Ni JK au GT wa JF ndio wasiojua ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni JK au GT wa JF ndio wasiojua ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GeniusBrain, Sep 27, 2011.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Baraza la mpito la Libya limegungua kaburi la pamoja ambalo wamezikwa watu wapatao 1200 ambapo limetangaza litatumia vipimo vya kutambua vinasaba (DNA) ili kujua ndugu wa wafu hao. Ilipotokea ajali ya MV spice landers zanzibar, Rais JK aliwaomba wataalam watumie DNA ili kutambua maiti za wale ambao waliozikwa na serikali ili kujua ndugu zao. Lakini cha kushangaza , watu humu JF walikuja juu na kumshambulia Rais kuwa alikuwa hajui asemalo. Hii yaonyesha kabisa, kumbe GT wa humu JF ndio hawajui wasemalo na kuandika vitu kwa ushabiki badala hali halisi.
   
 2. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  kwa akili zangu nadhani inatakiwa kuwa na database ya dna ili kufanya comparison na zile ambazo zitapatikana,
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  'Rais' alisema ikibidi DNA itumike..........haikubidi
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu siyo lazima kuwa na data base ya DNA profiles ili uweze kutambua maiti. Unahitaji ndugu wa marehemu ambao wanachangia wazazi ili uweze kulinganisha DNA zao.

  Siyo kazi ngumu sana kwani pale kwa Mkemia Mkuu wanafanya...Kama kipimo hiki hakikutumika kwa wahanga wa Meli huko Zenji ni uzembe wa serikali!
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ogopa Wanasiasa bwana GB!
  Ishu ya Libya haijajiegemeza kwenye u-political vampire'

  Ishu ni kwamba Mkubwa alikurupuka kusema, wakati anajua wazi kuwa zoezi hilo maandalizi yake yatachukua miaka kadha, na hadi kufikia ukamilifu itakuwa yeye hayupo madarakani!
  Kama ishu ndogo za kuunda kamati kuchunguza chanzo cha mlipuko wa silaha hazitoi majibu kwa miaka, itakuwa suala hilo la uchunguzi wa kisayansi wa DNA?...
  JE REAGENTS ZIPO ZA KUTOSHA?...Maabara vipi?...Je related cases za kawaida zisizo za emergency zinakuwa solved kwa efficiency gani?
  Kuna maswali mengi zaidi ya majibu kwenye kauli ya JK!
   
 6. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Kwani hapa hoja hasa ni nini? Rais kusema? Mambo mangapi yametolewa tamko na Rais
  lakini hadi sasa hayajatekelezwa au hayatekelezeki? Kwanza tunajua gharama ya DNA?
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hujamwelewa Silly alichomaanisha, Tanzania hatuna DATA BANK ya DNA hata hizo DNA za wazazi wa marehemu unaowasema hazipo sehemu yeyote ile itabidi na wao wapimwe kwanza. Nchi za wenzetu mtoto anapozaliwa anakuwa na file lake likiwa na vipimo vya DNA kwa hiyo inakuwa rahisi kumtambua janga linapotokea, kwa Tanzania ni vigumu sana kwa vile hatuna data bank yeyote mbali ya cheti cha kuzaliwa Birth certificate hata hicho kwa wazazi wetu ni vigumu kuvipata sembuse vipimo vya DNA zao. Ndio maana watu walikejeli JK aliposema maiti watapimwa DNA kutambua ndugu zao ambao hajui atapata wapi vipimo vyao.
   
 8. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu, umumwambia mambo mengi ya kumtosha kabisa.

  1) Anaijua maabara ya mkemia mkuu huyu?? dokezo.....reagents ni issue kubwa sana pale.
  2) Kama hamuwezi kuifikia meli, mtapima vinasaba vya samaki au??.......Mmeleta wazamiaji wanaozama 53m only, wakati mnajua pale Nungwi pana zaidi ya 300m. Mlifikiri hiyo meli ingezama ki-sharobaro??

  Watuwalimpiga Kikwete kwasababu alitoa political statement isiyo na mashiko.
   
 9. B

  BANNED 4EVER Member

  #9
  Sep 27, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwani dhamira si kujua ndugu zao walioko hai ili wafu wale waweze kutambulika walikotoka????
  data base ya nini wakati ndugu zao wapo??????
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wewe nawe maiti imeharibika labda imeliwa na samaki na kubaki mifupa utaitambuaje wakati kuna maiti(mifupa) zaidi ya mia mbili.
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Rais alisema nini kuhusu waliozembea na kupelekea meli kuzama???? na akisema ni kweli atatenda??????????
   
 12. m

  mbasamwoga Member

  #12
  Sep 27, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna habari za mil 600 kumwagwa ili msifie ccm na serikali yake. Vipi na wewe umepewa laptop hiyo kusifia kaka..... Hongera
   
 13. l

  luckman JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Zero brain hawezi kuwa na kitu kichwani! Hukum watu kwa matendo yao!
   
 14. W

  WIZARD Member

  #14
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mara nyingi viongozi wanaongea kujiongezea umaarufu tu, hata hao viongozi wa serikali ya mpito ya wali bia hamna lolote.
   
Loading...