Kwanini Simba/ Yanga Kosa lolote lawama ni kwa marefa?

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Hizi timu za Simba na Yanga zipate matokeo au zikose siku zote lawama Ni Kati ya hizi:

1.Upangaji matokeo

-Utaskia wale wameshinda kwa sababu timu waliocheza nayo wamewapa kiasi fulani Cha pesa au mchezaji fulani kapewa kibunda ndio maana wameshinda!

2.Refa kauza mechi

-Hawa ndio wanapokea lawama, wakichezesha hizi timu za kawaida Ni fresh tu no lawama, ila kwenye mechi za Simba/Yanga Ni lawama hasa pale hizi timu mbili zinapocheza na timu nyingine na kupata matokeo tofauti na ushindi

MY TAKE
-Kuondoa Hivi vyote natamani ligi yetu iendelee kukua na kupata wawekezaji wenye Nia kubwa, na kuleta challenges kwa hizi timu mbili,

Na siku tukifika level hiyo tayari U Simba/Yanga utaisha na hata timu yetu ya taifa itakuwa Bora Sana.
 
Back
Top Bottom