Ni kama Dr. Magufuli anatengeneza vita

Ni kama Dr. Magufuli anatengeneza vita

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Ukiangalia Watanzania wa hali ya chini tangia zamani walizoea kuonewa sana na walizoea kabisa hayo maisha, lakini amekuja John Pombe amewafungua macho hawa watu duni na kuwaambia kuwa mlikuwa mnaonewa.

Tazama mazingira ya kazi za bodaboda, mama lishe, wafanyabiashara ndogondogo, wachimbaji wadogo, wakulima wadogo na wengine leo hayafanani kabisa na kabla ya kuingia Dr. John Pombe.

Je, akiondoka huyu mtu atakaye fuata kama akishindwa kutimiza ya mtangulizi wake au akija mwanasiasa tupu na kuwa mpiga mdomo tupu na maonezi kurudi kama zamani si kutakuwa hakutoshi na siitakuwa vita ya wenyewe kwa yenyewe.
 
sorry nikuulize. hayo mazingira ya boda boda na mama ntilie yamebadilikaje?

coz sio kipya au wao kupanda kiuchumi
 
Hao ni zao la kushindwa kwa awamu hii kuhusu sera ya ajira.Hao wote ilitakiwa wawe kwenye uzalishaji Ili kukuza export tupate pesa nyingi za kigeni tuweze fanya miradi kwa pesa zetu na sio kutegemea mikopo.

Bodaboda na machinga hawa ni madalali wa kuuza vitu vilivyozalishwa china wanasaidia kuukuza uchumi wa China.

Ilitakiwa wote waingizwe kwenye uzalishaji mashambani, viwandani, kwenye uvuvi,kilimo na sio kuzagaa mijini kama daraja la wanasiasa uchwara wasiotazama future ya taifa kwa kutengeneza bomu la kesho wakijua kesho awapo.
 
Hao bodaboda ndo usiwataje kabisa, kuna siku kidogo anidondoshe akikimbia askari wa jiji. Yaani huku town wanaishi kama wakimbizi kila wakati wanapepesa macho kuangalia wapuuzi kama wapo

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Na huyo boda boda bora alikuwa mwepesi mwingine anakutia mshono anakimbia anakupigia simu ukatoe chombo hapo ujiandae faini ya laki mbili na kama hauna sticker ya Latra ujiandae na faini ya laki so jumla ujipange na laki tatu na thelathini au zaidi.
 
Mpaka aondoke madarakani barabara zote zitakuwa zimejaa wamachinga....akija mwingine awaondoe Amani itakuwa shakani....
 
Tumeingia uchumi wa kati huku tunajivunia kuikuza sekta isiyo rasmi ya “wanyonge”: mama lishe, machinga, bodaboda, kama tegemeo kuu la wananchi! Kuni zinapikiwa prime area ya jiji - posta! Badala ya kuhamasisha uwekezaji mkubwa unaotoa ajira za maana. Wapi hamasa ya Tanzania ya viwanda?
 
Ukiangalia watanzania wa hali ya chini tangia zamani walizoea kuonewa sana na walizoea kabisa hayo maisha, lakini amekuja John Pombe amewafungua macho hawa watu duni na kuwaambia kuwa mlikuwa mnaonewa.
Tazama mazingira ya kazi za bodaboda, mama lishe, wafanya biashara ndogondogo, wachimbaji wadogo, wakulima wadogo na wengine leo hayafanani kabisa na kabla ya kuingia Dr. John Pombe.
Je. Akiondoka huyu mtu atakaye fuata kama akishindwa kutimiza ya mtangulizi wake au akija mwanasiasa tupu na kuwa mpiga mdomo tupu na maonezi kurudi kama zamani si kutakuwa hakutoshi na siitakuwa vita ya wenyewe kwa yenyewe
Unaandika bila kujua unaandika nini.Unataka kutuambia maisha ya wanyonge yamekuwa bora chini ya Magufuli?
 
Ukiangalia watanzania wa hali ya chini tangia zamani walizoea kuonewa sana na walizoea kabisa hayo maisha, lakini amekuja John Pombe amewafungua macho hawa watu duni na kuwaambia kuwa mlikuwa mnaonewa.
Tazama mazingira ya kazi za bodaboda, mama lishe, wafanya biashara ndogondogo, wachimbaji wadogo, wakulima wadogo na wengine leo hayafanani kabisa na kabla ya kuingia Dr. John Pombe.
Je. Akiondoka huyu mtu atakaye fuata kama akishindwa kutimiza ya mtangulizi wake au akija mwanasiasa tupu na kuwa mpiga mdomo tupu na maonezi kurudi kama zamani si kutakuwa hakutoshi na siitakuwa vita ya wenyewe kwa yenyewe

Hizi propaganda mfu kawapigie wazee na watu wa kijijini waliopoteza ramani maana hawajui lolote. Ni kwakuwa amefanikiwa kudhibiti vyombo vya habari, angepewa ukweli wake kuhusu kuharibu maisha ya watu. Na alijua jinsi watu hawamkubali mpaka akaamua kunajisi uchaguzi.
 
Ukiangalia watanzania wa hali ya chini tangia zamani walizoea kuonewa sana na walizoea kabisa hayo maisha, lakini amekuja John Pombe amewafungua macho hawa watu duni na kuwaambia kuwa mlikuwa mnaonewa.
Tazama mazingira ya kazi za bodaboda, mama lishe, wafanya biashara ndogondogo, wachimbaji wadogo, wakulima wadogo na wengine leo hayafanani kabisa na kabla ya kuingia Dr. John Pombe.
Je. Akiondoka huyu mtu atakaye fuata kama akishindwa kutimiza ya mtangulizi wake au akija mwanasiasa tupu na kuwa mpiga mdomo tupu na maonezi kurudi kama zamani si kutakuwa hakutoshi na siitakuwa vita ya wenyewe kwa yenyewe
Magufuli is the President for eternal. Atake asitake. Uko sahihi. Akiondoka mapema ajue kuwa Tanzania haitakuwa salama tena. Mimi binafsi namsihi aendelee mpaka mihula minne. Akijifanya mkaidi ajue kuwa amani anayo ililia haitakuwepo tena.

Umesema ukweli mtupu kuwa watanzania walio zoea kunyanyasika hawatakubali tena kama kiongozi atakaye mfuata Rais Magufuli kuwa wa upande wa walio navyo, that is for sure.
 
Wewe umewahi kuwa boda boda au mama ntilie? Na kilichobadilika ni kipi chenye faida? Yani naandika hapa nimetoka pigwa faini ya kukomeshwa na wenye mamlaka.
Acha uzushi. Wewe unafikiri ni sifa hiyo kusema sema uongo?
 
Back
Top Bottom