Orodha ya Mizimu iliyoibiwa mkoani Kigoma

Kigoma Region Tanzania

JF-Expert Member
May 25, 2021
229
593
Je umewahi kusikia milango 7 ya kuzimu ya Ziwa tanganyika? sio hadithi za kusikika ni vitu ambavyo vipo na vinatendeka hadi sasa, tutaileta mada hiyo siku zijazo, leo tunazungumzia Mizimu iliyoibiwa hapa mkoani Kigoma.

Itakuchukua dk 12 kusoma taarifa za maajabu haya

Kwanza fahamu maana ya Mzimu ni nini?
Mizimu ni roho zilizoishi katika mwili kabla ya kuiaga dunia. Katika baadhi ya dini na mila inaaminika kuwa mizimu inaweza kuwa na faida kwa watu walio hai duniani na ina uwezo wa kuwasiliana nao kwa kutumia njia mbalimbali kufuatana na mazingira au utamaduni.

Kwa kifupi ni kwamba, Imani yetu sisi wa Africa katika dini zetu za jadi kabla ya Uislamu na Ukristo tulikua na imani ya (Mizimu). Lakini kila jamii ina namna yake ya pekee ya kuwaza na kushughulikia imani hizo, ndio maana kukawa na ibada ya Matambiko.

Tambiko "kutamba" au "kutambika" ni utekelezaji wa ada maalumu ili kutuliza mizimu, Mababu au Mapepo. Mara nyingi matambiko hufanyika kwa kuambatana na kafara. Baadhi ya makabila huweza kuchinja wanyama, wengine hutumia pombe na kadhalika. Kimsingi kafara linalotolewa katika tambiko hutegemea na kabila na mzimu husika. Kwa hapa Kigoma Matambiko ya Waha ni tofauti na matambiko ya Wamanyema.

Dhumuni la kutambika ni kupata baraka, kuponyesha maradhi, kuomba msaada, kutuliza mizimu, kuiridhisha n.k

Matambiko huwa hayaaminiki sana katika imani/dini kwani huchukuliwa kuwa ni ushirikina na kukufuru. Mara zote matambiko huaminika katika makabila kama Mila na desturi za jamii hizo.

Kila kabila huwa lina mizimu yake, na pia kuna mizimu ya asili kutokana na eneo husika: Kigoma kulikuwepo mizimu ya asili mbali na mizimu ya makabila yetu. (Mizimu ya asili ni ile ambayo haifungamani na kabila, ni roho za viumbe ambao hawakuwahi kuishi duniani).

Kuzimu ni wapi?
"Kuzimu" ni mahali ambapo watu huwasiliana na roho za watu waliofariki dunia hapo zamani. Kuna mizimu iliyoumbwa katika hali hiyo, yaani haikuwahi kuwa binadamu hapo kwanza. Sehemu zinapopatikna hizo roho ambazo hazikuwahi kuwa binaadamu ndio panaitwa 'Kuzimu'

Kwa hiyo, kuna imani ya mizimu ya aina mbalimbali: mizimu ambayo ni roho za watu waliokufa na mizimu ambayo haijawahi kuwa binadamu. Kwa kuwa mizimu ni roho, haina umbo maalumu, lakini ina uwezo wa kutokea katika maumbile tofauti tofauti kama vile mtu, mnyama, mdudu, mimea, au vitu visivyo na uhai. Huku kwetu Kigoma mti wa Mrumba ulitumiwa sana kama mti wa kiibada katika matambiko mengi.

Mizimu mizuri ni wahenga, yaani roho za watu ambao walipokuwa katika hali ya ubinadamu waliishi vizuri kulingana na tamaduni na matakwa ya jamii, walikuwa na sifa nzuri. Sasa ni mizimu mizuri ambayo hulenga kuilinda jamii au mtu mmojammoja dhidi ya matatizo. Hivyo, pale mtu anapokumbwa na matatizo wahenga humsaidia. Aidha, kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa jamii katika masuala mbalimbali kunatokana na uhusiano wao na wahenga.

Jamii inapaswa kufuata mila na desturi zake na kuepuka, kadiri iwezekanavyo, kuvunja miiko ya jamii kwa sababu kufanya hivyo kunawaudhi wahenga.

Mtu anayefuata kanuni zote hulindwa, hupata mafanikio na kuishi kwa amani ilhali yule anayekiuka mila na desturi hupatwa na majanga makubwa au anaweza kuiingiza jamii nzima katika matatizo kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wahenga kujitoa katika ulinzi na hivyo kuyaachia mizimu mibaya nafasi ya kufanya mambo mabaya, au wahenga wenyewe kutoa adhabu kwa jamii au kwa mtu mmojammoja.

Aidha, inasadikiwa kuna mizimu mibaya, ambayo malengo yao ni kuidhuru jamii na wakati mwingine hujitokeza kama pepo ambao huwaingia na kuwadhuru watu; Baada ya Uislamu na Ukristo kuenea barani Afrika kusini kwa Sahara yanatumika pia majina yanatokana na lugha ya Kiarabu kama mashetani au majini ambayo kwa asili yana maana tofauti.

Hao mizimu mibaya huwa na kinyume cha sifa hizo hapo juu, yaani walipokuwa binadamu waliishi katika hali isiyotakiwa katika jamii au inayochukuliwa kuwa ni ya kutia aibu, halafu kufa katika hali inayochukuliwa kuwa ni ya laana, Aidha, inasadikiwa kuwa baadhi ya mizimu mibaya hutokana na watoto ambao walikufa kabla ya kuzaliwa: hao huidhuru jamii kwa sababu huwa na hasira na hutaka kulipa kisasi.
Maana nyingine ni kwamba:

Mzimu ni nishati (energy), roho au haiba (personality) ya mtu ambaye amefariki dunia lakini Roho yake imekwama katika sehemu iliyo kati ya duniani (ulimwengu wa dunia) na mahali ambapo roho hiyo inatakiwa kwenda kuishi baada ya maisha ya hapa duniani kukamilika (ulimwengu usio onekana/ afterlife/ land of the souls).

Roho hizi zinakuwa hazijui kama zimekufa katika ulimwengu wa dunia ama hazitaki kuamini kama zimekufa katika ulimwengu wa dunia ama hazikubaliani na kifo chao katika ulimwengu wa dunia. Mara nyingi roho hizi huwa ni roho za watu ambao walikufa katika mazingira yanayo tatanisha kama vile kufa kwa kuuliwa bila sababu (cold blood), kutolewa kafara, ama kufa baada ya maisha ya msukuleni. Kwa ufupi hizi huwa ni roho za watu ambao walidhulumiwa haki yao ya kuishi hapa duniani.

Mizimu inaweza kujidhirisha na kuonwa na wanadamu katika namna tofauti tofauti kama vile mizimu huwatokea ndugu, jamaa na marafiki zao wakiwa katika maumbo ya sura zao wakati wanaishi duniani na mara nyingi huwatokea wakiwa na nguo walizo penda kuzivaa wakati wa uhai wao), sauti, harufu (hapa kwenye harufu mzimu unapo mtokea muhusika hujidhihirisha kwa harufu yake ya mwili (kila mtu ana harufu yake ya asili, watu huweza kuwatambua watu wao wa karibu kwa harufu zao za asili), ama pafyumu (katika pafyumu, mzimu utamtokea mtu kwa harufu ya marashi ambayo alikuwa anapenda kuyatumia wakati yupo duniani katika ulimwengu wa dunia. Wakati mwingine, mzimu huweza kuwatokea ndugu jamaa na marafiki zake kwa kuwashika.

Kwa ufupi mzimu huwa ni roho ambayo imewahi kuishi katika ulimwengu wa dunia kama mwanadamu ama mnyama.

TOFAUTI kubwa kati ya mizimu na mapepo ni kwamba, mizimu ni roho za watu ambao waliwahi kuishi hapa duniani kama binadamu ilihali mapepo (demon) ni roho ovu ambazo hazijawahi kuishi duniani kama wanadamu. Hivyo kuna mizimu mibaya na mizuri, mizimu inanguvu kubwa za kudhuru, kuponesha, kusambaratisha, kuunganisha, mzimu pia unaweza kutumika ukafanya kile unachokitaka wewe mwanaadamu ikiwa ni pamoja kuitumikisha kukufanyia kazi, kukutajirisha, kukuondolea matatizo n.k.

Inaaminika kwamba ni mizimu ambayo hutumika kukausha maji wakati wa ujenzi wa madaraja makubwa duniani na ndio sababu ndugu zetu wazungu hupendelea kuzifanya kazi hizo nyakati za usiku kwasababu kuna viumbe wanavitumikisha. Mfano wa hayo ni daraja maarufu nchini Ujerumani liitwalo ''Rokotzbrücke'' pia huitwa daraja la Shetani 'The Devil's Bridge' daraja hili lilijengwa na mizimu, kwani ilikuwa ngumu sana kwa wanadamu kujenga. Mizimu ilikubali kujenga daraja kwa kubadilishana na roho ya mtu wa kwanza kuvuka daraja hilo ndio atakua kafara.

Pia kuna mizimu inayotumika katika migodi,

Hapa chini ni orodha ya Mizimu ya asili inayosadikika imeibiwa kutokea Kigoma na imehamishiwa nchi za mashariki ya mbali na inatumikia huko kunufaisha jamii za huko.

1-Mzimu wa Rutale, (tangu uchukuliwe mzimu huu hakuna tena maajabu pale Rutale, yamebakia maji tu, mzimu kwasasa unafanya kazi nchi za watu). Kuthibitisha hilo, kwasasa Rutale hakuna tena masharti katika uchotaji wa maji tofauti na zamani masharti yalikua ni mengi na matukio yalikua ni mengi.

80842780_2580800962138936_6941215823818129408_n.jpg

2-Mzimu wa Tanganyika (Ziwa Tanganyika lina milango 7 ya kuzimu (ni mada tutakuja kuijadili siku za usoni), inasadikaka milango yote imefungwa, hakuna tena mawasiliano ya kufika huko tangu mzimu huo kuondolewa kwa upande huu wa Kigoma). Kuthibitisha hilo ni kwamba shughuli nyingi za kibiashara zinazotokana na maji kwasasa hazina tena faida kama zamani.

347642009_180047897984358_5482048583470318457_n.jpg

3-Mzimu Nondwa (Jiwe la Nondwa pale Kibirizi halina tena maajabu tangu mzimu wake kuibiwa na kuhamishwa). Ilikua ni marufuku bibi harusi kupitishwa akiwa amefunikwa kichwa karibu na jiwe la Nondwa.
Ili boti livuke hapo ni lazima Bibi Harusi afunuliwe kichwa. Jiwe Nondwa ndio Kizio cha Msingi cha miji ya mwambao wa kaskazini mwa Ziwa Tanganyika.

12919914_1759773280908379_6387385569138374597_n.jpg

4-Mzimu Mungonya (Uliwahi kuvuma lakini hausikiki tena tangu kunyakuliwa kwake)

241472988_3092976910921336_2870365029415739469_n.jpg

5-Mzimu wa Kalunga (Huu ni mzimu wa kabila la Wagoma na wabembe, waliusimika hapa Kigoma, wagoma waliutupa wabembe wakauchukua kwasasa upo ulaya) Kinyago cha Kalunga Huuzwa Kati ya dollar 100,000 mpaka Dollar 70,000. ni Mzimu unaofanya kazi hadi sasa huko Ulaya.

sunga-bembe-kalunga-helmet.jpg

6-Mzimu wa Jogoo (Ulipatikana kijiji cha Sibwesa eneo la rasini kwenye mawe, uliporwa miaka ya 1980) Ndio mzimu ulikua unaongoza mazao ya Ziwa (Samaki na dagaa mwambao wa Kigoma). Ulikua ukionekana mchana kweupe mfano wa mtu aliyesimama, na jogoo alikua akiwika eneo hilo. Inasemakana Mzimu huu uliwakimbia kutokana na tabia ya ushirikina kuzidi kijijini hapo, na baadhi husema mzimu huu uliibiwa.

361609302_668980765261659_6323778392540586273_n.jpg

7-Mzimu wa Kipampa (Huko Ujiji mzimu huu ulikua ukigeuza madarasa ya shule kuwa treni na kusafirisha watu nyakati za usiku (watu wenye siri za giza), kwa mujibu wa mashuhuda wachache waliwahi kusimulia. Mzimu huu ulifutika tangu miaka ya 1970. Shule ya msingi Ujiji na Kipampa zimewahi kutajwa katika sakata hili la ajabu.

320389253_1633131697120069_8989429523646009486_n.jpg

8-Upande wa Kigoma Kaskazini, Kibondo na Kasulu (Mizimu mingi imeibiwa huko na kusafirishwa nchi za mashariki ya mbali).

357718731_660437596115976_6436827436561582849_n.jpg

Mazingatio: Yaliyoandikwa hapa sio nadharia tu, yamethibitishwa na yameelezwa kutoka kwa wakongwe wa mji.
Picha hizo ni matukio ya uhalisia.
 
View attachment 2762698

2-Mzimu wa Tanganyika (Ziwa Tanganyika lina milango 7 ya kuzimu (ni mada tutakuja kuijadili siku za usoni), inasadikaka milango yote imefungwa, hakuna tena mawasiliano ya kufika huko tangu mzimu huo kuondolewa kwa upande huu wa Kigoma). Kuthibitisha hilo ni kwamba shughuli nyingi za kibiashara zinazotokana na maji kwasasa hazina tena faida kama zamani.

View attachment 2762701

3-Mzimu Nondwa (Jiwe la Nondwa pale Kibirizi halina tena maajabu tangu mzimu wake kuibiwa na kuhamishwa). Ilikua ni marufuku bibi harusi kupitishwa akiwa amefunikwa kichwa karibu na jiwe la Nondwa.
Ili boti livuke hapo ni lazima Bibi Harusi afunuliwe kichwa. Jiwe Nondwa ndio Kizio cha Msingi cha miji ya mwambao wa kaskazini mwa Ziwa Tanganyika.

View attachment 2762882

4-Mzimu Mungonya (Uliwahi kuvuma lakini hausikiki tena tangu kunyakuliwa kwake)

View attachment 2762883

5-Mzimu wa Kalunga (Huu ni mzimu wa kabila la Wagoma na wabembe, waliusimika hapa Kigoma, wagoma waliutupa wabembe wakauchukua kwasasa upo ulaya) Kinyago cha Kalunga Huuzwa Kati ya dollar 100,000 mpaka Dollar 70,000. ni Mzimu unaofanya kazi hadi sasa huko Ulaya.

View attachment 2762884

6-Mzimu wa Jogoo (Ulipatikana kijiji cha Sibwesa eneo la rasini kwenye mawe, uliporwa miaka ya 1980) Ndio mzimu ulikua unaongoza mazao ya Ziwa (Samaki na dagaa mwambao wa Kigoma). Ulikua ukionekana mchana kweupe mfano wa mtu aliyesimama, na jogoo alikua akiwika eneo hilo. Inasemakana Mzimu huu uliwakimbia kutokana na tabia ya ushirikina kuzidi kijijini hapo, na baadhi husema mzimu huu uliibiwa.

View attachment 2762885

7-Mzimu wa Kipampa (Huko Ujiji mzimu huu ulikua ukigeuza madarasa ya shule kuwa treni na kusafirisha watu nyakati za usiku (watu wenye siri za giza), kwa mujibu wa mashuhuda wachache waliwahi kusimulia. Mzimu huu ulifutika tangu miaka ya 1970. Shule ya msingi Ujiji na Kipampa zimewahi kutajwa katika sakata hili la ajabu.

View attachment 2762886

8-Upande wa Kigoma Kaskazini, Kibondo na Kasulu (Mizimu mingi imeibiwa huko na kusafirishwa nchi za mashariki ya mbali).

View attachment 2762887

Mazingatio: Yaliyoandikwa hapa sio nadharia tu, yamethibitishwa na yameelezwa kutoka kwa wakongwe wa mji.
Picha hizo ni matukio ya uhalisia.
Hakunaga kitu kinaitwa MIZIMU dunia hii watu mnaabudu viumbe wenzenu wanaozaliana ,wanakula na kufariki pia mnawaita mizimu.
 
Hata makanisani na misikitini mnaabudu viumbe wenzenu, kina Mohamad na Emanuel (Yesu) ni mizimu ya kigeni ndo maana haina msaada nanyi si bora kuabudu mizimu yetu.
 
Jiwe Nondwa hadi kesho ndipo yapo madhabau ya wachawi wanatumia kupondea vichwa vitoto vichanga.
Sawa na Lile jiwe la Bismarck la Mwanza zote zile ni madhabau za wachawi hadi kesho
 
Walijenga madaraja usiku kwa sababu hawakuwa na technology za kukaushia maji kama Sasa.Pia mambo ya expansion joint ilikua ni factor pia.
Siku hizi zipo technology za kukausha maji iwe ziwani au baharini ili kuweka nguzo
 
Back
Top Bottom