'Nguvu ya umma' kumstaafisha siasa za Kenya Raila Amollo Odinga...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,284
2,000
Akilala akiamka kwa takribani miaka 20 hivi, Raila Amollo Odinga amekuwa hafikirii kazi nyingine ila kuwa Raisi wa Kenya na kuhitimisha lile ambalo baba yake Odinga Oginga alishindwa kulifanya.........kuwa mjaluo wa kwanza kutawala Kenya.

Lakini wazungu wana msemo usemao........................"like father like son"...........................nasi bila ya kuachwa mbali hulonga................."mtoto wa nyoka ni nyoka tu"....................sababu zilizomzuia baba yake Raila kuongoza kenya sasa zimeshamiri na baada ya uchaguzi wa 2013 nguvu ya umma itatimiza uhaja huu ambao umekuwa unahitajika ili kuinusuru kenya kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hapa ninaambatanisha sababu 10 kuthibitisha mtazamo huu:-

1) Historia hujirudiarudia yenyewe.

Baba yake Raila aliombwa na Mkoloni mwingereza aongoze Kenya mpya lakini kwa kuelewa ya kuwa waliopigania uhuru wa Kenya ni wakikuyu kupitia Maumau na akina Jomo Kenyatta, Oginga alikataa na kudai hakuna kuongelea uhuru hadi Kenyatta afunguliwe kutoka jela. Kauli hiyo ndiyo iliyomsaidia Oginga kuukwaa umakamu wa uraisi na sababu yake kuu hakuwa na mikwaruzano na wakikuyu bali aliwaunga mkono kwenye azma yao ya kukamata dola. Oginga alipokosana na kenyatta basi hata hicho cheo alipokonywa mchana kweupe.
Fundisho hapo ni kuwa kama Raila angelikuwa ana mkakati madhubuti wa kuwa Raisi wa kenya alipaswa kujenga miundo mbinu za nguvu na wakikuyu badala ya kuwabeza kuwa ni wakabila kwa kudai huwa hawachagui mtu yeyote isipokuwa wa kabila lao................na kubeza michango ya wakikuyu kwa kudai katiba mpya ifute kenyatta day na kuiita mashujaa Day...............jingine ni kudai hela ya kenya inamuenzi Kenyatta kwa sababu ni mkikuyu au hata kutohudhuria siku ya kumbukumbu ya kifo cha kenyatta.........

2) Kuunguza madaraja ya kisiasa

Raila alikuwa kinara wa kumkataa Uhuru Kenyatta mwaka 2002 na hata kushawishi baadhi ya viongozi wa Kanu akiwemo Kalonzo Musyoka kuikimbia Kanu na kuisababishia maumivu makali. Pamoja na kufanikiwa kupata kuungwa mkono na wakalenjini katika chaguzi ya 2007 lakini aligombana na William Rutto na hivyo kushindwa kulinda muungano wao na sasa kumgharimu.

Hata akina Rafael Tuju ambao wanatoka kabila lake, Raila amekuwa akiwabughudhi kwa kisa hawamwuungi mkono yeye!
Machafuko ya kujaribu kumpindua Moi mwaka 1982 kwa kiasi kikubwa yalichochewa na Raila na wapo wanajeshi wengi nchini Kenya ambao amejenga nao uhasama kwa tukio hilo na kufanya kuwa ni vigumu kuungwa mkono na majeshi ya Kenya hususani vinara wajeshini...............

3) Kumuunga mkono Kibaki mwaka 2002 bila ya MOU inayoeleweka.

Hata juzi kwenye hafla ya kutangaza muungano wao, Kalonzo Musyoka alimlaumu Raila kwa kuingia makubaliano na kibaki bila ya MOU inayoeleweka na matokeo yake kibaki aliwatimua kazi pale walipokosana naye. Kama wangelikuwa na MOU Kibaki asingeligombea muhula wa pili kama alivyokuwa kawaahidi hapo awali na baada ya kipindi kimoja tajwa, umaarufu wa Raila mwaka 2007 ungelimwezesha kuwa Raisi.

4) Kumsaliti William Rutto Uwaziri mkuu.

Katika makubaliano ya Raila na Rutto mwaka 2007 yalikuwa Rutto lazima awe Waziri Mkuu. Sasa alipoona kaukosa uraisi badala ya kuheshimu makubalino yake na Rutto akamnyang'anya Rutto ugali wake......................kama Rutto angelikuwa waziri mkuu leo Raila angelikuwa ana nafasi nzuri ya kuwa Raisi kwa sababu kura zote za wakalenjini zingelikuwa za kwake..........na kwa kuwa waziri mkuu Raila kawapa nafasi wapiga kura kumpima na utendaji wake haujawafurahisha wengi........................angelijifunza hapa TZ ukimwondoa J.K Nyerere hakuna Waziri Mkuu ambaye aliwahi kuwa Raisi na sababu alitusaidia Sumaye pale alipokuwa anatoa hotuba yake ya mwisho kama Waziri Mkuu na kuwalaumu wabunge kumchukia wakidhani yeye ndiye anawasumbua kwenye majimbo yao..............................somo hapo ni kuwa uwaziri mkuu na mahali pa kumsaidia Raisi siyo mahali pa kujijengea umaarufu wa bei poa wa kuwa Raisi...................Lowassa angelijifunza hapo kama Kawawa alivyojifunza

5) Upendeleo wa ajira kwa ndugu zake (nepotism)

Moja ya mapungufu makubwa ya Raila ni kuwa bunge la Kenya limekuwa likihoji juu ya teuzi nyingi ambazo Raila amekuwa akizifanya serikalini ambazo zimekuwa za kupendelea ndugu zake wa karibu ambayo ni mbaya zaidi ya hata ya ukabila........................yaani hii ya Raila ni "nepotism".

Tatizo ni kuwa watu wanapokuhusisha na kuwabagua ujue kukuchagua wakati wakijua fika huna mpango wa kuwasaidia bali wewe sera yako ni kubeba ndugu zako tu, kukuchagua inakuwa vigumu sana........

6) Kumtegemea Obama na ICC kumpa Uraisi!

Huu ni sehemu ya upumbavu mkubwa kichwani mwa Odinga..........mara nyingi amekuwa akijifananisha na Obama wakati Obama hakulelewa kwenye misingi ya ukabila wa hapa Afrika...........amekuwa akihoji kwanini iwe rahisi kwa wazungu kumchagua mjaluo na Kenya inakuwa shida aisichojua wazungu hawakumchagua Obama kwa sababu ya Ujaluo wake bali kwa kukidhi vigezo vya mahitaji ya siasa za marekani..........period!

ICC imetumika kuwachafua Uhuru na Rutto kwa tuhuma ambazo zilipikwa na wafuasi wa Raila waliomo kwenye NGOs na KNHRC.................na wengineo tunawaona sasa wamekuwa wasemaji wakuu wa kampeni ya Raila na ODM............................tatizo la ICC ni kushindwa kuwafungulia mashitaka Kibaki na Raila. Vilevile ICC wameshindwa kutoa maelezo ya kina kwanini vurugu za Kibera ambako Raila ni mbunge na kisumu hazikufunguliwa mashitaka ICC pamoja na watu wengi kufa na kupoteza mali zao kwenye maeneo hayo? Koffi Annan na fisadi Ken Mkapa wanafikiri ya kuwa wanaweza kutumiwa na Marekani na Ulaya kuishinikiza Kenya kumchagua Raia kuwa Raisi na hivyo kibaraka wa nchi matajiri duniani ziendelee kulinyonya taifa hilo......................wasichojua walinzi wa mwisho wa utaifa wa Kenya ni wakikuyu kama vita vya maumau vinavyotufunza.......................makabila mengineyo aidha yalikaa kimya au yalimsaidia mwingereza kuzima vuguvugu la uhuru nchini humo.
Jana usiku kwenye taarifa ya habari ya saa 3 usiku kwenye luninga ya the CITIZEN, mbunge wa kuteuliwa mwanamama Shebeesh aligusia masuala haya ingawaje alikuwa akiilaumu Ikulu na kibaki kwa kutaka kushinikiza Uhuru aachie ngazi kwa Musalia Mudavadi...............

Uchaguzi huu utamkataa Amollo kwa kuwa ni kipenzi cha ukoloni mamboleo...........

7) Kumnyanyasa Makamu wa Raisi Kalonzo Musyoka.

Raila Odinga katika khali isiyo ya kawaida amekuwa akitumia muda mwingi kupigania "seniority" kati yake na Musyoka.......................akidai baada ya Kibaki ni yeye............nilimshangaa jana kwa mara ya kwanza tangia awe Waziri Mkuu alikwenda kumtembelea Kalonzo ofisini kwake......................siyo kwa sababu anamheshimu bali kumshinikiza awe namba mbili wake kwenye uchaguzi ujao!.............How pathetic!

Unapojikuza ujue Muumba atakushusha tu..........................na Raila katika kudai makuu sasa inabidi aoshe unyayo wa Kalonzo ambaye amekuwa akimdharau sana........................katika miaka 5 iliyopita................na uzoefu unaonyesha mwisho wa yote muungano wao utaishia pabaya kabla ya uchaguzi..................

8) Kuizuia demokrasia kufanya kazi yake ndani ya ODM

Hili linashangaza lakini ni ukweli. Musalia Mudavadi kisa ya kuikimbia ODM ni pale alipobaini katiba yao tayari ilimtamka Raila ndiye mwenye sifa za kugombea uraisi kupitia chama hicho bila ya kuweka utaratibu shirikishi, wazi na ambao utakuwa na misingi ya utu ya kumpata mgombea uraisi wa chama hicho......................

Sasa Musalia kajiunga na mahasimu wa Raila wakiongozwa na Uhuru na "majuto ni mjukuu..............:'

9) Saa ya "Kizazi kipya" imewadia.............

Kutokana na ukweli na bila ya kujali makabila yao, vijana nchini Kenya wamechoshwa na wazee na Raila ambaye ana umri wa miaka 73.............................hana mvuto kwa kizazi kipya...................huo ndiyo ukweli wake.............kuchaguliwa na hiki kizazi cha dot.com ni njozi ya kufikirika tu.........

10) kukabiliwa na kutetea watuhumiwa wa ufisadi.

Moja ya mvuto wa Raila ulikuwa anachukia ufisadi lakini la ajabu alipoingia kwenye meza kuu ya mlo amekuwa akitumia watoto wake kufanya ufisadi kama ule wa kashfa ya mahindi.....................watu walikuwa wanakufa na njaa Raila akaona kivuno kwake!

Swahiba wa Raila, Charity Ngilu alipokuwa kashikwa pabaya na taasisi ya kuzuia Rushwa nchini Kenya.............Raila alikuwa mstari wa mbele kumtetea bila ya kujali mabwawa kibao hayakuchimbwa au yalichimbwa kwa viwango vya chini na mabilioni kutoweka........na miradi ya maji ni nyeti sana katika kumkomboa masikini mnyonge kwenye ufukara wake................Raila alipokuwa upinzani alijiita ni "mkombozi wa wanyonge"................................lakini kila mmoja sasa anajua hizo zilikuwa ni ghiliba..........

HITIMISHO.

1) Kutokana na uchu wa madaraka wa taswira ya Amollo ni dhahiri ya kuwa ni nguvu ya wananchi ndiyo tu itamwondoa kwenye anga za siasa za kenya na Afrika haina muda mkubwa wa kulisubiria hili............kwa hamu kubwa.

2) Kustaafu kwa Raila kwenye anga za siasa za kenya kutapunguza sana misuguano ua kikabila nchini humo.........

Kabaridi

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
2,028
2,000

Lakini wazungu wana msemo usemao........................"like father like son"...........................nasi bila ya kuachwa mbali hulonga................."mtoto wa nyoka ni nyoka tu"....................sababu zilizomzuia baba yake Raila kuongoza kenya sasa zimeshamiri na baada ya uchaguzi wa 2013 nguvu ya umma itatimiza uhaja huu ambao umekuwa unahitajika ili kuinusuru kenya kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hapa ninaambatanisha sababu 10 kuthibitisha mtazamo huu:-

1) Historia hujirudiarudia yenyewe.

Baba yake Raila aliombwa na Mkoloni mwingereza aongoze Kenya mpya lakini kwa kuelewa ya kuwa waliopigania uhuru wa Kenya ni wakikuyu kupitia Maumau na akina Jomo Kenyatta, Oginga alikataa na kudai hakuna kuongelea uhuru hadi Kenyatta afunguliwe kutoka jela. Kauli hiyo ndiyo iliyomsaidia Oginga kuukwaa umakamu wa uraisi na sababu yake kuu hakuwa na mikwaruzano na wakikuyu bali aliwaunga mkono kwenye azma yao ya kukamata dola. Oginga alipokosana na kenyatta basi hata hicho cheo alipokonywa mchana kweupe.
Fundisho hapo ni kuwa kama Raila angelikuwa ana mkakati madhubuti wa kuwa Raisi wa kenya alipaswa kujenga miundo mbinu za nguvu na wakikuyu badala ya kuwabeza kuwa ni wakabila kwa kudai huwa hawachagui mtu yeyote isipokuwa wa kabila lao................na kubeza michango ya wakikuyu kwa kudai katiba mpya ifute kenyatta day na kuiita mashujaa Day...............jingine ni kudai hela ya kenya inamuenzi Kenyatta kwa sababu ni mkikuyu au hata kutohudhuria siku ya kumbukumbu ya kifo cha kenyatta.........

Rutashubanyuma
,

una historia nzuri ya Kenya tangu kupata uhuru...

....Naunga sehemu nyingi ya makala hii lakini kwenye red napinga kwa sababu kuna uzushi wa kupotosha ambao unasema Migawanyiko kati ya wakikuyu na wajaluo ulianza wakati wa kenyatta. Pia inaashiria Odinga hakupenda amani ambayo si sawa. Sababu zilizomfanya Odinga kushindwa kuongoza kenya hazifanani na zile zilizomzuia Raila. (nasistitiza).

....Odinga alikataa madaraka kutoka kwa mkoloni alipoona wakimpa sera zinazofanana na apartheid kuongoza kenya, ndipo makubaliano yakafanywa kumwachilia huyo kenyatta.

Haikumbukwi ya kuwa Odinga Snr. na Kenyatta Snr walikuwa na uhusiano mzuri katika uongozi na siasa hadi kifo cha marehemu Tom Mboya ilipowapiga butwaa. Jambo hili liliwagonganisha wawili hawa lakini haikubaki kwa muda. Yakua Odinga Snr. aliiweka tukio hilo nyuma yake na hata ingawa kukosana huku hakukuendelea kwa muda.

......Imesahaulika kuwa kunawiri kwa kenya kisiasa, kiuchumi nk kulitimia katika msingi wa uhusiano huu mzuri.

Ruwaza yake haikuwa kuleta migawanyiko kati ya wakikuyu na wajaluo, kinyume na mafikira ya wengi. Jambo hili ilimgharimu Odinga kustaafu siasa na madaraka ya VP chini ya kenyatta kwa kujitoa na kurudi nyumbani.

Ruwaza ya Odinga Snr ya umoja ndani ya taifa la kenya, ilikuwa yenye maana sana kwake akizingatia changa-moto na dhuluma nchi iliopitia chini ya wakoloni.

...........Mwanya huu wa mgawanyiko kati ya wakikuyu na wajaluo umepanuka baada la tukio la 82, na ndipo siasa za kenya zilichukua mkondo mbaya. Kukaongezeka siasa za chuki na ukabila na ubinafsi pamoja kati ya "kambi" hizi mbili, na kwa kuwa pia Odinga jr, aliambatanishwa na tukio hilo.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,284
2,000
Raila is no God but he doesn't deserve to be demonised like this either, i am sure everyone has his own faults.

Dhuks..........................demonized or this is what he is...................facts always hurt
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,284
2,000
Rutashubanyuma,

una historia nzuri ya Kenya tangu kupata uhuru...

....Naunga sehemu nyingi ya makala hii lakini kwenye red napinga kwa sababu kuna uzushi wa kupotosha ambao unasema Migawanyiko kati ya wakikuyu na wajaluo ulianza wakati wa kenyatta. Pia inaashiria Odinga hakupenda amani ambayo si sawa. Sababu zilizomfanya Odinga kushindwa kuongoza kenya hazifanani na zile zilizomzuia Raila. (nasistitiza).

....Odinga alikataa madaraka kutoka kwa mkoloni alipoona wakimpa sera zinazofanana na apartheid kuongoza kenya, ndipo makubaliano yakafanywa kumwachilia huyo kenyatta.

Haikumbukwi ya kuwa Odinga Snr. na Kenyatta Snr walikuwa na uhusiano mzuri katika uongozi na siasa hadi kifo cha marehemu Tom Mboya ilipowapiga butwaa. Jambo hili liliwagonganisha wawili hawa lakini haikubaki kwa muda. Yakua Odinga Snr. aliiweka tukio hilo nyuma yake na hata ingawa kukosana huku hakukuendelea kwa muda.

......Imesahaulika kuwa kunawiri kwa kenya kisiasa, kiuchumi nk kulitimia katika msingi wa uhusiano huu mzuri.

Ruwaza yake haikuwa kuleta migawanyiko kati ya wakikuyu na wajaluo, kinyume na mafikira ya wengi. Jambo hili ilimgharimu Odinga kustaafu siasa na madaraka ya VP chini ya kenyatta kwa kujitoa na kurudi nyumbani.

Ruwaza ya Odinga Snr ya umoja ndani ya taifa la kenya, ilikuwa yenye maana sana kwake akizingatia changa-moto na dhuluma nchi iliopitia chini ya wakoloni.

...........Mwanya huu wa mgawanyiko kati ya wakikuyu na wajaluo umepanuka baada la tukio la 82, na ndipo siasa za kenya zilichukua mkondo mbaya. Kukaongezeka siasa za chuki na ukabila na ubinafsi pamoja kati ya "kambi" hizi mbili, na kwa kuwa pia Odinga jr, aliambatanishwa na tukio hilo.
Last edited by Kabaridi; Today at 12:15.

Kabaridi hongera naona ni mfuatiliaji mzuri...........ila odinga Jnr aliandika kitabu cha maisha yake na katika mafanikio aliyojivunia nayo ni kuwashawaishi maafisa wa ngazi za chini wa kabila lake kumpindua Moi............it is his own admission not mine...
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,284
2,000
namwona Magufuli kavalia magwanda ya ODM kwenye huu mkutano wao...akipungua kofia yao....ana ajenda gani na ODM?
 
Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
2,000
Asante sana Ruta kwa taarifa hii kuhusiana na siasa za Kenya! Lakini penda usipende lazima zitapigwa tuu subiri na usikilizie hiyo March 2013!
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,058
2,000
Asante sana Ruta kwa taarifa hii kuhusiana na siasa za Kenya! Lakini penda usipende lazima zitapigwa tuu subiri na usikilizie hiyo March 2013!

kweli mkuu wakenya nawajua sana,ni wakatili sana,asa kwa jambo linalohusiana na masilah ya ukabila,lazima zipigwe tena
 
Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
2,000
Hawa watu kutoana Kisusio ni jadi! Lazima jamii ya Raila waingize Jando na sio ombi ni lazima!
 
mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,271
1,225
ndugu yangu RUT umeingea marefu na makuu kuhusu Raila na Kenya, ila nafikiri umekosea kwa kusema nguvu ya umma itamfanya raila astaafu baada ya 2013. hapo kwenye nguvu ya umma nina matatizo napo kwa sababu umma wa kenya hauko kama watz yaani na umoja. umma wa kenya ni kama kondoo waliogawanywa katika makundi madogo dogo kila moja na mchungaji wake...in other words politics in kenya are dominated by tribal kingpins who need to join other kingpins to gather enough "numbers" to continue influence the political arena..kibaki was a kikuyu afterthought, a lightweight candidate, a perennial loser, a guy who coulndnt take the fight to Kanu like Matiba, Rubia, and other kikuyu elites who joined the fight for second liberation in the late 80's. Kibaki in 2002 wasnt expected to do anything special other than loosing once more and retire.

All changed thanks to Moi contempt and arrogance in choosing "kamwana" as his successor, Kibaki got a political lifeline since he was deemed soft enough to push aside by his kingmakers-akina Raila, Ngilu, kalonzo, etc Raila lost in 97, and 2007, surely tribal arithmetic dont favor him this time around as he has lost the kalenjin voting block to Uhuru, but he will still remain a political patron in kenya as long as kenyan politics remains played in tribal chess board na hapa hamna huu umma utakaomua kua Raila sasa basi.
 
Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
2,000
Hata sijui kwa nini siasa za personalities za Kenya siwezi kufuatilia? yani zinanichosha ajabu. Huwa nashindwa kuamini, kama sio walala hoi kupewa kitu na hao mabepari, sidhani kama wote hawa wangekuwapo, au kama sio ukabila na udini uliokithiri, pesa ya kukufuru, kama wangekuwapo hawa wote.
Lakini nahisi kwa kutokusoma kwangu habari sao, huwa nakosa mengi ya maana.
 
Makendelu

Member
Sep 27, 2012
13
0
Mwandishi wa uzi huu ni mbumbumbu wa siasa za kenya

kweli kabisa mkuu,wakikuyu ndio walioleta ukabila hata ukiangalia kama sio Kenyatta kufia madarakani wakikuyu wangetawala kwa miaka mingi,Raila anaogopwa kutokana sera zake za kupambana na unyakuzi wa aridhi(land grabes) kwa mfano familia ya Kenyatta inamiliki aridhi ambayo ukiiweka kwa pamoja inalingana na mkoa wa nyanza,Moi na Ruto wamenyakua aridhi ya msitu wa mau ndo maana wanamchukia Raila coz anawapinga,angalia muungano wa Uhuru na Ruto ni kikabila ndo maana wabunge wa TNA ambao ni wakikuyu wamemkataa Mudavad lakini muungano wa cord una makabila yote.
 
SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,543
2,000
Let Kenyans make a statement and choose their own head of state through the ballot box instead of demonizing Raila and others in this forum. After all, who are you to speak on the behalf of the Kenyan voters?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom