Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Akiwa kwenye mahojiano na kipindi maalum cha Clouds leo aliyekuwa Rais wa awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema kuwa mchakato uliokuwa mgumu zaidi kwake ni kuzuia uhuni wa kubadili muhula wa uongozi ndani ya CCM kutoka miaka mitano kuwa saba.

Jakaya anasema mjadala ulipoletwa ulikuwa ni moto ila tayarI CCM kulikuwa na utaratibu wa miaka mitano na uamuzi huo uheshimiwe.

======

KUONGEZA MIAKA YA URAIS
Kikwete:
Kuna kipindi walianza sana mjadala wa kubadili katiba sijui iwe miaka 7, pale wazee tulishauriana tukasema hapana, huku wanapotaka kutupeleka hawa sipo.

Nchi yetu ina viwango, hapa ilipofikia heshma yake kubwa ni kuheshimu vipindi viwili vya miaka mitano, wakianza hawa na miaka 7 huko tunakokwenda siko.

Nakumbuka tulikutana wazee na siku hizi hamna haja kukutana hata kwa simu mnaunganisha, tukakubaliana hawa lazima tuwaambie vijana hawa.

Akiwa kwenye mahojiano na kipindi maalum cha Clouds leo aliyekuwa Rais wa awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema kuwa mchakato uliokuwa mgumu zaidi kwake ni kuzuia uhuni wa kubadili muhula wa uongozi ndani ya CCM kutoka miaka mitano kuwa saba.

Jakaya anasema mjadala ulipoletwa ulikuwa ni moto ila tayarI CCM kulikuwa na utaratibu wa miaka mitano na uamuzi huo uheshimiwe.
Heee! Ya kweli haya?
 
Back
Top Bottom