

  ... Ni naamini kwenye historia and it cant be changed ... yaani Rais Kikwete historia haiwezi tena kumbadilisha kuwa hakuwa Raisi wa Tz na aliyeiwezesha Tz kujigundua kuwa Baaadooo sana Kimaendelao ... Naamini kuwa hakufanya hivyo kwa sababu he is that good! NDIO MAANA ANAWISH MUDA UNGEKWENDA HARA AKAJIONDOKEA.. Lakini in either way and since history cant be changed ...GENERALY SPEAKING ... kwa udhaifu wake atakuwa amechangia jambo kubwa la kutuamsha kuwa UONGOZI wa nchi na UFISADI si mambo ya kufanyia mzaha ...na kwa kweli hili liwe ni fundisho kwa uongozi wa vizazi vijavyo!
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Azimio Jipya,
  Sidhani Kikwete alikuwa na mpango wa ku expose uozo ulioko ndani ya serikali yake. Nakumbuka ilipoibuka scandal ya EPA Slaa aliitwa kila aina ya majina na makele ya kumpeleka mahakamani. Lakini walikwama. Hili wimbi lililoibuka la kufuchua ufisadi hawakuwa kabisa na mbinu za kulidhibiti. Angekuwa mtu jasiri, angekiri makosa yaliyofanyika na kuchukua hatua za kuwahakikishia Watanzania kwamba hayatatokea tena. Watanzania wangemsamehe. Lakini amekuwa akicheza dana dana tu na Watanzania huku akiwa hana jinsi ya kudhibiti uchafu unaozidi kufichuka kila kukicha ndani ya serikali na chama chake. Ni kama mtu aliyepigwa na wimbi ambalo hajui limetoka wapi.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  AshaDii,
  Nadhani hoja nzima ilikuwa fikra za watu wanaosema ni kheri ya Mkapa angerudi kuliko uongozi wa JK kuwa msingi wa hoja yako kuwashangaa watu hawa lakini sikutegemea kwamba hata wewe unaona bora ya JK ktk kipimo cha viongozi wawili wabovu. Binafsi siku zote humpima kiongozi sio kwa jambo moja na wala simpimi kiongozi kwa kufanikisha sheria zisiyokuja Uchumi wa nchi kwani hakuna sifa kama hiyo ktk uongozi bora kama huboreshi maisha ya wananchi..

  Niliwahi kusema kwa wanaomsifia Mkapa kwamba aliweza piga hatua tatu mbele muhimu za ufanisi ktk uchumi wa Tanzania lakini akatudisha nyuma hatua saba hivyo kwa ujumla wake Mkapa aliturudisha nyuma hatua nne sawa na JK ambaye aliukuta uchumi upo hatua nne nyuma katurudisha hatua nyingine mbili zaidi na kufika hatua sita nyuma. hatua mbili nyuma hazina unafuu wowote kwa sababu gari lililokwama huwezi jaribu kuliendesha ktk tope bila kutafuta mbinu za kulikwamua kwanza.

  Kwa nini wananchi wanasikia uchungu zaidi leo wakati wa JK kuliko wakati wa Mkapa au Miwnyi?..ni kwa sababu tulikuwa ktk kuporomoka tayari (hatua nne nyuma) hivyo ongezeko lolote la kuporomoka chini linakuwa na machungu zaidi kuliko tungekuwa ktk hali nzuri ya kiuchumi na tukashuka kama nchi za Ulaya leo hii.

  Sasa sababu hasa ya wananchi kushindwa kufikia maamuzi mazuri na ya busara ktk mapendekezo kama haya ni kwa sababu hatujawahi kuona maendeleo ya kiuchumi zaidi ya miaka ya mwanzo ya Nyerere between 1972 na 1978 kabla ya vita ya Uganda ambapo GDP yetu ilikuwa ikipanda kwa zaidi ya asilimia 6 na hadi 10 kwa mara ya kwanza ktk historia ya nchi yetu. Lakini kwa bahati mbaya ni ktk miaka ya 80's ndio watu wengi tunayo kumbukumbu yake kwa sababu tulishuka hadi kuanza kula mtaji na kifo cha Ujamaa ndio kilitumaliza kabisa.

  Ni vigumu sana kumpata mtu leo hii anayekumbuka Tanzania ya mwalimu Nyerere ambayo ilikuwa nchi ya pili duniani kwa kuproduce Chai, halafu ukitazama pamba, kahawa, korosho na katani tukiwa ktk best 10 bila kusahau Zanzibar ikiongoza duniani kwa kuzalisha Karafuu na spices nyinginezo. Leo hii ni historia ktk vitabu, hatupo hata katika picha ya wazalishaji pamoja na kuwa tumeingia ktk Ubepari - Pamoja na kwamba Ardhi bado tunayo na nguvukazi imeongezeka maradufu.. hatuna cha kujivuania zaidi ya kuhesabu madeni na mchango wa misaada ktk GDP yetu wakati hakuna mfumo bora wa kutoza na ukusanyaji kodi..

  Bado mahotel yanabadilishana mikono kwa majina kila baada ya miaka mitano na Jk hawezi kuwalazimisha wenye Hotels wasiuze kwa sababu hiyo ni biashara ya mtu sio ya serikali. Biashara ikishuka hakuna sheria ya kumfunga mtu kulazimishwa abakie na biashara isiyolipa, ingawa tunajua wanatengeza faida kubwa. Hayo Madini, Wanyama pori, Viwanda na uwekezaji woote ulotanguliwa na mikataba/ubinafsishaji wa Mwinyi na Mkapa ulikuwa Mbaya sana kiasi kwamba JK hawezi kurekebisha kitu unless yeye mwenyewe achukue maamuzi magumu..Nakumbuka Jk alisema mashirika ya madini yataanza kulipa ushuru wa mapato mwaka 2010 lakini ktk bajeti sikusikia hilo likizungumziwa na limeongeza pato la taifa kwa kiasi gani..

  Ni yapi hayo maamuzi magumu.. nadhani hapa ndipo napoweza kumpongeza Lowassa kwa kauli yake ingawa sina hakika kama alikuwa na maana sawa na yangu. Maamuzi magumu ni kuvunja mikataba yote mibovu, mikataba iisiyokuwa na faida kwa nchi yetu zaidi ya kuuza utu wetu kwa fedha. Kuchukua maamuzi kama ya rais Chavez wa Venezuela kwa sababu mikataba yote iliyotanguliwa na Mwinyi au Mkapa imeifunga serikali ktk gereza, hali ambayo sii rahisi kujikwamua na labda niseme kwamba serikali imekamatwa pabaya kama shirika la Tanesco ktk sekta zote za Uzalishaji...Ubinafsishaji umekuwa Ukoloni mamboleo tunalipa madeni yasiyokwisha, kuwadhalilisha wananchi zaidi badala ya kuwajenga.

  Na maadam JK ameshindwa kusimama imara na kusoma alama za nyakati na kuchukua maamuzi magumu kama Lowassa alivyofanya na Citywater matokeo yake ndio maana JK anaonekana kiongozi dhaifu na asiyeweza kuongoza kutokana na urithi alochukua na kuapa kuboresha maisha ya wananchi...Kifupi JK kashindwa kuongoza, GDP inayoongezeka kwa mauzo ya mashirika ya nje hali mfuko wa Taifa haifaidiki na rasilimali/ maliasili zilizopo ni sawa na kujaribu kujaza maji ndoo iliyotoboka..Haisaidii kitu kupanda kwa GDP ikiwa hakuna kitu kinaongezeka ktk mfuko wa Taifa kulingana na mahitaji na kupanda kwa maisha..
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Asante Azimio... Hapa ulichofanya ni kuelezea kwa kirefu kile ambacho ni mawazo/utambuzi na analysis yangu... Putting Politics na ushabiki pembeni, you have to give it to Jakaya kuwezesha kwa kiasi kikubwa kuweka mambo wazi - thou ni a weak leader...

  Believe me you.... jamaa (JK) ana attitude inayo boa kwetu wananchi.. ule mtindo wake wakuchukulia mambo ka vile it is ok, na kana kwamba yataisha kesho hali things are getting worse!! Jasusi sijui lakini.... but from my observation and IMO naamini kabisa most ya vitu vilivyokua reavealed ni tokana na yeye mwenyewe kulegeza kamba na kuachia kwamba yawafikie wananchi (i think aliamini kua maybe atasifika kwa hili)... Jiulize saana, this can not be a coincidence kua huu uozo woote utoke at the same time - thou woote unahusishwa na uongozi wake, ambao ni dhahiri kua ni failure... in most cases ni issues ambazo zipo for more than 20 and more years ago.... Hizo issues, ni zile ambazo kila Mtanzania Mzalendo mwenye utambuzi atagundua kua Leadership ya CCM is not only about Presidency but who is involved behind the seat... Na kwamba leadership yao yooote ni mbovu, na before waliiisuka in a way kua mwananchi wa kawaida asijue what is/not happenning...
   
 17. j

  jobswygant01 Member

  #17
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutakapopata rais mwingine wa ccm.....


  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
   
 18. Terrire

  Terrire Member

  #18
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini hawezi tokea kiongozi wa ajabu kama JK, bora muda wake uishe coz hatuoni msaada wake kwa wa TZ
   
 19. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Bado mnamawazo ya kurudisha ccm kwani?damn ccms
   
 20. T

  Tata JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Tatizo la nchi hii siyo kiongozi mmoja mmoja kama watu wanavyotaka kutuaminisha. Tatizo ni mfumo wa kikatiba na kisheria unaotoa mwanya wa viongozi wabovu kuzalishwa, kulelewa na hadi kushika nafasi za juu za uongozi. Kwa taarifa yako tatizo la uongozzi nchi hii limeshuka toka kwa raisi mpaka kwenye ngazi za juu na za kati za uongozi wa serikali na kwa bahati mbaya hapo ndipo maamuzi makubwa ya matumizi ya pesa za walipa kodi yanapoanzia. Hata utamaduni wa utendaji kazi wa serikali hautuwezeshi kwenda mbele kwani umesababisha wataalamu kuwa mabingwa wa kusoma matakwa ya wanasiasa na kutoa ushauri unaoendana na mambo ambayo wanasiasa wanapenda kuyasikia. Kwa ufupi tupo kwenye tope zito "quagmire"na tunaendelea kuzama.
   
Loading...