Nimekuwa napata shida sana kupata njia nzuri ya kutuma na kupokea fedha kutoka nje ya Tanzania. Kwa muda mrefu nimekuwa natumia Western Union na MoneyGram kwa sababu ni njia za uhakika na naweza kupokea kiasi kikubwa cha pesa. Ila njia hizi zina changamoto zake ambazo zinanifanya niendelee kufatua njia nyingine.
Baadhi ya changamoto ni
Ningependa msaada wenu wana JF kujua ni njia/kampuni gani rahisi na salama kutuma na kupekea fedha kutoka nje Tanzania.
Baadhi ya changamoto ni
- Lazima nifike benki au kwa wakala wa western union ndio uweze kupata fedha zangu, huwa hii inazingua sana hasa kama nipo sehemu ambayo hakuna agent au benki yenye Western Union.
- Kama kuna makosa (hata ni herufi moja tu) kwenye majina huwezi kupokea fedha.
- Ni ghari sana kutuma pesa, unaweza kuta gharama za kutuma zinakaribiana na pesa unayotuma kama ni kiasi kidogo.
- Exchange rates zao huwa sio rafiki, wanauza fedha za kigeni kwa gharama ya juu.
Ningependa msaada wenu wana JF kujua ni njia/kampuni gani rahisi na salama kutuma na kupekea fedha kutoka nje Tanzania.