Nguvu ya mwanamke

Nguvu ya mwanamke

Nimefarijika kuona mwanamke akiwaasa wanawake wenzie kama hivyo. Ila huyu jamaa hakufanya kitu cha maana ingawa kesha kwenda ila yaonekana tayari alikuwa kaivuka hatua ya Msongo wa mawazo mpaka kwenye Sonona
 
atoto nataka kujua huyo mama baada ya kupata taarifa za kifo cha mumewe alikuwa kwenye hali gani.
 
Sasa hivi amekosa mume, atakosa na pesa..atalea watoto mwenyewe na amebaki kuwa single mother.
 
Wewe Atoto toka lini ukawa na ushauri mwema kwa jamii?,wewe ni muharibifu na tena mgonga nyoka mzuri sana weye au unakataa?,na ukibisha mimi nitatoa ushahidi wa yote uliotendea wanaume plus picha kama ushahidi au unabisha?,acha zako bhana,wewe ni miongoni mwa wachuna ngozi na wanyonya damu bila huruma weye au unabisha?,usiache nikakuanika jukwaani na kufanya ukonde bureee,please kaa kimya kabisa,usinikumbushe machungu ulonifanyia weye ajuza,.,.,..,.nitaendelea wanajamii wakinitaka kufanya hivyo,na tena nitatoa ile siri siku ile liliposanuka na bwana wako mpaka ukachezea makofi kefule weye,au unabisha nitoe au nisitoe? eti Atoto kumbe jina lake ni kama jinamizi eboo?
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Hizi ni stress au nini ndugu!!!
 
Habari zenu wapendwa.

Leo kuna jambo limenigusa nikatamani sana kushare nanyi, haswa wanawake wenzangu(haswa wale midomo chuchunge)

Kuna baba ni jirani yangu amejiua baada ya kuhitilafiana na mkewe ( ilani tatizo la kipindi kirefu sana), kwakweli mwanamke ana kelele yule, akianza kumtusi mumewe majirani wooote mtasikia.

Sasa ikatokea mumewe akayumba kidogo kiuchumi, lakini mkewe hakutaka kuelewa na kumtuhumu kuwa ana michepuko(sina hakika kama kweli alikuwa nayo au la), hapo ndipo balaa lilipoanzia.

Mume akaamua kumshirikisha mkewe katika mapato yake, na wakafungua account ya pamoja, mke ndio mara nyingi alikwenda kudeposit pesa, ikatokea mume akapatwa na dharura ya kifamilia(kwao) akahitaji pesa, akamueleza mkewe kuwa anahitaji kiasi fulani cha pesa ili aende kwao, mke akaanza kelele.

Mume akaamua kwenda bank,cha ajabu akakuta account alotegemea ina zaidi ya milioni6 ina laki tu, akarudi kwa hasira na kumuuliza mkewe, akamjibu simple 'usinulize maswali ya kipuuzi',( haya ni maelezo ya rafiki wa mwanamke) ugomvi ulikuwa mkubwa hadi mume akaamua kuondoka nyumbani, na hakurudi mpaka kesho yake ilipofahamika kuwa mwili wake umekutwa nyumba ya wageni akiwa amejiua kwa kunywa sumu.

Jamani wanawake hii midomo yetu ina nini? Ni kwanini hatujifunzi kila siku!!!
Twapaswa kutambua kuwa tuna nguvu kubwa sana dhidi ya hawa wenzetu, mwanamke unauwezo wa kumfanya mwanaume masikini ajisikie na kujiona tajiri, lakini nguvu hiyo hiyo tukiitumia vibaya inaweza haribu kila kitu.

Tuwe basi watu wa kuwapa moyo na kuthamini wanachofanya hawa wenzetu, wanakazi kubwa sana na mzigo mkubwa sana walioubeba katika kuhakikisha tunapata mahitaji na mambo yote yanakuwa sawa. Tuwe faraja yao, tuishi katika misingi ya upendo,kujaliana na kuchukuliana kadiri ya mapungufu yetu.

Tujenge familia bora zenye misingi imara,maana watoto wetu sisi ndio role model wao wa kwanza(hii ni kwa wote wanaume na wanawake). Tusije shangaa watoto baadae wanakuwa watu wa ajabu ajabu kumbe wamerithi kutoka kwetu.

Muwe na usiku mwema.

Dah yaani siku nikiona mwanamke wangu kaandika haya maneno na akayaishi hakika nitaamini mimi ni Mwanaume niliyebarikiwa kuliko wanaume wote hapa duniani.

Duh kumbe wewe huwa unajitoaga tu ufahamu ila una akili, hekima na busara hivi.
 
Story imeelemea ushahidi wa upande mmoja na huyu mwanamke anaonekana kama ''shetani''.Ni vizuri umetoa ''maangalizo'' kadhaa kuonesha maoni uliyotoa si conclusively...Matukio kama haya huwa na ''hearsay'' za kutosha kiasi cha kushindwa kutoa hukumu sahihi.....
Its true.
Nimeongea kinachoongelewa haswa na marafiki wa mwanamke, ila sina uhakika, ila kwakuwa ni jirani na matusi nilikuwa nikiyasikia maana akianza kutukana majirani wote mtasikia, ila hayo mengine sina uhakika nayo.

Sema pia jambo likishatokea kila mtu huongea lake, cha msingi ni kukumbushana kuchunga midomo yetu na namna bora ya kulea familia zetu.
 
Labda kuwasaidia wanaume mmeumbwa na silaha moja ya uwezo wa kudharau mambo ukijifanya kusikiliza kila kitu lazima ufe,kamuulize baba au babu yako
Mie sio mwanaume mpendwa.
 
R. I. P
rest in power..


Ni Mara mia angemuua mkewe kwa kumtilia Sumu akafa,
Kuliko kujiua yeye mwenyewe kwa kunywa sumu ameonesha udhaifu sana na kutudhalilisha wanaume.

Mwanaume ndio kichwa cha familia, mwanaume hupaswa kuonesha msimamo wake,
Mwanaume hutakiwa kupambana na changamoto ya aina yeyote atakayo kutana nayo maishani mwake.
Ni kweli ila watu wanatofautiana ndugu yangu.
 
atoto nataka kujua huyo mama baada ya kupata taarifa za kifo cha mumewe alikuwa kwenye hali gani.
Its obvious, alikuwa akilia saaana na polisi walimchukua kwa mahojiano, bado sijajua nini kiliendelea.
 
Dah yaani siku nikiona mwanamke wangu kaandika haya maneno na akayaishi hakika nitaamini mimi ni Mwanaume niliyebarikiwa kuliko wanaume wote hapa duniani.

Duh kumbe wewe huwa unajitoaga tu ufahamu ila una akili, hekima na busara hivi.
Eti najitoaga ufahamu, Heaven Sent mbona hujawahi niambia hili??
 
Back
Top Bottom