Ni ipi athari ya kuwa na kiongozi anayetokea katika familia ya kimasikini au kitajiri? Funguka

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,556
2,996
Stori za mtaani zinasema kwamba Aliyekuwa waziri Mkuu kipindi cha Kikwete na kujiuzulu Marehemu Edward Lowasa Alikuwa ni mmoja wa vijana wenye kutoka familia ya kitajiri na mwenye shauku ya kuongoza nchi,ila kwa bahati mbaya alipitia katika vizingiti viwili akiwa pale CCM moja, Mwalimu Nyerere na Kikwete hivyo ilimlazima Lowasa kutafuta njia nyengine kufikia lengo lake japo hakuweza kutimiza mpaka kufa kwake.

Utaratibu wa kuongozi kutoka familia za kimasikini ni kama desturi kwa Tanzania; kwani tumeshuhudia Marais kadhaa wakitoka familia za kisasikini na kuongoza Taifa hili kwa Mwongo mmoja huku Chama Masikini kama kinavyojinasibu kwenye Bendera Nyundo na Jembe imeliongoza Taifa Tangu uhuru ila kwa bahati mbaya Hatujaweza kuanzisha jambo na Kufikia lengo kwa asilimia 90.

Bahati mbaYA iliyoje,Taifa hili limeingia katika mnyororo huo wa umasikini,sitambui sababu ya Viongozi wetu kuwa Masikini, kauli za viongozi au watendaji/watumishi wanaoajiriwa ni masikini au Tupo kwneye mnyororo wa Utumwa kutokana na hali ya ukoloni ambao tumeshaupita.

Miaka 60 chini ya viongozi masikini hatujafakiwa kwa namna tunayotaka huenda ikawa ni sababu ya kushindwa kwetu?
 
Anafaa yule aliyeishi umasikini halafu akainukia hadi kuwa Tajiri.

Au aliyeishi mid class

Ila yote kwa yote, awe na maono na huo uwezo wa kuongoza watu kuuishi utajiri walionao au wanaoweza kuwa nao (potential wealth)
 
Anafaa yule aliyeishi umasikini halafu akainukia hadi kuwa Tajiri.

Au aliyeishi mid class

Ila yote kwa yote, awe na maono na huo uwezo wa kuongoza watu kuuishi utajiri walionao au wanaoweza kuwa nao (potential we
viongozi unaowasemea ni hao kina kikwete,Samia na wengine
 
Umasikini ni LAANA
Hilo halina ubishi
Masikini akipata hela anasahau umasikini aliokuwa nao
Na kwa sababu hajui thamani ya hela hapo akiwa kiongozi anaanza kumwaga hovyo maana hajui anachofanya

Kinyume na tajiri maana yeye ameisha zishika aidha amekulia utajiri au amefanya biashara na kujua thamani ya hela
Kwa hiyo hata akiwa kiongozi atajitahidi kufanya hata biashara ndani ya majukumu yake na kuongeza na kukuza uchumi

Masikini yeye ni shida tu
Ndio maana wengi masikini hawaweki hela
Hata Malaya ni wale wale anapata laki 2 usiku kesho zimeisha
 
Kikubwa ni uzalendo haijalishi katokea kwenye umasikini au ni tajiri, kama hana uvhungu na taifa hili na watu wake, hiyo status yake haitakuwa na msaada, kama katokea kwenye umasikini ndio atazichota fedha kweli kweli, kama ni tajiri atazidi kupiga, pesa haijawahi kumkinai mtu.
 
Kikubwa ni uzalendo haijalishi katokea kwenye umasikini au ni tajiri, kama hana uvhungu na taifa hili na watu wake, hiyo status yake haitakuwa na msaada, kama katokea kwenye umasikini ndio atazichota fedha kweli kweli, kama ni tajiri atazidi kupiga, pesa haijawahi kumkinai mtu.
TENA WENGINE WAKIPATA PESA NDIO WANABADILIKA
PESA SABUNI YA ROHO
 
1. JULIUS NYERERE
Nyerere baba yake alikuwa chifu hivyo sio maskini, Nyerere kasoma kwa kupendelewa na wazungu sababu ya baba yake. Ni mtu aliyezoea kwamba kiongozi hahojiwi sababu aliona kwa baba yake. Ndio maana watu kama Oscar Kambona waliokuwa intelligent na walioenda shule kwa tiketi ya akili zao hakuwapenda kwa kuwa walikuwa na critical thinking na wanatoa alternative sio ndio mzee. Na Nyerere akiwa Makerere alitokea kulichukia kabila alilochukia siku zote sababu walimuona average na walishangaa alifikaje pale.

Hata masomo aliyosoma UK pamoja na privilege zote za background utaona angezaliwa kwa mkulima au mfugaji alikuwa mtu wa kawaida sana. Pamoja na hizo hasara za background yake, zilikuwa na faida pia.

2. HASSAN MWINYI
Mwinyi sijui historia yake ila alikuwa humble guy, hivyo alikuwa rahisi kushauliwa. Mwinyi namchukulia kama Rais aliyekuwa average kichwani, hakuwa kipanga ila aliweza kushauriwa na kusikiliza anaoamini wanajua.

3. B.W. MKAPA
Mkapa alikuwa smart kuliko wote, yeye ndio alikuwa maskini zaidi. Alikulia kwenye mateso na kutengwa mama yake nyumbani kwao ndio maana hakupapenda uko hata kustaafu. Mkapa ndio kiurahisi angeweza kuwa sadist kuliko marais wote Tanzania hii sababu ya background yake ya kinyonge na kunyanyaswa. Na alikuwa Rais mfupi zaidi, angeweza kuwa na Napoleon syndrome (short man syndrome) ile mtu mfupi anajitutumua ili uwepo wake uonekane na kila muda anajishuku unamdharau kwa kimo chake. Mkapa hakuwa hivyo.

4. J.M. KIKWETE
Kikwete hakuwa maskini, baba yake alikuwa na cheo serikali ya Nyerere. Nepotism ilimbeba Kikwete na mfumo huohuo aliutumia serikalini, "kamlete system/we unamjua nani". Na ndio huo alitaka kuutumia kwa B. Membe. Kwa asili ya Pwani ni shughuli kwa wingi, hata yeye serikali yake ilikuwa na hafla na shughuli nyingi na safari za kutosha.

5. JOHN MAGUFULI
Huyu kwao hawakuwa maskini, alipofukuzwa shule (wengine wanadai alifeli Katoke Seminary) alipelekwa Lake Secondary, kwa kipindi hicho huo sio umaskini. Alikuwa sadist kwa mbali na ukorofi wa kawaida kwa jamii ya wafugaji. Hakuwa very bright ila tu alijua sana kukariri, na wabongo mtu akikariri wanadai ana akili. Alikuwa na msimamo na kuamini anachokiamini. Huyu angekuwa baba angeweza kukopa kujenga nyumba ya kuishi ili asifiwe, ila sio kukopa kuendeleza biashara inayorudisha faida na deni lijilipe.

6. SAMIA SULUHU HASSAN.
Huyu nyinyi wenyewe si mnaona?

Background ya watu wote awe gaidi mkubwa, serial killer, kiongozi, msanii au nani huwa inaonekana kwenye matendo yake na maisha yake.
 
Back
Top Bottom