Ni faida kubwa kwa Yanga kutoka sare na Mbeya City

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Hii ni kwasababu:

Mbeya City ni moja ya timu inayotoa upinzani, hivyo matokeo ya mechi baina ya hii timu na timu zingine zinazofukuzia ubingwa, ni matokeo decisive katika kuja kutoa bingwa.

Kwa maneno mengine, timu vigogo(Simba, Yanga na Azam) ni lazima zihakikishe zinaishinda ama kutoka sare na hii timu na siyo kufungwa.

Yaani tuna timu nyingi lakini zisizotoa upinzani kwa vigogo wa ligi, hivyo mechi baina ya timu hizi na vigogo wa ligi sio decisive kama ilivyo baina ya timu vigogo na hii Mbeya City.

Kwa lugha nyingine, kwasababu timu zingine ni kama wasindikizaji, timu inayoweza kuamua nani awe bingwa ni ile inayotoa upinzani kwa vigogo wa ligi kama hii Mbeya City ingawa mechi bado ni nyingi.

Kwahiyo, matokeo ya mechi za nyumbani na ugenini baina ya vigogo wa soka na Mbeya City, ndio yatakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuamua kigogo yupi achukue kombe.

Simba akishindwa kuwafunga katika mechi ya marudiano huku Yanga akishinda, basi Yanga atakuwa na nafasi kubwa ya kuwa bingwa unless round ya pili timu zingine zitaacha kuwa wasindikizaji jambo ambalo naona ni gumu kutokea.
 
Kuna Namungo mliponea chupuchupu mkabebwa na tefa, wako Azam, bado hao Mbeya City, Simba yenyewe, wake Coastal mliwafunga kwao lakini hakuna uhakika wa kuwafunga DSM msiseme mko nyumbani, hii ligi bado mbichi..

Prison nao hawatabiriki, kwa ushindi wenu mnaoupata wa 1-0 kila siku lazima muanze kutetemeka tu hakuna namna nyingine.
 
Kuna Namungo mliponea chupuchupu mkabebwa na tefa, wako Azam, bado hao Mbeya City, Simba yenyewe, wake Coastal mliwafunga kwao lakini hakuna uhakika wa kuwafunga Dsm msiseme mko nyumbani, hii ligi bado mbichi..

Prison nao hawatabiriki, kwa ushindi wenu mnaoupata wa 1-0 kila siku lazima muanze kutetemeka tu hakuna namna nyingine.
Be objective, sometimes weka ushabiki pembeni na angalia facts.
 
Nilikuwa naangalia gemu ya leo kiukweli nikawa najiuliza hv Kuna timu Gani nyingine yenye upinzani kwa vigogo msimu huu km mbeya city.

Nikawa najisema moyoni kama Yanga wakiwafunga Hawa Mbeya city nawapa 100% za ubingwa mwaka huu. Japo hawajashinda lakina bado nawapa Yanga ubingwa kwa 80% coz Simba bado hawako vizuri msimu huu, wana struggle sana kwenye kushinda mechi zao
 
Be objective, sometimes weka ushabiki pembeni na angalia facts.
Which facts are u talking about Sir? football is not like 1 + 1=2, sometimes timu unayoidharau ndio itakufunga au uta draw, na isiwe kati ya hizo ulizoandika hapo, nasema tena hii ligi bado mbichi sana hasa kwa timu inayopata ushindi wa goli moja kwa mechi zake nyingi.
 
Kuna Namungo mliponea chupuchupu mkabebwa na tefa, wako Azam, bado hao Mbeya City, Simba yenyewe, wake Coastal mliwafunga kwao lakini hakuna uhakika wa kuwafunga Dsm msiseme mko nyumbani, hii ligi bado mbichi..

Prison nao hawatabiriki, kwa ushindi wenu mnaoupata wa 1-0 kila siku lazima muanze kutetemeka tu hakuna namna nyingine.
Nyie ambao hamtacheza nazo hizo timu kisa mshafuzu.
 
Kuna Namungo mliponea chupuchupu mkabebwa na tefa, wako Azam, bado hao Mbeya City, Simba yenyewe, wake Coastal mliwafunga kwao lakini hakuna uhakika wa kuwafunga Dsm msiseme mko nyumbani, hii ligi bado mbichi..

Prison nao hawatabiriki, kwa ushindi wenu mnaoupata wa 1-0 kila siku lazima muanze kutetemeka tu hakuna namna nyingine.
Huu sijui tuite ujinga kichwani?
Nyinyi mara ya mwisho kushinda hata 2 ni lini?
Mkishinda ni moja tena penalty.
 
Huu sijui tuite ujinga kichwani?
Nyinyi mara ya mwisho kushinda hata 2 ni lini?
Mkishinda ni moja tena penalty.
Mkiambiwa ukweli mnakuwa wakali kisa mmetengeneza scenario zenu za ushindi vichwani, msikariri football.
 
Leo kama Young Africans kwa matokeo ya sare kwetu sawa tumepoteza. Ila Amini Amini nakwambia It's a minor setback for a major comeback.

Wape Salamu Vituo Vinavyofata Tumeumia Sana Kwa Sare Hii.
 
Kuna Namungo mliponea chupuchupu mkabebwa na tefa, wako Azam, bado hao Mbeya City, Simba yenyewe, wake Coastal mliwafunga kwao lakini hakuna uhakika wa kuwafunga Dsm msiseme mko nyumbani, hii ligi bado mbichi..

Prison nao hawatabiriki, kwa ushindi wenu mnaoupata wa 1-0 kila siku lazima muanze kutetemeka tu hakuna namna nyingine.
huoni aibu hata! mpka sasa mna goli ngapi za kufunga nyie mnao shinda nyingi
 
Ligi ya msimu huu ni ngumu kuliko misimu mingi iliyopita.

Misimu kadhaa iliyopita ilikua ni rahisi kupata ushindi kwenye timu ambazo wachezaji wake hawajalipwa mishara au wamechelewa kufika kituoni kutokana na gharama za usafiri

Tutarajie kuona ushindani zaidi kwenye round ya pili ya msimu huu.
 
Back
Top Bottom