MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,997
Nimeangalia sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump lakini kilichonishangaza zaidi ni kuona madhehebu ya Kiislam yakitengwa katika sala ya kuliombea taifa na Rais Trump.
Madhehebu ya Kikristo na Kiyahudi yamepewa nafasi ya kutoa maombi lakini dhehebu la Kiislam halikupewa nafasi hiyo pamoja na takwimu kuonyesha Marekani ya sasa ina Waislam wengi.
Ni masikitiko sana kuona mpaka leo baadhi ya viongozi wa Marekani hawataki kukubali ukweli kuwa Marekani ya sasa ina waumini wengi sana wa madhehebu ya Kiislam.
Huu ni ubaguzi wa kidini ambayo unajenga chuki ndani na nje ya taifa la Marekani.
Ninatambua katiba ya Marekani haijasema kuwa Marekani ni nchi ya Kikristo.
Ninajaribu kufikiria Waislam walioko Marekani wameguswa vipi na hili tukio ambalo kwa mtazamo wangu linatoa picha halisi kuhusu serikali ya Trump katika kushughulikia masuala ya Waislam na nchi za Kiislam.
Je, hii ni hatua ya kwanza katika kuufutilia mbali Uislam nchini Marekani?