Ni katika hali gani Askari anaruhusiwa kutumia bunduki?

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
349
464
Sijawai kuwa Askari ila naona kuna matumizi yasiyo sahihi ya nguvu na risasi kwa wahalifu au watuhumiwa.

Kwa kisa hiki kilichomsababishia majeraha makubwa binti wa miaka 16 kwa kupigwa risasi na askari utaona kabisa hapa kuna kitu hakijakaa sawa.

Risasi zinazopigwa hovyo hovyo zimegharimu maisha ya watu wasio na hatia.

Tuendelee kuelimishana na kuwajibishana ipasavyo ili makosa kama haya yasijirudie.

IMG_4832.png
 
Muda wowote askari akiona kuna mtu analeta mazingu ambayo yanahatarisha maisha yake (askari) risasi inafyatuliwa.

Kipimo cha "kuhatarisha maisha" ni moyo, dhamira na utashi wa askari mwenyewe.

Yaani hata ukijitia ujuaji ukamuangalia askari kwa kijicho cha pembeni halafu yeye akahisi maisha yake yako hatarini anakubutua na risasi. Potelea pwete!
 
Ukute mjeruhiwa ni mmoja wa waliokua wanang'ang'ania kuokota mawe licha ya kuwepo katazo na onyo kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,kama polisi hivyo askari wakaona wawafyatulie risasi.
 
Maisha ya kuokota mawe mgodini huko Nyamongo sishangai huyo kupigwa risasi ile mbilinge huwa ni kufa kupona hata gari za hao maaskari ikitokea ikaja Dar wakazi wa Dar watashtuka hii imetoka vitani au Tanzania hii hii ya amani na utulivu?

Maisha ya askari alieko mgodini nyamongo si lelemama ni kazi kweli hata yeye lo lote laweza kumpata kama sio kifo basi hata ulemavu utampata.

Ile bunduki inatakiwa imlinde kwanza yeye na yeye ailinde hiyo silaha ndipo iwalinde na wengine!
 
atatumia muda wowote akiona silaha yake ipo hatari pamoja na yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom