Ni aibu kama tutaanza kupamba hata kwa vitu vya kipuuzi

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,514
Plato alipata kusema. "We can easily forgive a child who is afraid of the dark; the real tragedy of life is when men are afraid of the light"

"Tunaweza msamehe kirahisi mtoto anayeogopa giza. Janga katika maisha ni pale ambapo mtu mzima anaogopa mwanga"

Si tafsiri rasmi.

Tunapoendelea na Serikali iliyo chini ya Rais Samia Suluhu. Kumeibuka kama kawaida wacheza zeze kama ilivyokuwa kwa Dr. Magufuli.

Bahati mbaya sana watanzania wengi huwa hawapendi kufikiria,kuhoji na kutafakari. Kipindi cha Magufuli sikuwahi kuwa mfuasi wake. Binafsi sipendi kuwa mfuasi au mcheza ngoma wa chama au kiongozi yeyote.

Waliwahi msema mengi ambalo nlilipinga sana kuwa ni la kipuuzi ni kuwa hakujua kuzungumza kiingereza. Hii sikuona hoja. Sababu kiingereza si lugha yake.

But pia kujua au kutojua kiingereza si kigezo. Mimi najua vizuri kiingereza. Lakini sijachaguliwa kuwa Rais au Mbunge. Nabaki na kiingereza changu nikiwa ni Mtanzania.

Shuleni kuna watu ambao walikuwa wanafahamika kama "mangwini" hawa walikuwa ni watu wanaobobea kwenye lugha. Ukienda kwa wanaosoma michepuo ya Kilimo,Sayansi Hawa hawakuwa wazuri katika lugha hata utanashati.but haimaanishi hawakuwa na akili. Most of them walikuwa ni best katika masomo yao.

The same kwa aliyekuwa Rais. Usitegemee mwalimu wa kemia,fizikia au hesabu akawa mzuri kama wa kiingereza,historia n.k

Lakini bado lugha haijawahi kuwa kigezo cha kupima akili ya mtu au ubora. Watoto wa kizungu wangekuwa wanatutisha sana.

Mimi nliwahi kuandika Insha nzuri ya kiingereza kuliko Mwingereza mwenyewe. Mwisho wa siku naye alirudi kwao anaendelea na maisha yake nami nipo Tz na kiingereza changu.

Tunaweza mshangaa mtu ambaye hana Elimu anapodhani kiingereza ndiyo Elimu. Lakini itakuwa janga kubwa sana kama mtu ambaye amesoma naye akaamini kiingereza ndiyo Elimu.

Tulikuwa na wakata kiuno wa Magufuli sasa tunao wengine wa Samia Suluhu. Then mnategemea nchi hii Ufisadi,udhulumati na wizi utaisha. Ni ngumu.
 
..lazima Watz tuwe mahiri ktk lugha za makabila yetu, kiswahili, na kiingereza.

..Tunapaswa kujiuliza tumekosea wapi mpaka wahitimu wetu hawawezi kujieleza kwa Kiingereza, na wakati mwingine hata Kiswahili ni shida.
 
Lugha zote muhimu, Mama Samia ametumwa miaka mitano kumuwakilisha Rais wakati Rais anatembea mkoa kwa mkoa kusilikiza matatizo ya maskini.

Vyote muhimu. Maslahi ya nchi ni muhimu zaidi ya vyote.
 
Achana na hao mapunga hawajui maana ya lugha. Lugha siyo mathematics na ndiyo maana kwenye kingereza kuna Literature ambayo usomaji wake uko tofauti na common English. sasa kama wanataka kingereza waje kwangu THE LOST niwachachafye wabaki wanajishangaa. Sipendi mtu anayewadharau wenzake asee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom