Ni CCM pekee ndiyo inaweza kuleta Katiba Mpya

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Apr 26, 2022
259
353
Harakati za kudai Katiba Mpya Tanzania ni harakati za muda mrefu sana, takribani miaka 30 iliyopita baada ya Tanzania kuingia rasmi katika mfumo wa vyama vingi. Watu wengi wamefungwa, kuteswa na wengine kupoteza hata maisha yao kutokana na kupaza sauti katika kudai Katiba Mpya.

Licha ya damu kumwagika na vilio vya majonzi kutamalaki juu ya madai ya katiba mpya, lakini kwanini bado inakuwa ni ndoto isiyofikiwa katika upatikana na wakati hiyo. Jaribio pekee ambalo lilifikia karibu sana katika kuipata katiba hiyo ni mwaka 2014 kwenye mchakato wa rasimu wa Warioba, baada ya hapo hakuna chochote kilichotokea hadi leo zaidi ya mayowe ya wapinzani kudai Katiba Mpya. Hii maana yake ni nini?

Hii ina maana kwamba CCM ndio muhimili mkuu katika upatikanaji wa katiba hapa nchini, bila CCM hakuna katiba mpya. Upinzani mtaumia makoromeo na kukauka damu kwa kupiga nduru mkidai katiba, kwa mtindo huo katu hamtoipata hiyo katiba, na mbaya zaidi, hakuna kitu kinawezakufanya juu ya hili.

Mnachopaswa kufanya, sio kudai katiba bali kuomba katiba huku mkiambatanisha maombi yenu na nia ya dhati kabisa. Mumedhihirisha kuwa na nia ya dhati baada ya kugundulika kwamba msukumo wa katiba mpya unatoka nje zaidi ya ndani. Yaani kuna fungu maalumu linakuja Tanzania kufadhili harakati hizo, na mnapima metrics kwenye mitandao ya kijamii kama sehemu ya harakati zenu.

Hiyo siyo sawa, hao wanaowatuma wana maslahi gani na Taifa letu? Ukweli ni kwamba unaweza ukaishi siku nzima bila kusikia neno katiba huku mtaani, lakini mitandaoni utalikuta. Hii ina maana kwamba watanzania sio jambo wanalotaka, bali kuna watu, hasa CHADEMA wanalipa chepuo kama ni hitaji la watanzania ila wasikaushe mirija ya ufadhili wa fedha kutoka nje. Madai ya Katiba haya nia ya dhati ndio maana, CCM imeziba masikio.

Ombeni tupate Katiba Mpya, hata CCM wanajua sana kwamba katiba hii ina changamoto, pengine watazirekebisha, sio kuleta mpya, lakini kwa utaratibu maalumu utakazingatia wakati, adabu, busara na malengo makuu wa taifa letu ambayo yatahakikisha kulinda umoja wetu na upendo. Katika Mpya kuna siku itapatikana, lakini sio kwa sababu CHADEMA imepiga sana kelele, bali kwa sababu CCM imetaka.
 
Back
Top Bottom