Kuna nguvu za giza zinasukuma vijana kuoa

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,850
Ndugu kwa masikitiko makubwa.

Ipo nguvu iliyopo mioyoni mwa wazazi wetu, ndugu, jamaa na marafiki na hata wazee wetu kabisa ya kumlazimisha mara kwa mara kijana aliyefika 30+ kuoa pasi na kupepesa macho upande wa pili

Utakuta kijana akienda kusalimia kwao ana lazimishwa kuoa mpaka anaona nyumbani ni kero kweli kweli, ndugu wana mshambulia , dada zake ndiyo usiseme anakaliwa kakikao kabisa wakidai ni lini utatuketea wifi, wazazi wataseme unataka tufe ndiyo uoe kwa kweli hili jambo ni gumu sana.

Hii nguvu ukiifatilia sana haina tofauti na nguvu za uharibifu unamsukuma kijana kuoa,unamjaza stress na presha juu unatarajia nini si nikumuangamiza huku kwa makusudi kabisa.

Hebu njoeni mseme wenyewe kwa hawa wanawake wasasa hawa wazee na ndugu zetu wanatuchukuliaje sisi vijana wa 30+ ambao hatujaoa
 
Hakuna kitu nashukuru na kimenisaidia sana kama kuoa japo kabla nilikua naona magumashi,,,kikubwa Mungu akusaidie upate mtu muelewa mnaeendana maana changamoto hazikosekani na ukiwa na roho nyepesi unaweza ukataka kurudisha mpira kwa kipa,,,ila mke na mtoto ndo ambao kwa sasa wananipa nguvu ya kupambana
 
Ndugu kwa masikitiko makubwa.

Ipo nguvu iliyopo mioyoni mwa wazazi wetu, ndugu, jamaa na marafiki na hata wazee wetu kabisa ya kumlazimisha mara kwa mara kijana aliyefika 30+ kuoa pasi na kupepesa macho upande wa pili

Utakuta kijana akienda kusalimia kwao ana lazimishwa kuoa mpaka anaona nyumbani ni kero kweli kweli, ndugu wana mshambulia , dada zake ndiyo usiseme anakaliwa kakikao kabisa wakidai ni lini utatuketea wifi, wazazi wataseme unataka tufe ndiyo uoe kwa kweli hili jambo ni gumu sana.

Hii nguvu ukiifatilia sana haina tofauti na nguvu za uharibifu unamsukuma kijana kuoa,unamjaza stress na presha juu unatarajia nini si nikumuangamiza huku kwa makusudi kabisa.

Hebu njoeni mseme wenyewe kwa hawa wanawake wasasa hawa wazee na ndugu zetu wanatuchukuliaje sisi vijana wa 30+ ambao hatujaoa
Mnasingizia nguvu za giza siyo kweli moja ya sababu ni ugumu wa maisha, mtu aoe ataleaje familia kama walio oa na kuolewa wenyewe mambo yao hayaendi?
  1. Usiku kucha wajasiliamali na wafanya biashara wanalalamika biashara haziendi na baadhi wako humu wanatafuta waganga wakuwatengenezea nyotta
  2. Watumishi wa umma ndiyo hao wanachangishana vikoba huko still maisha hayaendi madeni lukuki, vitu vimepanda bei vipato haviongezeki
  3. Wakulima nao wanazalisha masoko yakipatikana wanapangiwa bei kandamizi na wapi wauze bidhaa na wapi wasipeleke hata kama bei ni nzuri.
  4. Wageni wanachukua nafasi za ajira ambazo zingefanywa na hao wanaolalamikiwa kutooa,
 
Wengine Huwa wameshawekwa wakfu kwenye madhabahu ya uchawi tokea wakiwa matumbuni mwa mama zao mfano waje kuzaa watoto watakaorithishwa uchawi.

Ukiona mzazi anauchagulia mke/Mme jiulize swali kwamba ana maslahi yapi kwa mke/Mme huyo?
Mkuu,
Kwanza kabisa hakuna uchawi.
Pili, suala la kuchaguliwa lilikuwa ni tamaduni fulani katika kabila fulani.

Mfano; kama mimi na wewe ni marafiki na tuna utajiri wa ngo’mbe ili kuendelea kudumisha urafiki na utajiri huo wewe utaniambia kwamba nionzeshe mtoto wako wakike kwa mwanangu wakiume.

Na nitafanya hivyo, na urafiki na ule utajiri utaendelea kuwepo katika cycle yetu.
 
Mnasingizia nguvu za giza siyo kweli moja ya sababu ni ugumu wa maisha, mtu aoe ataleaje familia kama walio oa na kuolewa wenyewe mambo yao hayaendi?
  1. Usiku kucha wajasiliamali na wafanya biashara wanalalamika biashara haziendi na baadhi wako humu wanatafuta waganga wakuwatengenezea nyotta
  2. Watumishi wa umma ndiyo hao wanachangishana vikoba huko still maisha hayaendi madeni lukuki, vitu vimepanda bei vipato haviongezeki
  3. Wakulima nao wanazalisha masoko yakipatikana wanapangiwa bei kandamizi na wapi wauze bidhaa na wapi wasipeleke hata kama bei ni nzuri.
  4. Wageni wanachukua nafasi za ajira ambazo zingefanywa na hao wanaolalamikiwa kutooa,
Dunia Hii Babaa Lukumbalukumba
 
Back
Top Bottom