Nguvu za giza zimevunja ndoa ya jirani yangu

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,134
5,243
Jamaa alikuwa anaishi vizuri na mkewe,wameoana kwa shangwe na furaha kubwa, wakabahatikiwa kupata mtoto mmoja katika ndoa yao.

maisha ya ndoa yalianza kubadilika baada ya rafiki yangu kuanza safari za kikazi mara kwa mara,ndipo shemeji akaanza tamaa za kimapenzi kwa kijana mmoja mkopesha vyombo kutoka kigoma.

Yule kijana alikuwa anafika karibu kila siku nyumbani kwa rafiki yangu,kwa kweli roho iliniuma sana aisee kuona dogo mshamba mshamba kutoka bush anakula mzigo wa maana sana tena wa jamaa yangu wa karibu,halafu sisi born town tupo tupo tunashangaaa.

Siku moja nimetoka zangu kibaruani jioni...nikasema ngoja nipite nikamjulie hali shem....dah! sikuamini nilichokiona kwa mboni safi za macho yangu kumkuta dogo wa kiha yupo chumbani kwa jamaa yangu wa karibu sana tunayeshirikiana kwa shida na raha...leo hii tunda lake lina liwa, mimi nikishuhudia aisee.....ikabidi nichukue maamuzi magumu ya kutaka kuingia moja kwa moja mpaka chumbani ili niweze kumuadabisha yule dogo kwa kipigo kikali,nafsi ikaniambia acha usije kuonekana nawe unahusika katika kutembea na mke wa rafiki yako niakondoka na majonzi makubwa sana moyoni safari hii niliapa nitamueleza jamaa yangu kila kitu baada ya kukaa kimya kwa muda kuona kama shemeji atabadilika baada ya kumkanya lakini wapi.

Nilipofika nyumbani usiku nikamwita wife nakumkanya tabia za kuwa na mazoea na hawa wakopesha vyombo wa hapa daslam...nashukuru wife alinielewa sana,nikawa najiuliza sijui nimwambie wife kuhusu sakata la mke wa jamaa yangu lakini roho ikawa inasita nikaamua kukausha kiume...nikavuta shuka nikasoma dua nikalala.

Asubuhi mapema nikiwa naelekea kibaruani nikaamua sasa nimpigie simu jamaa yangu kuhusu wife wake anavyomtendea ubaya ,kiasi kwamba hadi anadiriki kumleta mwanaume kwenye kitanda alichokinunua kwa pesa yake mwenyewe inatia uchungu sana....sijui shem alikosa nini jamani wanawake kwa nini mna hamridhiki?

Rafiki yangu ni kijana mtanashati aliyeajiriwa kwenye taasisi kubwa ya kifedha hapa nchini,kifupi ana maisha ya kipato cha kati amjenga nyumba,ana gari ya kutembelea ana miliki biashara kadhaa hapa mjini....kifupi pesa ya matumizi ipo,shemeji yangu ......................
 
Pole sana shemeji mtu, hiyo ni tabia ya mtu wengine mbona kawaida tu kubaki wenyewe mme akisafiri? Nitabia tu ya mwanamke huyo! Ila angalia sana ukimwambia mwenye Mme atalipokea vipi!
 
Halafu ulivyo andika kichwa cha habari tofauti kabisa na maudhui yake, mwenzetu Kiswahili vipi hukumpenda Mwl wako?
 
Sijasoma huu Uzi ila Ushauri wangu Ni

Nguvu za Kiume zitumike kutafuta Ndoa nyingine

Hayo mapepo ya nguvu za Giza yashindwe kwa Jina la Yesu
 
...............................Sijaziona bado nguvu za giza zikihusika hapo,au labda umri umesogea kiasi nimeshindwa kung'amua codes ulizotumia?

Nasoma comments labda yupo aliyeelewa nami nijue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguvu za Giza zimeingiaje hapo...!!! Una uhakika Kama rafiki yako ana-mkaza vizuri mkewe??!!? Vipi kuhusu amani ya moyo..!!...

Pesa,gari ,biashara si kitu ingawa hunogesha penzi.
Pesa si kigezo cha mtu kuridhika wanaume wengi huzani mahitaji ya nje ndiyo kila kitu kwa mke wanasahau kwamba hivyo vitu hata kwao alikuwa anavipata hapo kafuatwa yeye si kingine lakini kujifanya yupo busy hata muda wakukaa na mke ni mchache misamaki ya kwenye frigi ndiyo inamtosha wanajidanganya sana. Wake zao wataliwa sana wasipo jirekebisha
 
Pesa si kigezo cha mtu kuridhika wanaume wengi huzani mahitaji ya nje ndiyo kila kitu kwa mke wanasahau kwamba hivyo vitu hata kwao alikuwa anavipata hapo kafuatwa yeye si kingine lakini kujifanya yupo busy hata muda wakukaa na mke ni mchache misamaki ya kwenye frigi ndiyo inamtosha wanajidanganya sana. Wake zao wataliwa sana wasipo jirekebisha
Wanaume wengi hawalielewi hilo..wake zao wakiliwa wanaanza kulalamika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom