Nguvu za giza zimevunja ndoa ya jirani yangu

Uliona tokea mwanzo, lakini hukutaka kuchukua hatua kwa kutaka kujua nini kitaendelea. Leo hii umeona mwisho wake ulivyo mbaya na unajutia kwa kusimulia kilichotokea... Hongera
 
Jamaa alikuwa anaishi vizuri na mkewe,wameoana kwa shangwe na furaha kubwa......wakabahatikiwa kupata mtoto mmoja katika ndoa yao.

maisha ya ndoa yalianza kubadilika baada ya rafiki yangu kuanza safari za kikazi mara kwa mara,ndipo shemeji akaanza tamaa za kimapenzi kwa kijana mmoja mkopesha vyombo kutoka kigoma.

Yule kijana alikuwa anafika karibu kila siku nyumbani kwa rafiki yangu,kwa kweli roho iliniuma sana aisee kuona dogo mshamba mshamba kutoka bush anakula mzigo wa maana sana tena wa jamaa yangu wa karibu,halafu sisi born town tupo tupo tunashangaaa.

Siku moja nimetoka zangu kibaruani jioni...nikasema ngoja nipite nikamjulie hali shem....dah! sikuamini nilichokiona kwa mboni safi za macho yangu kumkuta dogo wa kiha yupo chumbani kwa jamaa yangu wa karibu sana tunayeshirikiana kwa shida na raha...leo hii tunda lake lina liwa, mimi nikishuhudia aisee.....ikabidi nichukue maamuzi magumu ya kutaka kuingia moja kwa moja mpaka chumbani ili niweze kumuadabisha yule dogo kwa kipigo kikali,nafsi ikaniambia acha usije kuonekana nawe unahusika katika kutembea na mke wa rafiki yako niakondoka na majonzi makubwa sana moyoni safari hii niliapa nitamueleza jamaa yangu kila kitu baada ya kukaa kimya kwa muda kuona kama shemeji atabadilika baada ya kumkanya lakini wapi.

Nilipofika nyumbani usiku nikamwita wife nakumkanya tabia za kuwa na mazoea na hawa wakopesha vyombo wa hapa daslam...nashukuru wife alinielewa sana,nikawa najiuliza sijui nimwambie wife kuhusu sakata la mke wa jamaa yangu lakini roho ikawa inasita nikaamua kukausha kiume...nikavuta shuka nikasoma dua nikalala.

Asubuhi mapema nikiwa naelekea kibaruani nikaamua sasa nimpigie simu jamaa yangu kuhusu wife wake anavyomtendea ubaya ,kiasi kwamba hadi anadiriki kumleta mwanaume kwenye kitanda alichokinunua kwa pesa yake mwenyewe inatia uchungu sana....sijui shem alikosa nini jamani wanawake kwa nini mna hamridhiki?

Rafiki yangu ni kijana mtanashati aliyeajiriwa kwenye taasisi kubwa ya kifedha hapa nchini,kifupi ana maisha ya kipato cha kati amjenga nyumba,ana gari ya kutembelea ana miliki biashara kadhaa hapa mjini....kifupi pesa ya matumizi ipo,shemeji yangu ......................
Vijana wa siku hizi mnafeli sana! Nani alikwambia mwanamke anafuata nyumba na gari nyumbani kwenu? Jitafakarini sana!
 
Yule kijana alikuwa anafika karibu kila siku nyumbani kwa rafiki yangu,kwa kweli roho iliniuma sana aisee kuona dogo mshamba mshamba kutoka bush anakula mzigo wa maana sana tena wa jamaa yangu wa karibu,halafu sisi born town tupo tupo tunashangaaa.


HUYU MTOA MADA NI WIVU TU UNAMSUMBUA BAADA YA KUZIDIWA KETE NA MKOPESHA VYOMBO
 
shemeji yangu sijui alikosa nini kwa jamaa yangu mpaka akaamua kutoa penzi lote kwa kijana muuza vyombo,dunia ina mambo kama wasemavyo watu pori, baada ya mahusiano yasiyo na uhalali kuendelea kati ya shemeji na muuza vyombo ,ikabidi sasa nimchane laivu shemeji yangu anachokifanya si kizuri...aachane na muuza vyombo kwani habari zake zimeshaenea mtaani, kuwa sasa hivi anatembea na muuza vyombo,alichonijibu nilichoka kabisa yaani akasema kwamba jamaa yangu alimuoa kwa bahati mbaya tu na siyo taipu yake hawaendani kabisa hivyo niachane na mambo yasiyonihusu nikiendelea kumfatilia atanizushia kuwa nina mtaka kimapenzi.

Hakika nilihuzunika sana jinsi jamaa yangu anayvompenda sana mke wake..... na kufikia hadi kujisifia tunapokuwa tumechill kijiweni ,baada ya kutoka katika mahangaiko ya kila siku ya utafutaji wa riziki kuwa mke wake anampenda sana na hawezi kumsaliti na kutembea na mwanaume mwingine tofauti na yeye.

Baada ya siku kupita jamaa yangu alirejea nyumbani kwake akitokea kwenye ziara za kikazi katika mikoa tofauti tofauti hapa Tanzania.....habari alizokutana nazo mtaani nikwamba mke wake anatembea na muuza vyombo ,jamaa kwa jinsi alivyokuwa anamuamini mkewe kwa asilimia zote bado hakuamini aliyoyasikia kuhusu mkewe.

Siku moja tumekaa na jamaa yangu kijiweni kama kawaida nikaamua kumgusia kuhusu tabia ya mkewe kuhusu kutoka na muuza vyombo,jamaa alihamaki na kutaka kunipiga akasema mkewe hawezi msaliti hata siku moja kwani anampa kila kitu hakuna anachokikosa chochote anachokitaka kutoka kwake....sasa hali ilibadilika kutoka kucheka mpaka kubadilika mpaka kushikana mashati jamaa alinikaba kola la shati yangu mpka nikataka kukata moto!!nikaona isiwe kesi nikamuomba msamaha alivyoniachia nikaondoka zangu huku nahema na kijasho kikinitoka,,,nilipofika mbali kidogo nikamwambia "haya ninayokwambia utakuja kuamini na utanikumbuka" akasema potelea mbali wife hawezi fanya ujinga huo.

Yule dogo muuza vyombo alianzana na shemeji bila kutumia njia zozote za kishirikina au nguvu za giza....ilifikia kipindi jamaa yangu alikuja kukamata meseji walizokuwa wakitumiana kati ya mkewe na yule dogo,jumbe za kimahaba kweli kweli... aliumia sana na akaja kuamini yale maneno yangu niliyomwambia,pia habari alizokuwa anazisikia mtaani kuwa mkewe kasha kuwa jamvi la muha muuza vyombo!aliamua kuanza kumsaka yule dogo huku akitumia bastola kama silaha itakayo ondoa uhai wa yule dogo kwa kosa la kutmbea na mkewe,baada ya dogo kusikia jamaa anamtafuta ndipo akaamua kutumia nguvu za giza au uchawi wa kiarabu unaojulikana kama felek au falak kumpumbaza jamaa yangu pia yule mwanake ,mke wa rafiki yangu asijielewe kabisa na yeye afanye anavyotaka.

Dogo anatoka katika familia ambayo baba yao alikuwa mtaalamu na nguli wa uganga wa falak.....mzee huyu aliitumia taaluma hii kusaidia wenye matatizo,lakini baada ya kufariki wanaye wamerithi nakuitumia ndivyo sivyo tofauti na marehemu baba yao mfano hai ni tukio la huyu dogo na mke wa mtu.

Ilifikia hatua mpaka jamaa yangu akagundua dogo anakula mke wake lakini akawa hana la kufanya kwani alipumbazwa akili....dogo akawa anafanya anavyotaka kwa mke wake kama alimtolea mahari, aisee dunia gunia kwa kweli....roho inauma lakini hakuna cha kufanya,kama mwenye chake hana cha kufanya anabaki kulia lia, sisi jamaa tu tutafanya nini masikini.

Dogo aliamua kwenda nyumbani kwa jamaa yangu bila uoga wala aibu akamwita mke wa jamaa na mumewe akiwa ndani naye asifanye chochote,dogo akamwambia shemeji chukua begi na kila kilicho chako tuondoke,jamaa yangu akawa anamuomba dogo msamaha huku analia eti "dogo niachie mke wangu"shemeji alichukua begi lake wakaondoka na dogo, wakaondoka wakimuacha jamaa analia machozi!!!

Hadi leo hii naandika dogo anaishi na mke wa jamaa mkoani kwao kama mke wake na kisha zaa naye mtoto mmoja....tena dogo anaishi maisha ya kiswahili tu, na yule mwanamke humwambii kitu kuhusu penzi la gizani kutoka kwa muuza vyombo.

muhimu: Hili ni tukio la kweli limetokea mjini Dar es salaam.
 
Mazoea huleta majanga mkuu.
Nilishamwambia wife siku nikikuta umekopa chombo kwa Muha ndio itakuwa talaka yako.
Mwanamke lazima umwekee mipaka ili akikengeuka ajue kitakachompata.
Una hela unaacha wife wako akope viatu vya elfu 10 kwa Waha!!!
 
Hakuna pepo hapo bali jinsi Mme alivyoshindwa kumtishisha mkewe mpaka mke kaamua kuliwa na muuza vyombo
kuna nguvu ya ushirikina katika tukio hili soma post namba 31 nimemalizia tukio.
 
Pesa si kigezo cha mtu kuridhika wanaume wengi huzani mahitaji ya nje ndiyo kila kitu kwa mke wanasahau kwamba hivyo vitu hata kwao alikuwa anavipata hapo kafuatwa yeye si kingine lakini kujifanya yupo busy hata muda wakukaa na mke ni mchache misamaki ya kwenye frigi ndiyo inamtosha wanajidanganya sana. Wake zao wataliwa sana wasipo jirekebisha
Unasema kweli lakini wanawake wengine hawaridhiki na mwanaume mmoja mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom