Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Mods niruhusini nimchane waziri huyu

Haya mambo ya kuhifadhihifadhi majina ndiyo yanatuchelewesha kukomesha ufisadi nchini!

Mkuu hakuna haja ya kuomba kibali kwa mods, achanwe tu! Mimi ngoja nimchane mbunge wa kanda ya ziwa aliyepigia kelele pesa ya Swiss, huyu atakuwa Luhaga J. Mpina! Tunaomba ajitokeze hadharani kujibu hizi tuhuma za Raia Mwema!
 
Wizara nyeti ni ya fedha,ulinzi,na mambo ya ndani full stop. Hapa atakua ni mchumi wa daraja la kwanza.
 
Kila kitu kimefichwa, namba ya simu, jina, aagh!
 
Zamani, vyombo vya dola ndivyo vilikuwa vinatumia maneno kama (Majina tunayahifadhi) ili kuwepuka kuharibu uchunguzi. Nashangaa hata vyombo vya habari navyo vinatumia maneno kama haya badala ya kuwataja wahusika ili vyombo vya dola vipate pa kuanzia.
 
Wizara nyeti ni ya fedha,ulinzi,na mambo ya ndani full stop. Hapa atakua ni mchumi wa daraja la kwanza.

mkuu watu hawajui nini maana ya wizara nyeti, angetumia neno idara muhimu kwa uchumi wa nchi ningemuelewa.
 
Haya mambo ya kuhifadhihifadhi majina ndiyo yanatuchelewesha kukomesha ufisadi nchini!

Mkuu hakuna haja ya kuomba kibali kwa mods, achanwe tu! Mimi ngoja nimchane mbunge wa kanda ya ziwa aliyepigia kelele pesa ya Swiss, huyu atakuwa Luhaga J. Mpina! Tunaomba ajitokeze hadharani kujibu hizi tuhuma za Raia Mwema!

Utumbo mtupu!
 
Umelewa gongo, mnatengeneza majungu hao hao mnaanza kuyakwepa, mtajeni huyo Waziri mnaetaka kumpaka matope muone kama hamjaozea segerea kwa kukosa kuthibitisha uzushi wenu.
 
Anatembelea Singida,analala katika Hoteli ****,amekabidhiwa wizara nyeti hivi karibuni (Presumably ya senti senti na chenji kidogo).
Huyu atakuwa naniiii aah naniiii.Loh jina limenitoka tena.

Halafu huyo Waziri ni member humu Jamii Forums, pia ni mkuu wa vitendo vya ugaidi.
 
....Ngoja tusubiri labda wiki ijayo wanaweza kuamua kushuka na more details ambazo zitazidi kumuweka wazi muhusika.

Uandishi wa namna hii..".mtu huyo, mrefu, jina linahifadhiwa, wa mkoa wa kaskazini, aliyeteuliwa na hivi karibuni n.k ni uandishi wa wala rushwa. Hapo wanamtonya Waziri husika ajue kwamba anajulikana , na afanye namna ya kutoa posho ili wasimuandike zaid. Hakuna umuhimu wowote kuandika habari ya hovyo kama hii na kutupotezea muda kuisoma. Raia Mwema walishacompromise na CCM siku nyingi na hawawezi kuisaliti kamwe. ANgalia wanavyopata matangazo kwa wingi, huwezi kulinganisha na MA.WI.O au Tanznia Daima ambayo hayapati Tangazo hata moja!
 
Eti waziri jambazi!! Hivi kuna aliye salama kwenye hii serikali ya CCM? Wote wananuka. Raia Mwema ni wale wale, wanachofanya ni kuhamisha mjadala muhimu wa katiba, pia ni kampeni kwa uchaguzi mkuu. Ni vita ya makambi ya URAIS.Hakuna chochote kwenye hiyo makala, upuzi mtupu. Habari iliyo moto sasa hivi KATIBA. Huu ni ujanja wa kuhamisha mjadala wa kitaifa.
 
Kabla mtu hajateuliwa kuwa waziri security services haimfanyii uchunguzi? Iweje sasa kuwepo waziri mwenye shutuma kubwa kiasi hiki? Kama hizi habari zina ukweli wowote nina hakika kabisa anajulikana na vyombo vya usalama na hata akitajwa ni nani hakuna hatua itakayochukuliwa dhidi yake.

Katika serikali hii, wenye kushika hatamu wote wameoza na hakuna hata mmoja wa kumnyooshea mwenzake kidole.

Si ajabu huyo anayewekwa madarakani hufanywa hivyo ili kufanikisha adhma za yule aliyemuweka kwenye utawala.
 
Inaudhi sana hii kitu, kama wana ushahidi kiasi hiki kwanini wasianike kila kitu hadharani? Raia Mwema najua baadhi yenu mnapita huku badilikeni katika uandishi wenu ili mkiamua kuandika habari ya ufisadi/ujangili au rushwa basi muweke kila kitu hadharani.

Gazeti bongo lilikuwa moja tu...-----------. Yaliyobaki ni magazeti ya kitchen part na yale ya kufungia chapati.
 
kaka hiyo inatokana na kanuni za kiuandishi,lazima umuhoji kwanza mhusika akikujibu ndo unataja jina,bila kusikiliza upande wake wa stori,utaonekana umevunja maadili ya kiuandishi,na sababu nyingine labda wasije wakaharibu uchunguzi,ila kwa mwenye kung'amua atajua wahusika.
Kulikuwa na haja gani ya kuwahi kuiweka hewani kabla hawajawahoji wahusika? Au ndo kanuni ya kuuza habari moja mara mbili kuzingatiwa baada ya kuhojiwa na kuichapa the same habari kwa mara ya pili?
Mi naona haikuwa na haja hiyo na habari kama hizi hata kama zina ukweli bila kutaja wahusika inakuwa ni kama ya kutunga tu.
 
Haya mambo ya kuhifadhihifadhi majina ndiyo yanatuchelewesha kukomesha ufisadi nchini!

Mkuu hakuna haja ya kuomba kibali kwa mods, achanwe tu! Mimi ngoja nimchane mbunge wa kanda ya ziwa aliyepigia kelele pesa ya Swiss, huyu atakuwa Luhaga J. Mpina! Tunaomba ajitokeze hadharani kujibu hizi tuhuma za Raia Mwema!

Tambua aliyetajwa hapo ni mbunge kijana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom