NHC yatelekeza miradi ya mabilioni wilayani Chato

Tangu mtu wa kazi rais wa awamu ya tano magufuli afariki miradi ya jimbo /wilaya imesimama jambo lililomkera naibu waziri wa ardhi Ms Mabura

Ukipita chato utashangaa licha ya kuwepo na mipango wa kuifanya kuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Geita kila jambo limesimama vyuo,mbuga,uwanja wa ndege, hospital kubwa ya kikanda hadi uwanja wa mpira umekufa

Wananchi wa chato wanaamini tukio la magufuli kusimamisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo baada ya kuingia madarakani anajibiwa na yeye akiwa amekufa,

USSRView attachment 1938304
Mliambiwa mapema kuwa Chato haikuwa na sifa ya kukidhi miradi iliyopelekwa huko na haiwezi kuleta tija kwa nchi.Tunalipa concequences.
 
kama nakuwa rais woote waliopitisha miradi Chato nawatafutia kesi tupa ndani hata mwaka 1
 
Hakika leo nimeamini ule msemo usemao “Marehemu hana thamani/Haki” leo Wilaya ya Chato ndio ya kukosa fedha za kumalizia miradi kweli?
Hiyo miradi haina tija ni kupoteza fedha za wananchi.
 
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula, amesikitishwa kwa kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wilayani Chato mkoani Geita.
-
Dk Mabula ambaye alitembelea na kukagua miradi hiyo leo Septemba 14, 2021 alionyesha kusikitishwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wake kunakosababishwa na ucheleweshaji wa fedha.
-
Miradi mitatu inayotekelezwa na NHC ni mradi wa mnada wa mifugo Buzirayombo wenye thamani ya shilingi Bilioni 4.8, mradi wa ujenzi wa shule maalum ya Mbuye Bilioni 5.14 pamoja na mradi wa nyumba 20 za watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato wa thamani ya shilingi Bilioni 1.139
-
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi yote mitatu Dk Mabula alisema, miradi hiyo ni muhimu na inapaswa kukamilika kwa wakati ili ianze kutumika.
-
Aidha Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Kagera, Maneno Mahenge, alimwambia Dk Mabula kuwa shirika lake la NHC limekuwa likisuasua kutekeleza kwa kasi miradi katika wilaya hiyo kutokana na kutopatiwa fedha za miradi kwa wakati.
Ingekua kipindi cha mwenda zake hii kauli ya kukosa pesa tusingeisikia..miradi ingekamilika kwa wakati.

#MaendeleoHayanaChama
 
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula, amesikitishwa kwa kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wilayani Chato mkoani Geita.
-
Dk Mabula ambaye alitembelea na kukagua miradi hiyo leo Septemba 14, 2021 alionyesha kusikitishwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wake kunakosababishwa na ucheleweshaji wa fedha.
-
Miradi mitatu inayotekelezwa na NHC ni mradi wa mnada wa mifugo Buzirayombo wenye thamani ya shilingi Bilioni 4.8, mradi wa ujenzi wa shule maalum ya Mbuye Bilioni 5.14 pamoja na mradi wa nyumba 20 za watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato wa thamani ya shilingi Bilioni 1.139
-
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi yote mitatu Dk Mabula alisema, miradi hiyo ni muhimu na inapaswa kukamilika kwa wakati ili ianze kutumika.
-
Aidha Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Kagera, Maneno Mahenge, alimwambia Dk Mabula kuwa shirika lake la NHC limekuwa likisuasua kutekeleza kwa kasi miradi katika wilaya hiyo kutokana na kutopatiwa fedha za miradi kwa wakati.

Aisee... Inatia faraja kuona madhara ya maangalizo tuliyokuwa tukitoa!
Screenshot_20210915-080309.png
 
Tutakuja ngoja tushughulike na mkataba wa Bagamoyo.
Alafu kura utaenda kuomba wapi?

Unaijua nguvu ya kanda ya ziwa au unaisikia?

Unajua kitatokea nini ikiwa watashawishiwa na chama chochote cha upinzani?

Subiri moto utawaka
 
Ni miradi iliyoanzishwa kwa sababu za ubinafsi tu lakini ilikuwa haina tija yule mtu hakustahili kabisa kupata madaraka aliyopewa, miradi mingi ilipelekwa Chato kinguvu tu.
 
Kama hiyo miradi ilishaanza ni vyema ikamilishwe tu, serikali ijitahidi kutafuta fedha, kuliko kuacha pesa iliyokwisha tumika ipotee bure, bora miradi ikamilishwe.

Hili linaweza kuwa fundisho huko tuendako, Rais wa nchi asiwe kila kitu, pawepo mamlaka ya kufuatilia na kuagiza nini kifanyike na kipi kisifanyike kwa manufaa ya taifa.
Hiyo miradi haina faida
 
Alafu kura utaenda kuomba wapi?

Unaijua nguvu ya kanda ya ziwa au unaisikia?

Unajua kitatokea nini ikiwa watashawishiwa na chama chochote cha upinzani?

Subiri moto utawaka
Acha ujinga, kura ndio nini, magu alifanyaje? Nae atafanya ushindi 98% upige usipige, uchague usichague! Hamna wa kumtisha.
 
Alafu kura utaenda kuomba wapi?

Unaijua nguvu ya kanda ya ziwa au unaisikia?

Unajua kitatokea nini ikiwa watashawishiwa na chama chochote cha upinzani?

Subiri moto utawaka
Acha mikwara mbuzi wewe kanda ya ziwa hawajawahi kuipenda CCM
 
Tulisema na Tundu Lissu akawaeleza kwa mifano mkabisha. Matokeo ndo hayo.
Pesa ya maendeleo ya nchi kodi na mikopo zote kwa miaka mitano imeeharibiwa Chato mapolini, nchi imesimama kiuchumi na imekua masikini, na uchumi umeshuka kutoka 7% mpaka 2%
Walaaniwe MaCCM wote..!
Alaaniwe Mwendawazimu wa Chato.!
 
Alafu kura utaenda kuomba wapi?

Unaijua nguvu ya kanda ya ziwa au unaisikia?

Unajua kitatokea nini ikiwa watashawishiwa na chama chochote cha upinzani?

Subiri moto utawaka
kwa nini huandika pumba wakati wote humu?
 
Kama hiyo miradi ilishaanza ni vyema ikamilishwe tu, serikali ijitahidi kutafuta fedha, kuliko kuacha pesa iliyokwisha tumika ipotee bure, bora miradi ikamilishwe.

Hili linaweza kuwa fundisho huko tuendako, Rais wa nchi asiwe kila kitu, pawepo mamlaka ya kufuatilia na kuagiza nini kifanyike na kipi kisifanyike kwa manufaa ya taifa.
Kupatikana kwa katiba mpya ndo tiba itakayokomesha maamuzi ya kiimla kama haya!
 
Chato R. I. P Chato...

Nakumbuka wakati nipo mdogo nilikua najiuliza kwa nini hapa kijijini kwetu hakuna ghorofa hata moja. Nikatia nia one day nikipata pesa nitajenga ghorofa. Ila kwa sasa hata nipate hela za ziada siwezi kujenga kwa maana haina tija kujenga ghorofa pale kijijini zaidi ya ufahari tu.
 
Back
Top Bottom