Ni dhahiri Hayati Magufuli alichukiwa na wanaCCM wenzake alioziba mianya yao ya ufisadi

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Alidhibiti kwa kila namna wanaCcm wenzake walioliibia taifa la Tanzania kupitia sekta ya umeme. Hawa ni wale ambao kila mwaka walipiga dili kujifanya wanasaidia taifa kudhibiti upungufu wa umeme nchini ila kumbe walijinufaisha kwa asilimia kubwa.

Aliwadhibiti wanasiasa wenzake wa Ccm ambao walizoea kujizolea mali ya umma kadri wanavyotaka.

Hawa ni wale ambao kwao kupigia debe miradi ya kifisadi ili wapate hata ten parcent ni jambo la kawaida.

Leo hii wamerudi kwa kasi kama ilivyokuwa miaka ya 2005-2015.
 
Alidhibiti kwa kila namna wanaCcm wenzake walioliibia taifa la Tanzania kupitia sekta ya umeme. Hawa ni wale ambao kila mwaka walipiga dili kujifanya wanasaidia taifa kudhibiti upungufu wa umeme nchini ila kumbe walijinufaisha kwa asilimia kubwa...
Habari ya chato?

Alizibiti wasio wake kuiba huku akiiba yeye?

Sema hapa ilikuwaje Mayanga Construction ikapewa tender ya ujenzi wa ndege chato?

Ujenzi wa Uwanja wa ndege Chato fedha ziliidhinishwa na Bunge lipi?
 
Alidhibiti kwa kila namna wanaCcm wenzake walioliibia taifa la Tanzania kupitia sekta ya umeme. Hawa ni wale ambao kila mwaka walipiga dili kujifanya wanasaidia taifa kudhibiti upungufu wa umeme nchini ila kumbe walijinufaisha kwa asilimia kubwa...
Kwa hiyo akapendwa na wana CCM waliozibuliwa mianya yao ya ufisadi kama kina Sabaya, Makonda, pole pole, bashiri na wenzao?
 
Alidhibiti kwa kila namna wanaCcm wenzake walioliibia taifa la Tanzania kupitia sekta ya umeme. Hawa ni wale ambao kila mwaka walipiga dili kujifanya wanasaidia taifa kudhibiti upungufu wa umeme nchini ila kumbe walijinufaisha kwa asilimia kubwa...
Tuliposema tunataka katiba mpya alikuwa anajibu kwa kiburi kuwa katiba mpya sio kipaombele chake. Akaua mifumo yote ya kuhoji, huku akinajisi chaguzi za nchi hii ili kuwapa nafasi wanaccm wenzake.

Leo hayupo, ila kakabidhi nchi kwa wahuni wenzie. Mmebaki mnalilia wakati alipokuwa anavuruga utawala wa sheria mlikuwa mnakenua eti kaifanya CCM kuwa imara. Hivyo CCM sukuma gang kaeni kwa kutulia muone CCM Msoga line wanavyopiga bao.
 
Tuliposema tunataka katiba mpya alikuwa anajibu kwa kiburi kuwa katiba mpya sio kipaombele chake. Akaua mifumo yote ya kuhoji, huku akinajisi chaguzi za nchi hii ili kuwapa nafasi wanaccm wenzake. Leo hayupo, ila kakabidhi nchi kwa wahuni wenzie. Mmebaki mnalilia wakati alipokuwa anavuruga utawala wa sheria mlikuwa mnakenua eti kaifanya CCM kuwa imara. Hivyo CCM sukuma gang kaeni kwa kutulia muone CCM Msoga line wanavyopiga bao.
Ndugu una hakika na haya unayomsingizia hayati JPM?
 
Leo hii wamerudi kwa kasi kama ilivuokuwa miaka ya 2005-2015.
Inatisha. Tatizo la maji Dar linaweza kuelezeka kwamba mto ruvu maji yamepungua.

Chanzo cha maji kwa Dodoma ni visima virefu kijijini Mzakwe nje ya jiji la Dodoma. Cha kushangaza sasa hivi Dodoma, ndani ya mwezi mmoja, kuna uhaba mkubwa wa maji. Sitaki kuamini kwamba maji kwenye visima hivyo yamepungua.

Kuna kitu kinatengenezwa.
 
Back
Top Bottom