Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,405
1. Alipewa mwanadamu,mnyama zake
ni pungufu.
Toka zama zama damu,zama zisizo
na harufu.
Wote twende zamu zamu,ndivyo ataka
raufu.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
2. Ngumi yako ukunjapo,vyema kunjia
kichwani.
Hata teke urushapo,usitole kifuani.
Pia kichwa upigapo,nguvu toa
ubongoni.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
3. Mwenye maono shupavu,nguvu yao
maarifa.
Ila waso wasikivu,waenda poteza sifa.
Wamekufa wawajivu,na zimeoza
nyadhifa.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
4. Wamekwisha tamatisha,mwisho
wao umefika
tamati washafikisha,tena
hawatosikika.
Walichofanya chatisha,kinakwenda
tamatika.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
5. Mwenye nguvu hatoshinda,mwenye
akili ni bingwa.
Hata awe kama kinda,magoli hawezi
fungwa.
Harufu iliyovunda,kwa kamba
haitofungwa.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
Shairi=NGUVU MWISHO WA AKILI.
Mtunzi=IDD NINGA wa Tengeru
Arusha.
iddyallyninga@gmail.
com
ni pungufu.
Toka zama zama damu,zama zisizo
na harufu.
Wote twende zamu zamu,ndivyo ataka
raufu.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
2. Ngumi yako ukunjapo,vyema kunjia
kichwani.
Hata teke urushapo,usitole kifuani.
Pia kichwa upigapo,nguvu toa
ubongoni.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
3. Mwenye maono shupavu,nguvu yao
maarifa.
Ila waso wasikivu,waenda poteza sifa.
Wamekufa wawajivu,na zimeoza
nyadhifa.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
4. Wamekwisha tamatisha,mwisho
wao umefika
tamati washafikisha,tena
hawatosikika.
Walichofanya chatisha,kinakwenda
tamatika.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
5. Mwenye nguvu hatoshinda,mwenye
akili ni bingwa.
Hata awe kama kinda,magoli hawezi
fungwa.
Harufu iliyovunda,kwa kamba
haitofungwa.
Nguvu mwisho wa akili,wajinga
hawatambui.
Shairi=NGUVU MWISHO WA AKILI.
Mtunzi=IDD NINGA wa Tengeru
Arusha.
iddyallyninga@gmail.
com
Last edited by a moderator: