NHC yambwaga Mbowe Mahakamani

NHC yambwaga Mbowe Mahakamani

Mbowe alipe tu hakuna namna, na kama ikithibitika kuwa ni kweli aonyeshe ukomavu wa kisiasa...
 
Kwa masuala binafsi wanakimbilia mahakamani, kwa maslahi yao ya kisiasa, wanatumia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na maadamano, kudai kile kisichokuwepo, mradi waonekane wapo na wasikike
aisee umewaza kiundani sana big up
 
akina ben saa tisa , yereko nyerere, wako wapi maana ndio wanakuwa ma PS wa huyu jamaa
 
Hii inasikitisha sana kwa siasa zetu pamoja na sura halisi ya viongozi wetu
kitaifa. Je Mbowe ni kama Trump kuwepa kodi tangu miaka ya 90?

-------------
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameangukia pua mahakamani baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutupilia mbali maombi yake katika mgogoro wake wa umiliki wa jengo la Shirika la Nyumba (NHC).

Mbowe alifungua maombi mahakamani hapo kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd, akipinga uamuzi wa NHC kumuondoa katika jengo ambalo alikuwa akilitumia kama ofisi ya kampuni yake ya Magazeti ya Free Media na klabu ya Bilicanas.

Katika maombi hayo, pamoja na mambo mengine Mbowe alikuwa akidai kuwa aliondolewa katika jengo hilo jinyume cha sheria kwa kuwa hakupewa taarifa na kwamba kampuni ya udalali iliyotumiwa kumuondoa haijasajiliwa kama dalali wa mahakama.

Hata hivyo katika uamuzi wa mahakama hiyo uliotolewa leo na Jaji Sivangilwa Mwangesi, imetupilia mbali maombi hayo ya Mbowe ikisema kuwa hayana msingi

Jaji Mwangesi alikubaliana na hoja za NHC na akasema kuwa Mbowe aliondolewa katika jengo hilo kisheria.


Chanzo: Mwananchi
lissu yuko wapi yule bingwa wa kushinda kesi za dhamana. Jaji huyu ameenda kutoa haki sio kufuata ubabaishaji on technicalities ambapo kina lissu wamebobea. kama dalali hana leseni kwa jaji mtoa haki kwa mwenyewe ameona si issue.
 
Kama ana deni ni sahihi kulilipa ila mmmmhhhh, kesi imeenda haraka sana hii mpaka kufikia hatua hii.
 
Back
Top Bottom