Ni aibu kwa USA kutotambua Uislam katika sherehe za kuapishwa kwa Trump

Status
Not open for further replies.
pia ungeelezea kuhusu wakristo wanaochinjwa nchi za kiarabu.Iran saud Arabia.mfano saud Arabia hurusiwi hata kuingia na biblia.tatizo LA waarabu wanataka wao wazambaze dini yao nchi Nyingine lakini hawataki dini zingine zisambae nchini mwao.trump ndio saizi yao.
 
Mbona sisi tusioamini kabisa hatukupewa nafasi hatujalalamika japo tupo wengi sana ukifananisha na nyie waislam?
 
Hahahaha umenichekesha sana tangu lini hizo nchi za kiarabu. Embu ingia Google ujifunze kwanza hizo nchi ni za kikabila gani. Msiyo mnaropoka mambo hamjui.
Aisee....Hizo sio nchi za kiarabu au sio!! Turkey wanakaa watu gani?
 
Nchi za kiarabu ambazo ni za kiislamu hazina sababu ya kuutambua ukristo kwenye kuapishwa kwa sababu zenyewe zimeshajiweka wazi kwamba ni za kiislamu "Islamic states". Kama Marekani nao watajiweka wazi kwamba ni "Christian State" na sio dola ya kisekyula sidhani kama kutakuwa na shida.
Nchi za kiarabu ZISIZO za kiislamu, Huwa zinautambua Ukristo kwenye Kuapishwa viongozi?

Acheni kujifanya kama hamjaelewa swali langu
 
Nchi za Uarabuni huwa zinatambua Ukristo kwenye Sherehe za Kuapishwa?
Mkuu nchi zipo hivi;

Moja, nchi za kidini zina ongozwa kwa taratibu na sheria za kidini.. lkn sio kua raia wote wa nchi hizi ni wa dini ambayo sheria zake zina tumika kuendesha nchi hiyo..

Pili, kuna nchi zisizo za kidini japo raia wake wana dini zao. Sheria za nchi hizi si za kidini.. mfano wake ni marekani sasa..

Kwa mfafanuo huo utakua umepata mwanga kua jambo hilo limekosewa mkuu.. hata hao waislam wange paswa kupewa nafas kama kuwakilisha umat wa dini hiyo katika nchi hiyo.. kutoa nafas kwa baadhi ya watu na kuzuia wengine katika same key ni ishara ya ubaguzi tu.
 
Nimeangalia sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump lakini kilichonishangaza zaidi ni kuona madhehebu ya Kiislam yakitengwa katika sala ya kuliombea taifa na Rais Trump.

Madhehebu ya Kikristo na Kiyahudi yamepewa nafasi ya kutoa maombi lakini dhehebu la Kiislam halikupewa nafasi hiyo pamoja na takwimu kuonyesha Marekani ya sasa ina Waislam wengi.

Ni masikitiko sana kuona mpaka leo baadhi ya viongozi wa Marekani hawataki kukubali ukweli kuwa Marekani ya sasa ina waumini wengi sana wa madhehebu ya Kiislam.

Huu ni ubaguzi wa kidini ambayo unajenga chuki ndani na nje ya taifa la Marekani.

Ninajaribu kufikiria Waislam walioko Marekani wameguswa vipi na hili tukio ambalo kwa mtazamo wangu linatoa picha halisi kuhusu serikali ya Trump katika kushughulikia masuala ya Waislam na nchi za Kiislam.

Je, hii ni hatua ya kwanza katika kuufutilia mbali Uislam nchini Marekani?
Nchi ni ya kikiristo uislam wa nn kuwa na threads za akili ndugu
 
Nchi za kiarabu ZISIZO za kiislamu, Huwa zinautambua Ukristo kwenye Kuapishwa viongozi?

Acheni kujifanya kama hamjaelewa swali langu
Sasa we nimekuliza nchi gani Hiyo uliyo unadai kwamba ni yakiarabu Sio ya kislam embu nitajiye Hata moja?
 
Huyu Trump anawadanganya wajinga kama nyinyi,wakati ana vitega uchumi katika nchi za kiarabu na kiislamu.Na anafanya nao Biashara na kuwa na hisa katika makampuni ya waarabu.
Hivi hujui kuwa a company is a legal person separate from the owner?
 
Mfano mzur katika hayo ni Jirani zetu wa Zambia. Zambia is the Christian country
 
Kwani waislamu wangeenda kusoma dua ingesaidia nini ? Trump ana akili sana ndo maana hajawaalika.
 
Hakuna cha aibu wala woga, wamefanya yanayowahusu wao wewe sijui linakuumiza nini!!!! Na kama ni wingi wa waislam huko ni wangapi dhidi ya wangapi wasio waislam? Nimeona kuna sehemu wanasema waislam marekani hawafiki hata asilimia 2.
 
Nilishuhudia Maandamano fulani Mitaa ya New York jamaa wamebeba mabango yanasema ,, NO ALLAH IN AMERICA,, sasa huenda huu ni msimamo wa wengi ktk Nchi yao kwamba hawautambui wala kuuthamini Uislamu ktk nchi yao,,

Sasa tutafanya makosa kuwahukumu kuwa TRUMP amekosea kumbe ni Itikadi ya Nchi nzima
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom