HANGAYA THE CHIEF
JF-Expert Member
- Sep 10, 2021
- 329
- 947
Utangulizi:
Katika taaluma ya sheria kote dunia, na kwa kipekee hapa nchini Tanzania, ili mtu akidhi vigezo vya kuwa mshauri, au kuwakilisha watu mahakamani, au kushauri mambo msingi ya kisheria , au kuhakiki nyaraka mbalimbali ni lazima awe na taalum hiyo katika ngazi au nafasi ya uwakili.
Hivyo kwa sababu ni taaluma, ina taratibu zake kuweka kutambulikwa na jumuia wa wataaluma hao katika nchi, kwa mathalani wale waliomaliza shahada za sheria kabla ya 2007 walifanya mitihani iliyotambulika kama bar exams , na wale waliomaliza baada ya 2007 shahada zao, ilianzishwa shule ya sheria kwa vitendo (law school of Tanzania.)
Katika mifumo hiyo yote wanaofaulu wanaomba kupokelewa, na Jaji Mkuu akiwakubalia wanaapishwa na kufanywa kuwa jumuia ya mawakili, wakiwa na majukumu mbalimbali, kama mawakili, mafisa viapo, na waidhinisha nyaraka mbalimbali katika jamii; na mawakili wanaweza kuwa wakujitegemea au mawakili wa serikali.
Kama hujapitia hatua hizo hata ungekuwa una LLD (PhD), LLM. LLB, unaitwa legal officer, na chochote unachotaka kukifanya lazima uwe chini ya wakili (either private or public), kwa sababu hautambuliki kama member in professional fratenity na huna comitment za obligation ya taaluma hiyo. na hivyo ushauri wako sio ushari
Utata:
Ukifuatilia sintofahamu ya Bandari, chimbuko lake kubwa ni mkataba na wala si uwezo wa DP world kama inavyoelezwa na waunga hoja wa waarabu hao, na kimsingi mkataba ni kazi ya sheria moja kwa moja, na yeyote anayetaka kuzungumzia mkataba lazima arejee sheria, au awe na background ya sheria, aidha za mikataba mbalimbali, ikiwepo za ndani na za nje, au uwezo wa kisheria kiujumla.
Kumekuwa na mwanasheria ambaye amejinasibu kuwa alishiriki katika mchakato na kushauri, swali langu Je, "mwanasheria" huyo ni wakili? (private or public) (is he a member of professional fratenity in Tanzania? Jibu ni hapana Hamza Johari si wakili(public or private) inawezekana ni mwanasheria kwa maana labda ana LLD, LLM, LLB, lakini si wakili, na si lawyer by professional, labda ni mwanasheria kwa kumaliza degree za sheria. lakini haonekani katika kanzi data za mahakama (data base) za judiciary.
Kulijua hilo ingia kwenye (tovuti ya mahakama) www.ewakili.judiciary.go.tz. kuna sehemu ya kumjua wakili wako, (know your advocate) ingiza majina utagundua si wakili.
Wale mnaolaumu wanasheria, tujiulize kwanza, Je aliyetoa ushauri wa kisheria ni mwanasheria kwa mujibu wa taaluma yetu ya kisheria?
Na kama si hivyo, aliwezaje kufanya kazi asiyokuwa na taaluma nayo?