Ni huduma gani bora ya kutuma na kupokea fedha nje ya Tanzania?

Putenga

Member
May 1, 2019
41
25
Nimekuwa napata shida sana kupata njia nzuri ya kutuma na kupokea fedha kutoka nje ya Tanzania. Kwa muda mrefu nimekuwa natumia Western Union na MoneyGram kwa sababu ni njia za uhakika na naweza kupokea kiasi kikubwa cha pesa. Ila njia hizi zina changamoto zake ambazo zinanifanya niendelee kufatua njia nyingine.

Baadhi ya changamoto ni
  1. Lazima nifike benki au kwa wakala wa western union ndio uweze kupata fedha zangu, huwa hii inazingua sana hasa kama nipo sehemu ambayo hakuna agent au benki yenye Western Union.​
  2. Kama kuna makosa (hata ni herufi moja tu) kwenye majina huwezi kupokea fedha.​
  3. Ni ghari sana kutuma pesa, unaweza kuta gharama za kutuma zinakaribiana na pesa unayotuma kama ni kiasi kidogo.​
  4. Exchange rates zao huwa sio rafiki, wanauza fedha za kigeni kwa gharama ya juu.​
Sasa hivi naona mitandao ya simu na kampuni za nje wanatoa hii huduma, lakini bado siwezi kutumia laini yangu kutuma fedha nje ya afrika na pia kwenye kupokea fedha kuna transaction volume limit ambayo ipo, hivyo siwezi kupokea fedha zaidi ya hapo. Pia nimeona NALA inataka kuleta hii huduma ila bado sijajua yao itakuwaje?

Ningependa msaada wenu wana JF kujua ni njia/kampuni gani rahisi na salama kutuma na kupekea fedha kutoka nje Tanzania.
 
Sema nchi ambayo unatuma/kupokea zaidi. Njia zipo nyingi ila sio kila njia inapatikana kila nchi au kwa urahisi ule ule.
 
World remit moja kwa moja kwa simu yako
 
Jaribu PayPal pia unaunganisha na M-pesa MasterCard
Lakini paypal huwezi ku withdraw hapa Bongo ni kusend tu. Lakini pia Mpesa mastercard huwezi pokea pesa au wewe ulishawahi kupokea fedha kwa kwenye kadi moja kwa moja ya mastercard?
 
Sema nchi ambayo unatuma/kupokea zaidi. Njia zipo nyingi ila sio kila njia inapatikana kila nchi au kwa urahisi ule ule.
Ahaa ok! Mimi huwa napoke na kutuma sana kwenda China, UK, nchi za EU, USA na UAE. Njia nzuri itakuwa ipi?
 
Ukitumia debit card vp, mbona karibu bank zote wanayo huyo huduma
Hii huwa inachukua muda mrefu sana kupokea fedha kwa sababu wanafanya wire transfer au swift hivi (sina uhakika) pia gharama sio rafiki na upokea fedha hasa kiasi kikubwa kuna paperwork nyingi.
 
Ahaa ok! Mimi huwa napoke na kutuma sana kwenda China, UK, nchi za EU, USA na UAE. Njia nzuri itakuwa ipi?

Kutuma kutoka USA njia rahisi zaidi ni Sendwave. Makato yake ni nafuu na inaenda to the mobile wallet. Unaweza kuongea nao kuongeza daily limit.

World remit pia sio mbaya ila transfer fees zake zipo juu kiasi.
 
Shukrani sana ndugu!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom