Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 366,008
- 846,087
Katika maisha yangu nimeshuhudia watu wane wenye sauti zilizobeba mamlaka... Akisema neno hapa mirindimo yake huenda mbali sana halafu wala hatumii nguvu na wala mishipa ya shingo haimsimami wala hakunji sura... Lakini utahisi uzito na mamlaka.... Watu hao ni Mzee Mshana snr.. RIP ⚰, Mzee Mchonga meno RIP ⚰, Mzee wa kirachacha na Mkuu EL..!
Roho ni kitu kisichoonekana kwa macho wala kwa darubini wala kwa hadubini.. Lakini nguvu yake ni kubwa na isiyomithilika... Ni katika nguvu hiyo ya roho kuna nguvu chanya na kuna nguvu hasi... Chanya hukuletea matokeo mazuri, hasi hukuletea matokeo yenye uharibifu
Tunapolala usiku vitandani mwetu... Kinacholala ni huu mwili wa nyama lakini kamwe roho ndani ya mwili hailali hukesha ikikulinda... Ukiona kuna jambo baya limekupata usingizini jua tu roho yako ilipitiwa ama iliruhusu jambo husika likupate kwakuwa ilishaona hakuna madhara makubwa.. Lakini pia kuna roho ziko dhaifu kiimani
Nguvu ya kukemea huambatana na imani katika nguvu kuu nguvu kuu inayotawala ulimwengu wote... Imani juu ya nguvu husika hubeba uhai na mamlaka....!!!! Linapokujia jambo baya usiku la vinyamkera majinamizi, roho wachafu wanga nk... Ukikemea kwa dhati ya moyo na kwa jina kuu lilipatalo majina yote... Roho hizo hutii mamlaka hayo na kutoweka....
Nguvu ya kukemea kwa jina kuu lipitalo majina yote hubeba silaha za MAANGAMIZI na ndio maana hata shetani na mawakala wake huiogopa na kutimua mbio akikuacha salama salimini
Unapojiandaa usiku huu kupanda kitandani mwako usisahau kufanya maombi. Kwakuwa kuna nguvu katika maombi hasa UKIAMINI....