NHIF jambo hili liangaliwe

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Habari wakuu
Ni matarajio yangu kuwa kwa kutumia jukwaa hili ujumbe utawafikia walengwa na hatua zitachukuliwa.

Niko katika hospitali ya rufaa ya Bugando ambayo inahudumia wakazi wa mkoa ya Kigoma, Shinyanga, Mara, Mwanza na Kagera.

Mgonjwa wangu anatibiwa kwa Bima ya NHIF tangu September mwaka jana baada ya kupata rufaa kutoka hospitali ya chini.

Jana kumekuwa hapa na hadi kufika saa 12;30 jioni husuma hazikuwa zimekamilika tukaambiwa kurudi leo . Kufika asubuhi katika jengo la Bima kuna Jamaa wawili wanafanya usajili ambapo wale walioanzia hospitali nyingine na kupewa referral number zaidi ya siku 90 zilizopita wanapaswa kurudi kwenye hospitali ya awali wakapate referral number.

Wanasema hii refaral number itakulazimu upate mpya kila wakati ukiwa unahitaji aina nyingine ya matibabu. Kwamba kama awali ulikuwa ukitibiwa moyo na baadaye ukakutaa na sukari itakulazimu use na refarl number nyingine.

Kwangu, naona wakubwa hawa ametoka maamuzi ya haraka bila kuashirikisha wadau wao.

Kwamba jana nimetibiwa hadi saa 12 jioni na kuyokabunavhukuabkadi kutoka kwao lakini hawakuambii jambo hili, ila asubuhi unatakiwa kurudi hospitali uliyoanzia!

Hospitali inauohudukia watu kutoka Kigoma hadi mara leo unamwambia arudi alikotoka akafuate refarl number kama kwamba huko anakotakiwa kwenda ni umbali wa km 10.

Kwanini wasitume ujumbe kwa wanachama wao kama wanavyofanya baada ya kupata huduma ili kuondoka kadhia hii?

Hata kama wagonjwa wao wote ni wa mwanZa. Wamewafikiria wale wagonjwa wasio na taarifa ambao wamefika hospitali kwa mbinde na sasa wanatakiwa kurudi Sekou You're, Nyamagana, Buzuruga nk?

Kwanini hata yasiwekwe mabango katika maeneo ambako Bima wanatoa huduma ili kuaafahamisha wateja wao?

Na ni nani, aliyewaambia kuwa siku 90 zitatosha kwa mgonjwa kupata matibabu na kupona. Na vipi wanaotakiwa kuendelea na klinik?
 
hiyo Referral namba mimi nimeenda ccbrt kutimbiwa magoti wamekataa mpaka niipate referral namba nahangaika kuipata sasa hii card ya bima ikiisha sikati tena maana nimepoteza 9870000/ tz sh kwa kadi hii halafu usumbufu
 
Back
Top Bottom