Ni kama Dr. Magufuli anatengeneza vita

Ni kama Dr. Magufuli anatengeneza vita

Hao ni zao la kushindwa kwa awamu hii kuhusu sera ya ajira.Hao wote ilitakiwa wawe kwenye uzalishaji Ili kukuza export tupate pesa nyingi za kigeni tuweze fanya miradi kwa pesa zetu na sio kutegemea mikopo.Bodaboda na machinga hawa ni madalali wa kuuza vitu vilivyozalishwa china wanasaidia kuukuza uchumi wa China.Ilitakiwa wote waingizwe kwenye uzalishaji mashambani, viwandani, kwenye uvuvi,kilimo na sio kuzagaa mijini kama daraja la wanasiasa uchwara wasiotazama future ya taifa kwa kutengeneza bomu la kesho wakijua kesho awapo.
Uko safi lakini? BIG UP! Tanzania inawahitaji watu kama nyie mnao waza beyond the Horizon
 
Hao ni zao la kushindwa kwa awamu hii kuhusu sera ya ajira.Hao wote ilitakiwa wawe kwenye uzalishaji Ili kukuza export tupate pesa nyingi za kigeni tuweze fanya miradi kwa pesa zetu na sio kutegemea mikopo.Bodaboda na machinga hawa ni madalali wa kuuza vitu vilivyozalishwa china wanasaidia kuukuza uchumi wa China.Ilitakiwa wote waingizwe kwenye uzalishaji mashambani, viwandani, kwenye uvuvi,kilimo na sio kuzagaa mijini kama daraja la wanasiasa uchwara wasiotazama future ya taifa kwa kutengeneza bomu la kesho wakijua kesho awapo.

..sina uhakika kama Magufuli atashughulikia tatizo hili wakati anawaza kununua midege mingi zaidi toka kwa mabeberu, na wizara za kilimo na viwanda anazitengea 6% ya bajeti waliyoomba.
 
Hao ni zao la kushindwa kwa awamu hii kuhusu sera ya ajira.Hao wote ilitakiwa wawe kwenye uzalishaji Ili kukuza export tupate pesa nyingi za kigeni tuweze fanya miradi kwa pesa zetu na sio kutegemea mikopo.Bodaboda na machinga hawa ni madalali wa kuuza vitu vilivyozalishwa china wanasaidia kuukuza uchumi wa China.Ilitakiwa wote waingizwe kwenye uzalishaji mashambani, viwandani, kwenye uvuvi,kilimo na sio kuzagaa mijini kama daraja la wanasiasa uchwara wasiotazama future ya taifa kwa kutengeneza bomu la kesho wakijua kesho awapo.
Correct by 100%
 
Tumeingia uchumi wa kati huku tunajivunia kuikuza sekta isiyo rasmi ya “wanyonge”: mama lishe, machinga, bodaboda, kama tegemeo kuu la wananchi! Kuni zinapikiwa prime area ya jiji - posta! Badala ya kuhamasisha uwekezaji mkubwa unaotoa ajira za maana. Wapi hamasa ya Tanzania ya viwanda?
Safi sana. Rais Magufuli yeye bado anafikiri tukiwa na infrustructure nzuri ya barabara na Flyovers na majengo mazuri yanayo pendeza ya kutoa huduma kama hospitali na mashule mambo mengine ya viwanda yatakuja yenyewe. Hapo niko na wewe. Naona amesha feli.

Tanzania inahitaji vijana wenye skill kubwa ya kubuni vitu vya kuvifanyia manufancturing badala ya wachuuzi. Yaani products creation and manufacturing na sio tu uchuuzi na production industries peke yake. Uchuuzi unalemaza ubongo na ni kweli hatutafika kokote. Mifano ipo mingi sana. Angalia nchi kama Misri, Ugiriki, Tunisia na Nigeria zina vijana wengi ambao hawana kazi. Wanazurura tu mitaani na kuwa wachuuzi. Kwa hali hii hatuwezi tukajenga nchi yenye uchumi thabiti.

Nitoe mifano ya comodities creation and manufacturing; kwa mfano utengenezaji wa Pete na mikufu mizuri ya dhahabu na almasi ambayo tuna weza uza nje na ku compete na watengenezaji wengine wa kimataifa na utengenezaji wa viatu vizuri na bora vya ngozi yetu ambavyo tutavishindanisha kwenye soko la kimataifa na sio kiatu ili mradi kiwe kiatu tu pia nyuzi nzuri na bora kwa ajili nguo na kadhalika.

Kwenye hotuba zake Rais Magufuli za Dar juzi na jana ninemwona kama amekata tamaa vile. Ile energy aliyo kuwa nayo awamu ya kwanza ya kudhani watanzania ni creative au watakuwa watu ambao wana maarifa mapana ya kuanzisha viwanda hiyo naona hana tena ndiyo maana amebaki kuwatetea wamachinga na mama ntilie ambao wewe umewaita wanyonge.

Nafikiri amesha jua kuwa watanzania ni mabogus fulani ambao hawajui umuhimu wa kutumia akili na mamlaka yao na resources zilizopo zikawaletea faida ya pamoja.

Kwa hali ambayo nimeiona kwa watanzania katika muhula huu wa kwanza wa Rais Magufuli, kusema kweli imekuwa hali ya kukatisha tamaa. Watu wenye majukumu wanakosa kabisa ubunifu wanaotakiwa kuutumia kutekeleza miradi ya kimaebdeleo.

Viongozi wengi hawajui kazi na majukumu yao. Badala ya kutumia akili na rasilimali watu ambao wako nchini wao kazi yao kupiga piga kelele za kumshangilia na kumsifu Rais Magufuli kila wakati. Rais hataki kusikia kila mara viongizi wanasimama majukwaani na kupiga kelele za "Magufuli hoyeee" na "CCM hoyeee!" Yeye anachotaka kukiona ni mafanikio. Na Mafinikio sio takwimu tu za pesa bali improvement ya maisha ya watu.

Nitoe mfano hapa, wakati Rais Magufuli anamwapisha Naibu waziri wa madini Dodoma alimwambia kuwa aende akaangalie uwezekano wa kuanzisha kiwanda cha kuoka chuma yetu wenyewe kwa kuwagawia hao wenye viwanda vya kutengeneza hizo nondo maeneo yatakayo wawezesha wao kuchimba chuma.

Mpaka sasa hivi sidhani kama Waziri wa madini Biteko na Naibu wake wamesha chukua initiative yoyote ya kuona namna gani huo mtambo wa kuoka chuma unasimamishwa nchini. Maana kweye mkutano wa madini uliopita wiki hii sikusikia mpango wowote kuhusu mtambo wa kuoka chuma kwenye kauli zake wala naibu wake. Wao walicho fanya ni kuitisha mikutano au mijadala ya discusdions badala ya substance. Rais amesha waambia lakini.

Katika mpango huu wa mtambo wa kuoka chuma nitakacho ona mimi ni kwamba wao watafanya kile kile ambacho Rais amewaambia, cha kuwapa hao watengenezajia wa nondo maeneo ya kuchimba chumba wakati wanajua kuwa haita work. Chuma, yaani steel haitengenezwi hivyo. Ingekuwa rahisi hivyo mbona hivi sasa tungekuwa na viwanda vidogo vidogo kibao vya kutengeneza chuma.

Mimi ningewashauri kupanga haraka iwezekanavyo utekelezaji wa kusimamisha mtambo wa kuoka chuma kwa hali na mali. Jinsi ya kufanya wasisubiri mpaka mzungu atoke Ulaya au Amerika au mhindi na mchina aje awekeze, hata kuja mtu. Wizara iwakusanye wataalam wake wanaojua chuma ni nini, wanafunzi, watengezaji wa nondo na vyuma vingine wakubwa na wadogo nchini, wataalam wote wa metallogy, mechanical-, process- na designengineering na watu wa Material science na smithy watanzania walioko nje na ndani ya nchi wajadili nini cha kufanya, wapi waanze na nini kinaendelea badala ya kukusanya waandishi wa habari kem kem na wapiga domo kama akina Professor Lumumba, wa nini hao? Haiwasidii kitu na wala hawatoi mchango wowote kwenye utaalam wa kuoka chuma.

Mimi naumia sana ninavyo ona mawaziri wenye dhamana kama hawa wanavyoshindwa kufanya vitu vidogo kama hivi vya kukusanya wataalam wetu wakajichimbia kwenye hotel au Camp na kujadili mambo ya kimkakati kama huu wa kusimamisha mtambo wa chuma. Katika maswala kama haya waziri ndiye anatakiwa ajue nini anataka.

Katika maswala kama haya seriousnes na dhamira zinahitajika na sio kujali costs na wasifanye Shows. Wahakikishe wanawapata wataalaam husika na kujichimbia ili wakitoka hapo wanatoka na majawabu sahihi.

Niwape Tips tu. Watumie njia ambayo Prime Minister Churchill wa Uingereza alivyo fanya kwenye WW II au Queen Elisabeth I. kwenye vita kati ya nchi yake Uingereza na Spain. Mtu mwingine wa kumchukulia kama mfano ni Rais mwenyewe kwenye ile ishu ya makinikia na BARRICK GOLD.
 
Ukiangalia watanzania wa hali ya chini tangia zamani walizoea kuonewa sana na walizoea kabisa hayo maisha, lakini amekuja John Pombe amewafungua macho hawa watu duni na kuwaambia kuwa mlikuwa mnaonewa.

Tazama mazingira ya kazi za bodaboda, mama lishe, wafanya biashara ndogondogo, wachimbaji wadogo, wakulima wadogo na wengine leo hayafanani kabisa na kabla ya kuingia Dr. John Pombe.

Je. Akiondoka huyu mtu atakaye fuata kama akishindwa kutimiza ya mtangulizi wake au akija mwanasiasa tupu na kuwa mpiga mdomo tupu na maonezi kurudi kama zamani si kutakuwa hakutoshi na siitakuwa vita ya wenyewe kwa yenyewe
We akili huna kabisa,maisha ya hao bodaboda,mama ntirie yanafanana na yapi sasa?sukari ilipopanda kutoka 1600 mpaka 3000!hao bodaboda haiwagusi?
Uwezo wa kununua wa wananchi unapopungua,hata hao bodaboda hawapati wateja,safari ya buku,wanachaji miatano tu,sasa uzuri wa maisha upo wapi?

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Hata wajinga na wapumbavu pia huzeeka
Magufuli is the President for eternal. Atake asitake. Uko sahihi. Akiondoka mapema ajue kuwa Tanzania haitakuwa salama tena. Mimi binafsi namsihi aendelee mpaka mihula minne. Akijifanya mkaidi ajue kuwa amani anayo ililia haitakuwepo tena.

Umesema ukweli mtupu kuwa watanzania walio zoea kunyanyasika hawatakubali tena kama kiongozi atakaye mfuata Rais Magufuli kuwa wa upande wa walio navyo, that is for sure.
 
Hizi propaganda mfu kawapigie wazee na watu wa kijijini waliopoteza ramani maana hawajui lolote. Ni kwakuwa amefanikiwa kudhibiti vyombo vya habari, angepewa ukweli wake kuhusu kuharibu maisha ya watu. Na alijua jinsi watu hawamkubali mpaka akaamua kunajisi uchaguzi.
Watu wanataabika bila sababu za msingi
 
Basi tuache aendelee kuwepo ili tusijegombana😆😆
 
Hatukatai yapo mengi mazuri. Pia jiulize hao bodaboda wanamiliki hizo bodaboda ama wanaendesha tu. Je, wenye pikipiki ni nani hasa.
Ujue kuna mtu kajaza pikipiki na anangojea tu kukusanya na pengine yuko kwenye mfumo. Hivi hitu vinataka uchambuzi sio tu kusema.
 
Ukiangalia Watanzania wa hali ya chini tangia zamani walizoea kuonewa sana na walizoea kabisa hayo maisha, lakini amekuja John Pombe amewafungua macho hawa watu duni na kuwaambia kuwa mlikuwa mnaonewa.

Tazama mazingira ya kazi za bodaboda, mama lishe, wafanyabiashara ndogondogo, wachimbaji wadogo, wakulima wadogo na wengine leo hayafanani kabisa na kabla ya kuingia Dr. John Pombe.

Je, akiondoka huyu mtu atakaye fuata kama akishindwa kutimiza ya mtangulizi wake au akija mwanasiasa tupu na kuwa mpiga mdomo tupu na maonezi kurudi kama zamani si kutakuwa hakutoshi na siitakuwa vita ya wenyewe kwa yenyewe.
Jitihada zake ziko wazi na pia zipo changamoto. Watu wa kipato cha chini ni wengi na wanazaliwa bado.
Ufumbuzi ni upi hasa barabara za kariakoo zilizojengwa kwa gharama zitaendelea kujaa watu. Mafuriko kule. Je, tutaenda hivo milele au ni hatua ya kuanzia huku tukiweka mipango thabiti.
Kwa kuwa wanyonge unaosema wanzongezeka basi ujue miji yetu itaendelea kufurika machinga.
Ni vizuri kujiuliza kama itaweza kuwa hivo milele
 
Back
Top Bottom