Heaven Sent
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 32,717
- 98,377
Haha washakuzoea "mnyonya hela", kumbe hawakujui vizuri teh. Wanakuona wa sport sportEti najitoaga ufahamu, Heaven Sent mbona hujawahi niambia hili??
Haha washakuzoea "mnyonya hela", kumbe hawakujui vizuri teh. Wanakuona wa sport sportEti najitoaga ufahamu, Heaven Sent mbona hujawahi niambia hili??
Habari zenu wapendwa.
Leo kuna jambo limenigusa nikatamani sana kushare nanyi, haswa wanawake wenzangu(haswa wale midomo chuchunge)
Kuna baba ni jirani yangu amejiua baada ya kuhitilafiana na mkewe ( ilani tatizo la kipindi kirefu sana), kwakweli mwanamke ana kelele yule, akianza kumtusi mumewe majirani wooote mtasikia.
Sasa ikatokea mumewe akayumba kidogo kiuchumi, lakini mkewe hakutaka kuelewa na kumtuhumu kuwa ana michepuko(sina hakika kama kweli alikuwa nayo au la), hapo ndipo balaa lilipoanzia.
Mume akaamua kumshirikisha mkewe katika mapato yake, na wakafungua account ya pamoja, mke ndio mara nyingi alikwenda kudeposit pesa, ikatokea mume akapatwa na dharura ya kifamilia(kwao) akahitaji pesa, akamueleza mkewe kuwa anahitaji kiasi fulani cha pesa ili aende kwao, mke akaanza kelele.
Mume akaamua kwenda bank,cha ajabu akakuta account alotegemea ina zaidi ya milioni6 ina laki tu, akarudi kwa hasira na kumuuliza mkewe, akamjibu simple 'usinulize maswali ya kipuuzi',( haya ni maelezo ya rafiki wa mwanamke) ugomvi ulikuwa mkubwa hadi mume akaamua kuondoka nyumbani, na hakurudi mpaka kesho yake ilipofahamika kuwa mwili wake umekutwa nyumba ya wageni akiwa amejiua kwa kunywa sumu.
Jamani wanawake hii midomo yetu ina nini? Ni kwanini hatujifunzi kila siku!!!
Twapaswa kutambua kuwa tuna nguvu kubwa sana dhidi ya hawa wenzetu, mwanamke unauwezo wa kumfanya mwanaume masikini ajisikie na kujiona tajiri, lakini nguvu hiyo hiyo tukiitumia vibaya inaweza haribu kila kitu.
Tuwe basi watu wa kuwapa moyo na kuthamini wanachofanya hawa wenzetu, wanakazi kubwa sana na mzigo mkubwa sana walioubeba katika kuhakikisha tunapata mahitaji na mambo yote yanakuwa sawa. Tuwe faraja yao, tuishi katika misingi ya upendo,kujaliana na kuchukuliana kadiri ya mapungufu yetu.
Tujenge familia bora zenye misingi imara,maana watoto wetu sisi ndio role model wao wa kwanza(hii ni kwa wote wanaume na wanawake). Tusije shangaa watoto baadae wanakuwa watu wa ajabu ajabu kumbe wamerithi kutoka kwetu.
Muwe na usiku mwema.
usichelewe mapaparazi wengi humu miudenda inawatoka!Ooooh!!! Vere suni.
Hayo mambo kwako ni madogo?hey paul
mtu unakunywaje sumu kwa mambo madogo hivo eti?
Ingekuwa mimi nisingejiua, ningemwacha tu huyo mwanamke na kila kitu nitafute pesa zangu na Mwanamke mwenye roho nzuri zaidi yake.jamaa kama hakuwa boya basi mwanamke alimchezea akiri, yaan kajiua harafu kamwacha mal.aya wake anakula maisha na njemba zingine!
Manabii Uchwara au?Unasali kwenye yale makanisa ya manabii???
Kabisaaa.Huyo mwanamke nahisi ni mchaga
Ndugu, maneno yake ya pesa humu ni kufurahisha ukumbi tu...Dah yaani siku nikiona mwanamke wangu kaandika haya maneno na akayaishi hakika nitaamini mimi ni Mwanaume niliyebarikiwa kuliko wanaume wote hapa duniani.
Duh kumbe wewe huwa unajitoaga tu ufahamu ila una akili, hekima na busara hivi.
Aiseee!!!The same. Jamaa analikuwa na mke wake wakipendana sana Uchumi wa mume ukayumba sana. Mke akamtuhumu kwamba ana nyumba ndogo na anasaidia upande kwa wazazi wake. Baada ya Ugomvi kuwa mkubwa na kuzalilishana. Mume akaamua kuweka suruhu (si unajua kukwepa aibu ya maugomvi na makelele) akaamua kila kipato kinachoingia nyumbani kitahifadhiwa na kitatumika kwa maamuzi ya pamoja(wana Nyumba na frem za maduka) pesa zikawa nyingi na kuaamua kwa pamoja kukarabati nyumba yao(ukarabati mkubwa kama shs mil.5) ili kukwepa lawama mume akawa mtendaji mke ni mtunza pesa (pesa zote walihifadhi nyumbani na walificha sehemu flani waliokubaliana) kazi ikaenda ikaenda wakati ikikaribia kuisha mume akiwa amewafanyisha kazi mafundi anaomba pesa kwa ajili ya vifaa na fundi mke akamwambia hakuna pesa imeisha alipo enda kucheki pale zinapokuwepo hakuna kitu na kwa hesabu zake balance ilikuwa kama mil. 2 na zaidi.
Ugomvi ukafumuka upya mpaka ngumi kabisa na kuumizana. Yule Mke akamwambia wazi pesa imeisha na hakuna fanya ufanyalo. Jamaa akawa mpole lakini akaazimia yeye mwenyewe yafuatayo
1. Pesa yote ya nyumba itagawanywa nusu kwa nusu na ikitokea kuna hitaji ya pesa huyu anatoa nusu na mke nusu.
2. Miradi yote mipya ya Mume ataijua yeye tu na kipato chake,Mke hakijui.
3. Mke akimwaga Mboga, Yeye atamwaga ugali.(katika pesa za familia)
Sasa hivi jamaa wanaishi vizuri bila shida yeyote raha mstarehe mke akijua Mume amenyooka/ameshika adabu (si unajua ndiyo malengo yao siku hizi kuzibiti mume) lakini nyuma ya pazia kuna mambo.
Wanawake siku hizi mna nini? Muda mwingi mnatumia kugombana na waume zenu, haya majamaa yana akili za ziada. tulieni nao.
Ukitaka kula pesa ya mume wako mtii tu, na Mume ukitaka mafanikio kwa mke wako mpende tu.
Kitu kikubwa sasa hivi Kila mwanamke anataka kuwa mjasiriamali.
Naomba niwe wazi kabisa Mimi ninachukia sana hizi SACCOS natamani na mimi malaika ashuke azifute zote, maana zinawasumbua wanawake, wanachanganyikwa akili, wanaibiwa, wanahangaika kwa kudanganywa na hizi saccos. Kuna mwalimu wangu wa uchumi aliniaambia nikiwafundisha mfumo wa Interest za Saccos hakuna mtu atakaye kwenda kukopa saccos akiwa anamaanisha ni wezi na vigumu sana mtu kutoka (wapo wanafanikiwa 10% kati ya 90% wao hangaika tu bila kufanikiwa).
Any way jamaa alikosea kujinyonga, Hawa watu ni kuishi nao kwa akili. Si unajua siku hizi kuna Dawati la jinsia, sijui haki ya mwanamke, haki sawa ya mtoto na mama nk. dawa tu ni Kuishi na Mke kwa AKILI.
Da nimevutiwa na mtoa mada wewe ni mmoja kati ya wanawake wanaoelewa wajibu wao mungu akuzidishieHabari zenu wapendwa.