Walikuwa wenzetu katika mapambano. Walikuwa majemedari wa kuaminiwa. Kwa kweli walikuwa wapiganaji na tuliwategemea. Ghafla, wakabadilika. Wakaanza kutushawishi tubadili namna ya kupambana, eti tupambane kistaarabu na kizalendo dhidi ya adui. Wakati mwingine walitutaka tumuulize adui tumpige wapi na kwa silaha gani. Wakaanza kuwaambia adui zetu mahala tunapoweka silaha na wakati mwingine kutushambulia na baadaye kuomba msamaha. Je hao bado ni wenzetu?