Nguvu ya mwanamke


espy

espy

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Messages
53,882
Likes
68,669
Points
280
espy

espy

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2013
53,882 68,669 280
Habari zenu wapendwa.

Leo kuna jambo limenigusa nikatamani sana kushare nanyi, haswa wanawake wenzangu(haswa wale midomo chuchunge)

Kuna baba ni jirani yangu amejiua baada ya kuhitilafiana na mkewe ( ilani tatizo la kipindi kirefu sana), kwakweli mwanamke ana kelele yule, akianza kumtusi mumewe majirani wooote mtasikia.

Sasa ikatokea mumewe akayumba kidogo kiuchumi, lakini mkewe hakutaka kuelewa na kumtuhumu kuwa ana michepuko(sina hakika kama kweli alikuwa nayo au la), hapo ndipo balaa lilipoanzia.

Mume akaamua kumshirikisha mkewe katika mapato yake, na wakafungua account ya pamoja, mke ndio mara nyingi alikwenda kudeposit pesa, ikatokea mume akapatwa na dharura ya kifamilia(kwao) akahitaji pesa, akamueleza mkewe kuwa anahitaji kiasi fulani cha pesa ili aende kwao, mke akaanza kelele.

Mume akaamua kwenda bank,cha ajabu akakuta account alotegemea ina zaidi ya milioni6 ina laki tu, akarudi kwa hasira na kumuuliza mkewe, akamjibu simple 'usinulize maswali ya kipuuzi',( haya ni maelezo ya rafiki wa mwanamke) ugomvi ulikuwa mkubwa hadi mume akaamua kuondoka nyumbani, na hakurudi mpaka kesho yake ilipofahamika kuwa mwili wake umekutwa nyumba ya wageni akiwa amejiua kwa kunywa sumu.

Jamani wanawake hii midomo yetu ina nini? Ni kwanini hatujifunzi kila siku!!!
Twapaswa kutambua kuwa tuna nguvu kubwa sana dhidi ya hawa wenzetu, mwanamke unauwezo wa kumfanya mwanaume masikini ajisikie na kujiona tajiri, lakini nguvu hiyo hiyo tukiitumia vibaya inaweza haribu kila kitu.

Tuwe basi watu wa kuwapa moyo na kuthamini wanachofanya hawa wenzetu, wanakazi kubwa sana na mzigo mkubwa sana walioubeba katika kuhakikisha tunapata mahitaji na mambo yote yanakuwa sawa. Tuwe faraja yao, tuishi katika misingi ya upendo,kujaliana na kuchukuliana kadiri ya mapungufu yetu.

Tujenge familia bora zenye misingi imara,maana watoto wetu sisi ndio role model wao wa kwanza(hii ni kwa wote wanaume na wanawake). Tusije shangaa watoto baadae wanakuwa watu wa ajabu ajabu kumbe wamerithi kutoka kwetu.

Muwe na usiku mwema.
 
MO11

MO11

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Messages
16,780
Likes
21,936
Points
280
MO11

MO11

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2014
16,780 21,936 280
Marehemu kichwa cha juu kilikua kibovu
 
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2014
Messages
10,005
Likes
6,091
Points
280
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2014
10,005 6,091 280
kuna watu wana roho za paka hivi wanawake tuko VIP? hiyo yote kisa mwanaume kataka pesa kwenda kwao??

wanawake Tuwapende wazazi upande Wa Pili ndo wanatuletea duniani wanaume. .wenye vitabia hivi acheni roho mbaya
 
dyuteromaikota

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Messages
4,120
Likes
3,664
Points
280
dyuteromaikota

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2013
4,120 3,664 280
jamaa kama hakuwa boya basi mwanamke alimchezea akiri, yaan kajiua harafu kamwacha mal.aya wake anakula maisha na njemba zingine!
 
KENZY

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
7,110
Likes
6,477
Points
280
Age
23
KENZY

KENZY

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
7,110 6,477 280
duh! huku mwishoni umenena kwa hisia! ha ha ha leo umekula nini..?
 

Forum statistics

Threads 1,274,979
Members 490,865
Posts 30,529,417